Elections 2010 Aliyekuwa Mbunge wa Lindi Mjini anusurika kipigo cha raia wenye......................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
TBC1 imeripoti sasa hivi ya kuwa aliyekuwa Mbunge wa Lindi Mjini Mheshimiwa Mohamed Abdul Aziz na ambaye bado ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa alinusurika kipigo cha raia wenye hasira kali baada ya kumhisi ndiye aliyekuwa akishinikiza Msimamizi wa uchaguzi asimtangaze mgombea ubunge wa CUF ambaye ni mlemavu wa ngozi asitangazwe mshindi wa ubunge jimbo hilo.......

Leo saa nane ndipo msimamizi wa Jimbo hilo alipomtangaza mlemavu huyo wa ngozi mshindi na raia wenye furaha walimbeba juu na maandamano yakaanza kuelekea mjini huku baadhi ya mabango yakimshutumu Mheshimiwa Abdul Aziz hakuna alilolifanya kwa miaka 15 ya ubunge wake.........

Polisi tu ndiyo walimwokoa Mheshimiwa huyo kipigo hicho kwa kumpatia ulinzi mkali
 
Back
Top Bottom