Aliyekuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Mikumi 2015 kupitia (Ccm) JONAS ESTOMIAH NKYA amekamatwa kwa makosa ya Utakatishaji fedha na utapeli

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Ndugu NKYA ambaye ameshtakiwa kwa kesi mbalimbali za Utapeli nchini alikamatwa tangu tar 4 March baada ya shauri lake lingine la wizi wa kuaminika wa kiasi cha sh. Milioni 18 kusikilizwa siku hiyo kwenye Mahakama ya Kisutu, Ndugu Nkya anakabiliawa na shitaka la kumtapeli Dr. Hassan Mattaka mkazi wa Dar es salaam kiasi cha sh. Milioni 18 baada ya kukubaliana kuwa apewe kiasi hicho ili amuagizie Dr. Mattaka Gari aina ya KLUGER V Tangu mwaka 2011,

Inasemekana bwana Nkya aliagiza hiyo gari mpaka hapa nchini kupitia boda ya Horororo na akaliuza kwa mtu mwingine anayetambulika kwa jina la ndugu Isihaka Senga kwa kiasi cha sh. Milioni 20,

Bwana Nkya alitumia udanganyifu na kuliuza tena gari hiyo aina ya KLUGER V lenye namba za usajili T 965 CBW lililokuwa na majina ya Hassan Mattaka ambapo alipomkabidhi bwana Isihaka Senga gari hiyo ikiwa na majina hayo ya Mattaka kwa kudanganya kuwa yeye ndie anaitwa Hassan Mattaka tofauti na jina lake halisi la Jonas Estomiah Nkya, Baada ya kudai gari lake kwa muda mrefu bwana Mattaka aliamua kutoa taarifa Central police na Kesi ya Jonathan kufunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili apate haki yake lakini bwana NKYA alikuwa hafiki mahakamani kwa muda mrefu sana mara nyingi alikuwa akisingizia sababu mbalimbali ikiwemo Ugonjwa,

Mpaka siku hiyo alipokwenda Mahakamani kusikiliza kesi yake akiongozana na mawakili wake wawili na kubadilishiwa shitaka kutoka wizi wa kuaminika mpaka Utakatishaji wa Fedha (MONEY LAUNDERING) ambayo haina Dhamana na kupelekwa Moja kwa moja kwenye mahabusu ya gereza la SEGEREA,

Kesi ya Dr. Mattaka na Ndugu Nkya iliendelea kusikilizwa tena tar 18 Machi mwaka huu na akarudishwa tena Rumande SEGEREA, kesi Imeahirishwa mpaka tar 2 April itakaposikilizwa tena kwenye Mahakama hiyo ya Kisutu.
 
Tumesikiliza upande wako, upande wa Nkya hakana tuliyemsikiliza - uliwahi kufanya biashara?
 
Back
Top Bottom