Aliyekuwa Mbunge wa Sumbawanga Aeshi aruhusiwa na Mahakama kukata rufaa kwa mara ya pili.

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,195
ALIYEKUWA Mbunge wa Sumbawanga mjini, Aeshi Hillary aliyevuliwa wadhifa huo na Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, amepata tumaini jipya baada ya mahakama hiyo kumruhusiwa kukata rufani kwa mara nyingine.

Hillaly, aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), alivuliwa wadhifa huo na aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Bethuel Mmila April 30, 2012, kufuatia kesi iliyofunguliwa na Nobert Yamsebo.

Baada ya kuvuliwa wadhifa huo, Hillary alikata rufaa Mahakama ya Rufani akipinga hukumu ya Mahakama Kuu Sumbawanga kumvua wadhifa huo, lakini Oktoba 18, 2012, Mahakama ya Rufani ilitupilia mbali rufaa hiyo.
Hata hivyo, Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga imempa nafasi tena ya kukata rufaa, baada ya kuwasilisha maombi ya kuongezewa muda wa kuwasilisha kusudio la kukata rufaa upya, kupitia kwa Wakili wake, Richard Rweyongeza.

Wakili Rweyongeza alisema kuwa uamuzi huo ulitolewa na Jaji Lawrence Kaduri Alhamisi iliyopita, na kwamba wamepewa siku 14 kuwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa.

Wakili Rweyongeza aliongeza kuwa, kwa mujibu wa uamuzi huo, wanatakiwa kukata rufaa ndani ya siku 60 baada kufanya marekebisho ya dosari zilizobainika katika rufaa ya kwanza.

Rufaa ya awali ya Hilaly, ilitupiliwa mbali na mahakama hiyo katika uamuzi uliotolewa na Jopo la Majaji watatu, Januari Msofe, Edward Rutakangwa, na Engela Kileo, baada ya kubaini kasoro za kisheria.

Kasoro hiyo ni kutokuwepo kwa mwenendo wa maombi ya mlalamikaji katika kesi ya msingi, ya kuomba mahakama impangie kiwango cha pesa ambacho alipaswa kulipa kama amana ya kufungua kesi hiyo, kwa wa kifungu cha 111 (3) cha Sheria hiyo ya Uchaguzi ya mwaka 2010.

Kwa mujibu wa kifungu hicho, Mahakama ilisema kwamba mtu anayefungua kesi ya uchaguzi ni lazima awasilishe maombi ili mahakama impangie kiwango cha, amana anachopaswa kulipa ndani ya siku 14 tangu kufungua kesi.

Pia kifungu hicho kinaelekeza kwamba ndani ya siku 14 nyingine tangu siku ya maombi hayo, mahakama hiyo iwe imeshapanga kiwango hicho.

Mahakama hiyo ilisema kuwa ni muhimu wa mwenendo huo ni kuipa nafasi mahakama kuona kama maombi yaliwasilishwa ndani ya muda baada ya kesi kufunguliwa na pili ni kuona kama maombi hayo yaliamuliwa ndani ya muda tangu kuwasilishwa.

Mahakama hiyo ilisema kuwa, kwa mujibu wa Kanuni ya 96 (1) na (3) za Kanuni za Mahakama ya Rufani, si jukumu la upande katika kesi kuamua kuwa nyaraka fulani ni muhimu au si muhimu katika rufaa, kama wakili wa Hilaly, Rweyongeza alivyodai.

"Kutokuwepo kwa nyaraka hizo, rufaa haina nguvu chini ya Kanuni ya 96 (1) (k) ya Kanuni za Mahakama ya Rufani, hivyo rufaa inatupiliwa mbali.
 
Lwesye

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
5,292
0
Sikuwahi kujua kuwa mahakama wakati mwingine inaongozwa na watu waajabu sana wananunuliwa kwa harua mara Rwbakirila anatoa hukumu majini huko Arusha ,Mara mahakama sumbawanga inachelewesha haki ya mtu wapige dana dana tuu mpaka 2015 wawavue ubunge na wabunge wote wa chadema ambao wapinzani wao wamewawekea rufani ha ha ha kichekesho CCM inatangaza chadema bila kujijua
 
Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,700
2,000
Haki haipotei bali hucheleweshwa tu!watabana wataachia.Tusubiri!
 
dotto

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
1,725
1,500
Mkuu wa mihimili yote ni Kikwete; je hapo kuna kitu kipya?? Urais wa Kifalme.
 
Mwana va Mutwa

JF-Expert Member
Jun 9, 2009
460
225
ALIYEKUWA Mbunge wa Sumbawanga mjini, Aeshi Hillary aliyevuliwa wadhifa huo na Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, amepata tumaini jipya baada ya mahakama hiyo kumruhusiwa kukata rufani kwa mara nyingine.

Hillaly, aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), alivuliwa wadhifa huo na aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Bethuel Mmila April 30, 2012, kufuatia kesi iliyofunguliwa na Nobert Yamsebo.

Baada ya kuvuliwa wadhifa huo, Hillary alikata rufaa Mahakama ya Rufani akipinga hukumu ya Mahakama Kuu Sumbawanga kumvua wadhifa huo, lakini Oktoba 18, 2012, Mahakama ya Rufani ilitupilia mbali rufaa hiyo.

Hata hivyo, Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga imempa nafasi tena ya kukata rufaa, baada ya kuwasilisha maombi ya kuongezewa muda wa kuwasilisha kusudio la kukata rufaa upya, kupitia kwa Wakili wake, Richard Rweyongeza.
Wakili Rweyongeza alisema kuwa uamuzi huo ulitolewa na Jaji Lawrence Kaduri Alhamisi iliyopita, na kwamba wamepewa siku 14 kuwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa.

Wakili Rweyongeza aliongeza kuwa, kwa mujibu wa uamuzi huo, wanatakiwa kukata rufaa ndani ya siku 60 baada kufanya marekebisho ya dosari zilizobainika katika rufaa ya kwanza.

Rufaa ya awali ya Hilaly, ilitupiliwa mbali na mahakama hiyo katika uamuzi uliotolewa na Jopo la Majaji watatu, Januari Msofe, Edward Rutakangwa, na Engela Kileo, baada ya kubaini kasoro za kisheria.

Kasoro hiyo ni kutokuwepo kwa mwenendo wa maombi ya mlalamikaji katika kesi ya msingi, ya kuomba mahakama impangie kiwango cha pesa ambacho alipaswa kulipa kama amana ya kufungua kesi hiyo, kwa wa kifungu cha 111 (3) cha Sheria hiyo ya Uchaguzi ya mwaka 2010.

Kwa mujibu wa kifungu hicho, Mahakama ilisema kwamba mtu anayefungua kesi ya uchaguzi ni lazima awasilishe maombi ili mahakama impangie kiwango cha, amana anachopaswa kulipa ndani ya siku 14 tangu kufungua kesi.

Pia kifungu hicho kinaelekeza kwamba ndani ya siku 14 nyingine tangu siku ya maombi hayo, mahakama hiyo iwe imeshapanga kiwango hicho.

Mahakama hiyo ilisema kuwa ni muhimu wa mwenendo huo ni kuipa nafasi mahakama kuona kama maombi yaliwasilishwa ndani ya muda baada ya kesi kufunguliwa na pili ni kuona kama maombi hayo yaliamuliwa ndani ya muda tangu kuwasilishwa.

Mahakama hiyo ilisema kuwa, kwa mujibu wa Kanuni ya 96 (1) na (3) za Kanuni za Mahakama ya Rufani, si jukumu la upande katika kesi kuamua kuwa nyaraka fulani ni muhimu au si muhimu katika rufaa, kama wakili wa Hilaly, Rweyongeza alivyodai.

"Kutokuwepo kwa nyaraka hizo, rufaa haina nguvu chini ya Kanuni ya 96 (1) (k) ya Kanuni za Mahakama ya Rufani, hivyo rufaa inatupiliwa mbali."

HABARI YA GAZETI LA MWANANCHI
 
PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,261
2,000
Tunapoelekea mahakama zetu zinaelekea kuwa mahakama za kangaroo
 
andrewk

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
3,102
1,500
Kuna gazeti leo limezungumzia mahakama za TZ, sijaoma sijui walizungumza nini, lakini mengine ni kama haya madudu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom