YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,908
- 51,904
Dar es Salaam. Ndugu wa mbunge wa zamani wa Temeke, Abbas Mtemvu, wamekata rufaa wakipinga uteuzi wake kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu mama yao, Joyce Kilungo.
Abbas aliteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi hiyo na Mahakama ya Mwanzo, Temeke katika shauri la mirathi namba 474 la mwaka 2017.
Lakini ndugu zake wawili, Ibrahimu Mtemvu na Jasmine Mtemvu wamekata rufaa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki kuhusu Masuala ya Kifamili (ndoa, talaka na mirathi), Temeke.
Mbali na Ibrahim na Jasmine, warufani wengine ni watoto watano wa kaka zao wawili, George Mtemvu na Modibo Mtemvu pamoja na wa dada yao mmoja Amina Mtemvu waliofariki dunia.
Katika rufaa hiyo wanadai kuwa uteuzi wake si halali kwa kuwa hakuwahi kupendekezwa wala kuteuliwa na kikao cha familia kuwa msimamizi wa mirathi hiyo.
Wanadai kuwa alifungua shauri hilo kinyemela bila kuwashirikisha wala kufuata taratibu za kisheria na baada ya kuteuliwa amekuwa akiuza mali za mirathi kinyemela na kutumia pesa peke yake bila kuwashirikisha wala kuwajulisha.
Ndugu zake hao jana walilieleza Mwananchi kuwa Abbas ameshauza nyumba mbili za urithi, ikiwemo ya Masaki katika ploti namba 1036/2, Haile Selasie Road.
Ibrahim alilieleza Mwananchi nyumba hiyo Abbas alimuuzia Mustafa Mohamed, ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Delligent Group, kwa gharama ya Sh 900 milioni na pesa zote akatumia peke yake.
Hata hivyo akizungumzia madai hao, Abbas alisema kuwa hawezi kutoa maoni yoyote kuhusu hilo kwa kuwa shauri bado liko mahakamani.
Hata hivyo, alisema kuwa ndugu zake hao walishajaribu kufungua kesi Mahakama ya Temeke na Mahakama Kuu lakini wameshindwa.
“Mimi siwezi kuongeza zaidi, naiachia tu mahakama ndiyo itakayoamua,” alisema Abbas.
Source: Gazeti Mwananchi