Aliyekuwa mgombea ubunge kupitia CHADEMA, wanachama wengine zaidi ya 50 wahamia CCM

chilamanyika

JF-Expert Member
Nov 20, 2016
405
272
fe711da1df1a97034c65e92aadf8d442.jpg
b0d4452818477a44c1b032aa72654d5e.jpg

Hama hama ya vyama inazidi kushika kasi, Leo wakati tukiazimisha miaka 41 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi, chama hicho kimewapokea wanachama zaidi ya 50 kutoka CHADEMA akiwemo ndg James Mwanilyela aliekuwa mgombea wa ubunge jimbo la Kwela kupitia tiketi ya Chadema, hata hivyo Mbwana aliangushwa na mwenzake ndg Daniel Ngigo kwenye hatua ya kura za maoni.

Mwingine ni bwana Peter Kakondele pia alikua mgombea wa udiwani kata ya Laela kupitia Act wazalendo, katika hotuba yake wakati wa kupokea kadi ya CCM bwana James alisema "cdm kwa sasa wamekosa Sera na mipango kama chama kisichohitaji kushika dola, pia aliongeza na kusema CHADEMA ni kama kinyago kilicho chongwa na CCM kwa hiyo hakiwezi kuogopwa na wachongaji".

Kwa upande wake Kakondele alisema " kule act nilisukumizwa tu na nikabatizwa ubatizo usio wa kawaida, naomba kurudi kwa baba na nichinjiwe ndama kwani nimejuta kule nilikokuwa in utumwani".
 
DAAH HAO NAO WATAKUWA WAMENUNULIWA NINI?MAANA KWA AKILI YA KAWAIDA KUHAMA UPINZANI KWENDA CCM INASHANGAZA MNOO
 
Hivi senti hamsini ikirudishwa itaongeza ufaulu kwa wanafunzi wetu? hasa kule zanzibar ambao hawajawahi kutoa divisheni 1 achilia mbali kufaulisha.!?
kodi yangu inatumika vibaya!
 
utasikia kanunuliwa??? cdm mjitafakri upya haiwezekani eti kila anayehamia ccm kanunuliwa. tatizo lipo tena kubwa sana hasa mwenyekiti na fisadi lowasa
Hahaha...yaani nyie vijana wa lumumba mnatia huruma...hivi lowasa kahamia jana cdm.!?
 
yaan mtu alishindwa kwenye kura za maon anakuwaje mgombea ubunge?? yaan ukiwa na nia tu tayar umekua mhombea. mm mwenyewe nina nia ya kugombea urais je utaniita mgombea urais pasipo kupitishwa na chama changu?? lumumba punguzen mbwembwe kwenye maandishi
 
Nikaja mbioooooo nikidhani Salum kumbe James!! Habari nyingine jamani zitatuua kwa bp wallah!! Kwa nini mods msimpige bani ya miaka 4 huyu mtu? JF hatutaki majungu tunataka FACTS. Mtu kaangushwa kwa kura tu za maoni unampa cheo cha mgombea?? Ina maana cdm iliweka wagombea wawili??
 
yaan mtu alishindwa kwenye kura za maon anakuwaje mgombea ubunge?? yaan ukiwa na nia tu tayar umekua mhombea. mm mwenyewe nina nia ya kugombea urais je utaniita mgombea urais pasipo kupitishwa na chama changu?? lumumba punguzen mbwembwe kwenye maandishi
Bila kumpachika cheo feki na idadi ya watu feki ungesomaje hiyo article !!!?? CCM haiwezi kuzungumzia shs 300Billion zilizopotea ATCL au MAJENGO mabovu yanayofunguliwa huku yakiwa na ufa wanataka tuzungumzie vitu simple kama mtu aliyekataliwa na wananchi wala hakuwai kuwa mgombea alitaka kuwa mgombea wakamkataa.
 
MAZWAZWA akili zao ndipo zilipoishia hapo kuongea mambo ambayo hayana Tija yoyote ile kwa Watanzania.

Bila kumpachika cheo feki na idadi ya watu feki ungesomaje hiyo article !!!?? CCM haiwezi kuzungumzia shs 300Billion zilizopotea ATCL au MAJENGO mabovu yanayofunguliwa huku yakiwa na ufa wanataka tuzungumzie vitu simple kama mtu aliyekataliwa na wananchi wala hakuwai kuwa mgombea alitaka kuwa mgombea wakamkataa.
 
Haki ya katiba nivizuri tu uhuru wa kuchagua nawaza future ya kizazi chetu tu we tumbo wewe kwanini umekua mroho na mkaidi
 
Me nawaza kama hawa woote watakuwa wananunuliwa hivi mtu kama huyo hapo atakuwa amepewa kiasi gani na hao wenzie hamsini
 
Hata shaitwan alipoasi mbinguni alifukuzwa,lakini hii ya kuondoka na malaika wote ni ngumu kuielewa.
Weita!zungusha tena
 
Back
Top Bottom