Uchaguzi 2020 Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Manyovu, Albert Obama akamatwa na TAKUKURU kwa kugawa Rushwa

Mbona watia nia wa ccm wanakamatwa sana kwa kutoa rushwa? Kuna kitu gani kinaendelea jamani?
Ipo hivi,wale wote ambao mkulu hawataki ndio wamekuwa walengwa,na hii imeshatolewa list kabisa. Hutasikia TAKUKURU ikikamata Dk. Mpango,Prof. J. Ndalichako,Prof. Kabudi, na wengineo wanakuwa "backed up" na mukulu.
 
Mkuu watu wanakamatwa na vidhibiti kabisa unasema ni njama kweli.?
Mkuu idawa ,huo ndio ukweli. CCM wote ni watoa rushwa,ila kama haupo upande wa mukulu,na yeye ana mtu anayemuhitaji unapambana naye,kifuatacho ni kutumia fimbo hiyo ya TAKUKURU.
 
Watoa rushwa hawawezipita.majina yao yapo.wanadhani CCM ya sasa ni ile ya zamani.
 
DG,
Ninapenda kukujulisha kwamba katika ufuatiliaji wa vitendo vya rushwa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020, leo TAKUKURU(M) Kigoma katika jimbo la uchaguzi la Buhigwe tumekamata Tsh. 210,000/= zilizokuwa zimeshagawiwa Tsh. 10,000/= kwa kila mjumbe kwa wajumbe 21 kutoka kata ya Mnanila jimboni humo katika kikao kilichokuwa kimeitishwa na Mbunge wa jimbo hilo aliyemaliza muda wake Mhe. ALBERT NTABALIBA OBAMA.

Aidha mbunge huyo amesalimisha kwa maafisa wa TAKUKURU kiasi cha Tsh. 2,000,000/= alizokutwa nazo wakati akiendelea na kikao hicho. Fedha Tsh. 210,000/= zilizokamatwa kutoka kwa wajumbe 21 zilikuwa zimegawiwa na Mwenyekiti wa UWT(W) Buhigwe ambaye katika maelezo yake amethibitisha kukabidhiwa fedha hizo na Mhe. Mbunge ALBERT NTABALIBA OBAMA.

Uchunguzi wa tukio hili unaendelea, tutawasilisha taarifa ya matokeo ya uchunguzi mapema iwezekanavyo.

Naomba kuwasilisha tafadhali.
Stay tuned.

=======

Tukio hilo lilitokea Tarehe 07/07/2020 saa nane Mchana. Mbunge aliyemaliza muda wake Obama, alikuwa na kikao halali cha CCM.

Pamoja na kwamba hajatangaza nia ya kugombea Popote, TAKUKURU waliweza kujipenyeza kwenye kikao chake na Walimkuta anagawa elfu 10 kwa kila Mjumbe aliyehudhuria. (alikuwa hagawi yeye, alimpa mtu awagawie Wajumbe hapo Mkutanoni).

Walipomkagua wakakuta ana laki mbili na elfu kumi. Alikua kashagawa elfu kumi kumi kwa Wajumbe 21.

Obama alijitetea kwamba aliwachelewesha wajumbe kuondoka hivyo ilikua ni hela ya chakula cha Mchana kwa Wajumbe waliokuwa wapo mkutanoni tangu saa tatu asubuhi.

TAKUKURU wakawataka waliopokea hela warudishe na wakashikilia laki mbili na Elfu kumi zilizokuwa zinagawiwa kwa Uchunguzi.

Pia wakamtaka Obama kama ana hela yoyote aisalimishe, akasalimisha Milioni Mbili.

Baada ya hapo wakamruhusu aendelee na Vikao vyake kwenye vijiji mbalimbali kama ratiba yake inavyoonesha. Akimaliza atahojiwa..

Hata hivyo Kesho Tarehe kumi saa tatu asubuhi, TAKUKURU Kigoma, itatolea ufafanuzi wa kina swala hili.

Majuto ni mjukuu mkono shavuni,na mpunga wenyewe hadharani
 
Majuto ni mjukuu mkono shavuni,na mpunga wenyewe hadharani
Kwanini wanaokamatwa na rushwa ni ccm tu, shangaa et TAKUKURU wanaikomalia chadema kwa matumizi mabaya. Na ukitaka kujua kuwa wako juu ya sheria yataisha kimya kimya, hivi bado mnamkumbuka aliyekamatwa na rundo la bunduki ?. Shangaa wakiambiwa wanafanya biashara ya kununua madiwani na wabunge wanakuja juu. Hawa jamaa hawana uwezo wa kushawishi zaudi ya kununua na porice
 
DG,
Ninapenda kukujulisha kwamba katika ufuatiliaji wa vitendo vya rushwa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020, leo TAKUKURU(M) Kigoma katika jimbo la uchaguzi la Buhigwe tumekamata Tsh. 210,000/= zilizokuwa zimeshagawiwa Tsh. 10,000/= kwa kila mjumbe kwa wajumbe 21 kutoka kata ya Mnanila jimboni humo katika kikao kilichokuwa kimeitishwa na Mbunge wa jimbo hilo aliyemaliza muda wake Mhe. ALBERT NTABALIBA OBAMA.

Aidha mbunge huyo amesalimisha kwa maafisa wa TAKUKURU kiasi cha Tsh. 2,000,000/= alizokutwa nazo wakati akiendelea na kikao hicho. Fedha Tsh. 210,000/= zilizokamatwa kutoka kwa wajumbe 21 zilikuwa zimegawiwa na Mwenyekiti wa UWT(W) Buhigwe ambaye katika maelezo yake amethibitisha kukabidhiwa fedha hizo na Mhe. Mbunge ALBERT NTABALIBA OBAMA.

Uchunguzi wa tukio hili unaendelea, tutawasilisha taarifa ya matokeo ya uchunguzi mapema iwezekanavyo.

Naomba kuwasilisha tafadhali.
Stay tuned.

=======

Tukio hilo lilitokea Tarehe 07/07/2020 saa nane Mchana. Mbunge aliyemaliza muda wake Obama, alikuwa na kikao halali cha CCM.

Pamoja na kwamba hajatangaza nia ya kugombea Popote, TAKUKURU waliweza kujipenyeza kwenye kikao chake na Walimkuta anagawa elfu 10 kwa kila Mjumbe aliyehudhuria. (alikuwa hagawi yeye, alimpa mtu awagawie Wajumbe hapo Mkutanoni).

Walipomkagua wakakuta ana laki mbili na elfu kumi. Alikua kashagawa elfu kumi kumi kwa Wajumbe 21.

Obama alijitetea kwamba aliwachelewesha wajumbe kuondoka hivyo ilikua ni hela ya chakula cha Mchana kwa Wajumbe waliokuwa wapo mkutanoni tangu saa tatu asubuhi.

TAKUKURU wakawataka waliopokea hela warudishe na wakashikilia laki mbili na Elfu kumi zilizokuwa zinagawiwa kwa Uchunguzi.

Pia wakamtaka Obama kama ana hela yoyote aisalimishe, akasalimisha Milioni Mbili.

Baada ya hapo wakamruhusu aendelee na Vikao vyake kwenye vijiji mbalimbali kama ratiba yake inavyoonesha. Akimaliza atahojiwa..

Hata hivyo Kesho Tarehe kumi saa tatu asubuhi, TAKUKURU Kigoma, itatolea ufafanuzi wa kina swala hili.

Hili Bunge limejaa wabunge maskini sana na ccm imejaa watu wenye njaa zisizoelezeka.

Hivi kweli inaingia akilini mbunge unatoa rushwa ya shilling 10000/= kweli !!!!

Wajumbe wa ccm nao wanauza maisha ya wananchi miaka mitano kwa shillingi 10000/= !!!!!!.

😀😀😀😀😀😀
 
Kwa nini utoe rushwa kama.unaamini umeitendea haki.nafasi yako?
Halafu linatoa 10,000 halionekani tena hadi 2020.ajiandae tu kulima chikichi
 
Screenshot_20200710-132227_Chrome.jpg

Yuko chini ya ulinzi
 
TAKUKURU (M) Kigoma imemkamata aliyekua Mbunge wa Bihigwe (CCM) Albert Ntabaliba maararufu kama Obama, kwa tuhuma za kugawa rushwa kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo kata ya Mnanila. TAKUKURU pia imekamata wajumbe 21 ambao kila mmoja alikua amegawiwa rushwa ya TZS 10,000/= na Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Buhigwe kwa maelekezo ya Obama.

Aidha mbunge huyo amesalimisha kwa maafisa wa TAKUKURU kiasi cha TZS 2,000,000/= alizokutwa nazo wakati akiendelea na kikao hicho ambazo zinadaiwa kulenga kuwahonga viongozi wilaya wa chama hicho. Katika jimbo hilo Obama anachuana na makada wenzie 17 akiwemo Waziri wa fedha Dr.Philip Mpango, ambapo mmoja wao atapewa nafasi ya kugombea ubunge kupitia chama hicho.!
FB_IMG_1594376652697.jpg
 
Hio ni nafasi ya bwana Mpango, na huyu Dr. Atafute kazi nyingine. Wana CCM sijui kwa nini wanaamini katika rushwa kuliko kitu chochote!
 
Back
Top Bottom