Aliyekuwa Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga akamatwa na kikosi kazi kwa madeni

Hizi taarifa za Bavicha tabu tupu, mbona sisi tuna madeni ya mabenki na hatujakamatwa? Ukiwa na deni benki unakamatiwa dhamana zako na kupigwa mnada kufidia deni na siyo kulazwa ndani
Aliyekuwa Mbunge wa Monduli, JULIUS KALANGA anashikiliwa na kikosi kazi cha serikali kutoka Makao Makuu Dar, kinachohusika na kukusanya madeni.

Taarifa za uhakika zinasema Kalanga alikamatwa majira ya jioni nje ya ofisi za NMB na askari wa Takukuru na baadaye kupelekwa ofisi za Takukuru mkoa. Huku njiani akilalamika kwamba Mdhamini wake wa Mkopo huo Ndugu Kadogoo amemkimbia na hapokei simu zake tena.

"Juzi alikamatwa na kudhaminiwa na aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli, Isack Matasia aka Kadogo. Tumemsaka Kadogo hapatikani, lakini tumemtia nguvuni, leo tupo naye,"kilisema chanzo kimoja ofisi ya Takukuru

Kalanga anadaiwa kukopa matrekta kutoka NDC na amekimbia kulipa deni na kuzima simu.

Maofisa wa Habari waliopiga simu kupata taarifa, wametishiwa maisha na Ofisi ya MkuuwaMkoa Idd Kimantha.View attachment 1536105
 
Hizi taarifa za Bavicha tabu tupu, mbona sisi tuna madeni ya mabenki na hatujakamatwa? Ukiwa na deni benki unakamatiwa dhamana zako na kupigwa mnada kufidia deni na siyo kulazwa ndani

Punguza kuweweseka
Bavicha wametoka wapi kwenye hili jambo
Hata ukiingiliwa utasema bavicha tu
 
Aliyekuwa Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga anashikiliwa na kikosi kazi cha serikali kutoka Makao Makuu Dar, kinachohusika na kukusanya madeni.

Taarifa za uhakika zinasema Kalanga alikamatwa majira ya jioni nje ya ofisi za NMB na askari wa Takukuru na baadaye kupelekwa ofisi za Takukuru mkoa. Huku njiani akilalamika kwamba Mdhamini wake wa Mkopo huo Ndugu Kadogoo amemkimbia na hapokei simu zake tena.

Read More > Julius Kalanga, aliyekuwa Mbunge wa Monduli atiwa nguvuni - Imevuja!
Sasa kama alikudhamini ukapata huo mkopo na hutaki kuurejesha yeye sasa akusaidiaje zaidi ya kukukimbia kabla wewe hujamwacha solemba? Dawa yake ni wewe kulipa tu!!!
 
Katika makubaliano ya kuunga juhudi kilikuwwepo na kipengele Cha kumsamehee madeni yake, kulikoni tena akijatendewa haki
 
Back
Top Bottom