Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu TPA, Deusdedit Kakoko aachiwa kwa dhamana baada ya TAKUKURU kukamilisha Uchunguzi dhidi yake kwa 98%

Hii ndio taarifa ya TAKUKURU iliyotolewa kwa vyombo vya habari , na kwamba hizo 2% zilizobaki zitakamilishwa na ofisi ya CAG

Hakuna Taarifa kama atafikishwa Mahakamani au la .

Tuendelee kufuatilia .

Pia soma
Kuna watuhumiwa wa uhujumu uchumi wako rumande wengine kwa miaka mitano sasa na hakuna kinachoendelea dhidi yao, ushaidi wa kishamba tu usio na mashiko, mbona hawajapewa dhamana?
 
Huyo Kakoko ndio keshaachiwa huru msihangaike kujipa moyo, ila wewe polisi chukua rushwa ya elfu thelathini ukamatwe ndio utajua hii nchi ina sheria.
Hakuna kesi hapo watayamaliza juu kwa juu
Ushawahi ona au sikia mtu aliyepiga pesa za umma na mali akafungwa
Akifungwa basi huyo mfumo haumkubali

Ova
 
Karne ya 21 kwanini tuendelee kuongozwa na viongozi wanaoangukiwa na uongozi kama Unabii?
Hapo utakua unapropose tuongeze somo la Urais kwenye mitaala yetu.

Mawazo ya bavicha huwa hayatofautiani sana.
 
Magufuli aliupata uRais kwa Zali/hakujiandaa. Samia naye ameupata Urais kwa zali pia, hakujiandaa.
Tuendapo ni Mungu anajua.
Ulitaka Rais Samia afanye nini kwenye hili? Aagize kuwa Deus Kakoko atupwe ndani kwa uhujumu uchumi?

Samia anachofanya ndiyo Utawala wa Sheria tuliokuwa tunaulilia kwa Mwendazake.
  • Unamtuhumu mtu
  • Anachunguzwa na chombo/ time
  • Chombo kikijiridhisha kuwa kuna sababu za kutosha kufungua mashtaka, kinafungua


Siyo kutumbua tumbua watu HOVYO
 
Magufuli aliupata uRais kwa Zali/hakujiandaa. Samia naye ameupata Urais kwa zali pia, hakujiandaa.
Tuendapo ni Mungu anajua.
Ninakubaliana na wewe.

Lakini swali ni: Kuna kujiandaa kwa vipi kuwa rais? Kuna kozi au shule?

Sawa, tukubali, kwa watu kama Billy Clinton wa Marekani waliotamani kuwa marais wangali wadogo, lakini kweli walijiandaa?

Nani alijiandaa kwa kufanya nini na nini, kabla ya kuukwaa urais?
 
Huyu Mzalendo aliyetufanya tukajua maovu yaliyokuwa yamefichwa kwenye mkataba wa mradi wa bandari ya Bagamoyo ndio anateswa kiaina. Aliyo yasema hayafutiki lakini, mjue hilo.
Chnzo cha Kakoko kusurubiwa ilikuwa ni Bandari ya Machina wa Bagamoyo!
Hakika Mungu ni Mwema!
 
Njia aliyopitia Magufuli kuingia Ikulu ndiyo iyo kapitia Samia mimi sioni jipya nje ya huruma ya kimama maana kila alilotenda uyu mwenda zake wizi mauaji nk vyote mama alikuwepo lakini alikaa kimya ila simlaumu maana kama angejiuzulu kupisha ufedhuli wa nduli mwenda zake asingepata hii nafasi lakwangu namwombea afate sheria na kupeleka sheria kandamizi bungeni zifanyiwe marekebisho.
Ayo ya Malekani waachie ao matajiri na mimi nataka niwe tajiri kwenye mtaa wangu.
 
Ninakubaliana na wewe.

Lakini swali ni: Kuna kujiandaa kwa vipi kuwa rais? Kuna kozi au shule?

Sawa, tukubali, kwa watu kama Billy Clinton wa Marekani waliotamani kuwa marais wangali wadogo, lakini kweli walijiandaa?

Nani alijiandaa kwa kufanya nini na nini, kabla ya kuukwaa urais?
Kiongozi yoyote ana kazi kuu kama 3 hivi;
1-kurekebisha ya nyuma
2-kutengeneza ya wakati uliopo
3-kuandaa njia kwa mrithi wake.
Si Magufuli wala Samia aliyekuwa amejipanga kwa kushika uongozi.
 
Kiongozi yoyote ana kazi kuu kama 3 hivi;
1-kurekebisha ya nyuma
2-kutengeneza ya wakati uliopo
3-kuandaa njia kwa mrithi wake.
Si Magufuli wala Samia aliyekuwa amejipanga kwa kushika uongozi.
Mimi sikatai, kwa hao wawili kutokuwa tayari kwao kuwa marais; na hasa kwa huyu aliyepo sasa kwenye urais, kwa sababu hakutegemea kabisa kwamba angeshika cheo hicho.

Kwa mtu anayetafuta nafasi kama ya urais, labda tuseme kujiandaa kwake ni kuwa katika siasa na kushika nafasi za ngazi mbalimbali, huku akijijenga atambulike kwa wenzake na wananchi kwa kuwa na misimamo juu ya mambo yanayohusu serikali na nchi kwa ujumla.

Atakuwa ameshika nyadhifa na kufanya maamuzi muhimu juu ya mhimu yanayoihusu nchi.

Kiufupi niseme, mtu huyo atakuwa amejijengea historia inayomtambulisha kwa wenzake na kwa raia.

Mtu huyu pia atakuwa amekwishaonyesha sifa ya kuwa na maono ya nini kifanyike juu ya hatma ya nchi anayotaka kuiongoza.

Haya yote ndiyo yatakayomtambulisha kwa wenzake na wananchi kuwa yeye ni kiongozi na atakapofanya kampeni za uchaguzi atayasisitiza haya, na hatimaye wananchi wanampa ridhaa ya kuwaongoza.

Katika hawa wote tunaowazungumzia hapa, hakuna hata mmoja aliyepitia hatua hizo.

Kwa hiyo tunaweza kusema...Hawakujiandaa.
 
Back
Top Bottom