Aliyekuwa mgombea uras 2010 NCCR kunyang'anywa kadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyekuwa mgombea uras 2010 NCCR kunyang'anywa kadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Dec 15, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  List ni ndefu mbali ya Hashim Rungwe wengine wanaotajwa kuwamo ni mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali, Kamishna wa NCCR-Mageuzi Mkoa wa Tanga, Mbwana Hassan na wajumbe zaidi ya 20 wa NEC, hii ni kwa mjibu wa mtoa habari aliye karibu na katibu mkuu kuwa kazi hii inatarajiwa kukamilika jumamosi hii.
   
 2. tindo

  tindo JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 10,179
  Likes Received: 10,370
  Trophy Points: 280
  Wacha kivunjike tu maana ina viongozi waganga njaa na wabunge wake waliingizwa mkenge na CCM wakishirikiana na CUF kujifanya kuleta tafsiri ya kambi rasmi ya upinzani bungeni ili kuleta upinzani wa kinafiki na kuishia kuiwashia CCM kiyoyozi kwenye uwizi wa mali za nchi. Kwa mbaali wabunge wa NCCR wamejaribu kuomba msamaha indirect
   
 3. K

  KIROJO Senior Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mrema alikivunja hicho Chama sijuwi kimetokea wapi?
   
 4. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Kafulila aje aombe msamaha CDM ni mpiganaji mzuri.
   
 5. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hii kitu ya mgombea binafsi inabidi lazima iwepo kwenye katiba ijayo...nadhani hapo ndipo viongozi wa vyama watajua umuhimu wa kuendesha chama kama chama na si mali yao binafsi...!
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sintopenda kuanzisha mada mpya ila nawapa leo utabiri wangu..

  Mwaka 2012 kuna chama kipya kitaundwa na kuna uwezekano kikaitwa CCJ nawaona vijana wengi sana wasomi ambao kwa njjia moja ama nyingine wataondoka chama CCM, CUF, Chadema na hata kuua vyama vingine vidogo kuunda chama hiki. Chama hiki kitatokana na dhana ya kwamba wanaunda Upinzani wa kweli na hakika uchaguzi wa mwaka 2015 kitaleta ushindani mkubwa sana kwa Chadema lakini kama ilivyo kawaida watagawana kura na CCM ataendelea kutawala.
  2. Muafaka baina ya CUF na CCM utakomaa zaidi na upinzani utapungua kabisa kiasi kwamba siasa za chuki baina ya bara na Zanzibar zitakwisha, shukran kubwa kwa Shein na Seif kwa sababu Wazanzibar wengi walichokitaka ni kuona uuwiano wa madaraka, hizi siasa nyinginezo ilikuwa kutafuta kiti meza kubwa..


  Nawakilisha msije nimaliza kwa matusi lakini kaeni mkao wa sala....
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Eeeh bwana EASYFIT umebahatika bonge la avartar!!

   
 8. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  mbatia!!!, ni lini utaacha kuwa kibaraka wa ccm?
   
 9. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...kwani shek yahya kafufuka?,tulikuwa tumemshukuru Mungu ametuondolea huo ujinga,sasa huyu tena mtabiri wa mizim katoka wapi ktk karne hii ya utafiti wa kisayansi?!..."USHINDWE NA ULEGEE"
   
 10. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #10
  Dec 15, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280


  Viongozi wa vyama vya siasa walio wengi hawafanyi siasa,nadhani Jenerali ulimwengu anaweza kulielezea hili kwa ufasaha zaidi....

  Upinzani unapunguzwa nguvu na CCM kwa kusaidiwa na viongozi na wafuasi vipofu wa vyama vya upinzani.mtanzania wa kawaida anautamani ukombozi huku sisi tunacheza ngoma na wimbo ule ule wa miaka 50 ya kushindwa kwa CCM na serikali yake.Tuimarishe upinzani kwa dhati na kama mtu ana mawazo au fikra pevu zenye nia ya kuleta mabadiliko tumuunge mkono hata nje ya mipaka ya vyama vyetu.tukifanya hivyo tutatoa mwanya wa kuunda timu kubwa yenye fikra za maana katika mapinduzi halisi ndani ya Taifa hili.Tunaanza safari ya ukombozi wa pili wa Taifa letu,vyama vya siasa kwa kujitwalia madaraka ya kufanya maamuzi pekee vinawaburuza na kuwachelewesha watanzania.tutafakari,tuongeze nguvu ,tuipeleke Tanzania kule kunakostahili....

   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Halafu ajabu ni kwamba katika chama hiki namwona Rev. Kishoka na Mzee Mwanakijiji kama wasemaji na watetezi wakubwa..
   
 12. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Anafaa hata ccm
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Pale atakapoamua kuacha
   
 14. L

  LAT JF-Expert Member

  #14
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Joseph Selasini alikuwa nccr mageuzi tena karibu sana na Jemus Mbatia, sijui aligundua nini akatimua mbio akavaa magwanda fasta, sasa hivi ni mbunge, teh teh teh
   
 15. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #15
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Dawa si kukimbia, Mbona Kafulila ameingia na kupata Ubunge?NCCR imepata Wabunge ambao karibu wote ni wanachama hai wa CDM.Sasa suala hapa si kukimbia NCCR haikuanzishwa na Mbatia!!.NCCR inalipwa Ruzuku ambayo ni kodi yetu.Mbatia asifikiri Watu hawamuoni anapowatumikia ccm kwa siri! Saa ya kuaibika imefika bora utubu mbele za Mungu vinginevyo utang'oka
   
 16. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #16
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Dawa hapa sio kukimbilia CDM ,natoa rai kwa wanasheria na wana NCCR wote kuungana na kusema kweli Mbele za Mungu,.
   
 17. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Afadhali CDM nayo imepata tawi.
   
 18. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #18
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mbowe alisema Mbatia ni Kibaraka CCM,na aliwakataa Wabunge nccr kambi ya upinzani.Kumbe tatizo ni Mbatia !Mung'oe haraka!!
   
 19. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #19
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hata mimi naona NCCR inaweza kuwa nzuri bila Mbatia na kuweza kuungana na CDM bungeni, tumeona wameanza ku-practice.
   
 20. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #20
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  ccm hawataki vyama vya upinzani viwe na sura ya kweli ya Upinzani ndio maana wana wafuga watu kama Mbatia.Kwa mfano Kenya Vyama vya upinzani viliungana na kung'oa chama tawala,lakini hapa Tz vyama vya Nccr vinatafuta kuungana na kuimarisha chama tawala huku wakipinga upinzani ambao ni kazi yao.Angalia kwa sasa wananch wana hasira ndio maana kwenye vyama vyote vyenye mtazamo wa kuitumikia ccm vina mgogoro mkubwa(nccr na cuf).Dawa iliyopo ni kuwang'oa seif na Mbatia ili kuleta upinzani wa Kweli. Najua hofu ya CCM ni kuimarisha Nccr na endapo Mbatia atatoka Ni rahisi sana kuunda upinzani wenye kuungana kwa kauliko kuliko kufuga watu kama Mbatia ambaye ni Injinia wa Maji aliyeshindwa kutetea taluma yake
   
Loading...