Aliyekuwa Mhasibu wa Tanroads Ruvuma, Justin Rwendera adaiwa kujiua kwa kujipiga risasi

Miliki kila aina ya silaha lakini bastola au sime ka we sio mmasai ni hatari sana. Huwezi kwenda kuwinda kwa kutumia bastola hata kama una uchu namna gani. Huwezi kutoka na sime kuchinjia kuku ukaacha kutumia kisu.
Hivyo basi, bastola ukiimiliki kuna siku mtu atakuudhi uito umtolee roho. Ukiingia ndani kuchukua sime, Utamla mbata tatu nne hivi lakini kuna siku utamuonja mwizi sikio au shingo. Ni hayo tu.
Ushauri;
Miliki gobore utakula nyama ya ngiri siku moja. Miliki panga utakatia majani ya mbuzi. Sio silaha zisizo na faida
 
Mhasibu wa zamani wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Ruvuma, Justin Rwendera amefariki akidaiwa kujiua kwa kujipiga risasi mdomoni akiwa nyumbani kwake.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Machi 30, 2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa amesema alijipiga risasi jana asubuhi kwa kutumia bastola yake,” alijipiga risasi mdomoni na kutokea sikio la kushoto. Bastola alikuwa anaimiliki kihalali.”

Amesema siku ya tukio, Amida Mahamoud ambaye ni mpishi wa Rwendera alifika nyumbani kwa mhasibu huyo wa zamani wa Takukuru na kukuta mwili wake ukiwa kwenye kochi huku damu zikiwa zimetapakaa.

“Ile bastola ilikuwa chini, aliwapigia simu ndugu wa marehemu na kutoa taarifa polisi,” amesema kamanda huyo.

Amesema siku moja kabla ya kujiua, Rwendera alirejea nyumbani saa 11 jioni akiwa amekunywa pombe na kumkuta mtoto wa kaka yake, Raulian Bathomeo ambaye alimuomba aingie ndani kula.

Amesema baada ya kula Rwendera alitoka na kwenda katika zizi la ng’ombe na Bathomeo aliondoka kwenda nyumbani kwake ambako alipokea taarifa za kifo.

Maigwa amesema polisi walikuta bastola, risasi saba na ganda moja la risasi, “bastola inashikiliwa kwa uchunguzi, hakuna aliyekamatwa kutokana na tukio hili.”

My take:

Bastola haina faida kwa walio wengi.
Ngoja Basi kwanza marehemu ni Alikua Mhasibu wa TANROAD au alikua mhasibu wa TAKUKURU?

Anywayz Mwenyezi Muumba ataamua pahala pa kumuhifadhi marehemu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amestaafu, anafanya ufugaji wa kisasa na anapokea pension hata kama watoto wake engineers wapo upande wa mama yao unapataje msongo wa mawazo ??? Wakati angeweza tu akavuta mtoto mbichi kabisa maisha yakasonga

Sent from my iPhone using JamiiForums

umewahi kuondokewa na mtu ambaye alikuwepo kwenye maisha yako kwa miaka mingi ? , hata utafute binti gani bado utamkumbuka tu, yahitaji watu wenye moyo mgumu kupitia hiko kipindi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah masikini mzee Rweyendela, huyu mzee alikuwaga mtu poa sana na kawapa maisha sana vijana wake pale TANROAD Ruvuma, personally namjua vizuri sana na alitusaidia sana kwenye msiba wa marehemu baba yetu mzazi miaka kama 10 hivi iliyopita sitasahau. Kuna kipindi hapa kati aliletewa zengwe sana kazini alishushwa cheo na kuhamishwa toka Ruvuma kwenda Morogoro baada ya kufanya kazi kidogo ilibidi aombe kustaafu kwa hiyari, akarudi Songea na kuendesha biashara zake. RIP boss, mbele yetu nyuma yako.
 
Alikua TANROADS na alikua anajihusishaNa biashara Na ufugaji wa kisasa wa ngombe Na kuku.Kifupi ni wale maisha bora wa miaka hiyo. Likizo mambele na wanae ni magenious na wote wawili ni mainjinia wapo TANROADS mikoa tofauti.Marehemu baada ya kustaafu aliendelea na biashara.(alikua na depression sana mambo ya ndoa)Personally namfahamu kwa sababu alikua jirani yetu kule Mtaa wa Angoni Arms miaka hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu anakaa pale karibu na angon arms kwenye Kona? Kwake Kuna makontena nje na nyasi kibao zilizokaushwa kwa ajili ya mifugo?
 
Dah masikini mzee Rweyendela, huyu mzee alikuwaga mtu poa sana na kawapa maisha sana vijana wake pale TANROAD Ruvuma, personally namjua vizuri sana na alitusaidia sana kwenye msiba wa marehemu baba yetu mzazi miaka kama 10 hivi iliyopita sitasahau. Kuna kipindi hapa kati aliletewa zengwe sana kazini alishushwa cheo na kuhamishwa toka Ruvuma kwenda Morogoro baada ya kufanya kazi kidogo ilibidi aombe kustaafu kwa hiyari, akarudi Songea na kuendesha biashara zake. RIP boss, mbele yetu nyuma yako.
Yeah Sure, Alikua mkorofi ukiharbu kazi ila nje ya hapo alikua mtu poa sana kwa kwel, Rest in Peace.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiran tutafutane tukanunue ile hoteli vile vimisonge vimejaa mchwa tupu
Alikua TANROADS na alikua anajihusishaNa biashara Na ufugaji wa kisasa wa ngombe Na kuku.Kifupi ni wale maisha bora wa miaka hiyo. Likizo mambele na wanae ni magenious na wote wawili ni mainjinia wapo TANROADS mikoa tofauti.Marehemu baada ya kustaafu aliendelea na biashara.(alikua na depression sana mambo ya ndoa)Personally namfahamu kwa sababu alikua jirani yetu kule Mtaa wa Angoni Arms miaka hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
irani
 
Back
Top Bottom