Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
IDD Azzan aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni (CCM), amekubali kushindwa na Maulid Mtulia wa CUF,anaandika Faki Sosi.
Azzan kupitia wakili wake Abubakari Salim ameiomba Mahakama Kuu nchini kufuta kesi yake ya kupinga matoke ya ubunge uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana katika jimbo hilo dhidi ya Mtulia.
Wakili Salim, wakili wa upande wa mlalamikaji mbele Noel Chocha, Jaji kutoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya akisikili kesi hiyo amesema, wameamua kufuta kesi hiyo kwa maslahi mapana ya wapiga kura wa Kinondoni.
Amesema, “wakati shauri hilo linaendelea tulijadiliana pande zote mbili kati yetu walalamikaji na walalamikiwa hivyo tunapenda kulitoa shauri hilo mahakamani hapa.”
Nassoro Juma, wakili wa upande wa utetezi amesema kuwa, upande wa utetezi hauna pingamizi la kuondoa shauri hilo zaidi ya kuomba kurejeshewa gharama za uendeshaji kesi walizozitumia.
Amesema kuwa, kuliondoa shauri hilo mahakamani kumezingatia haki ya wapiga kura ya mwananchi wa Kinondoni.
“Uwepo wa shauri hilo yangu Novemba 2015 hadi Mei 2016 imemtia gharama kubwa Maulid Mtulia Mbunge wa Kinondoni kwa kutulipa sisi mawakili na mashahidi,”amesema Juma.
Hashim Ngole, Wakili Mkuu wa Serikali amekiri kupokea ‘notis’ kutoka kwa wakili wa mdai ambapo amesema “sisi hatuna pinganizi katika ombi hilo.”
Amemuomba hakimu aiagize mahakama kuamua juu ya gharama akitoa mfano kwamba, yeye amesafiri kutoka Bukoba, Kagera kwa ajili ya kuendesha kesi hiyo na kuwa, serikali imeingia gharama “shauri hili liondolewe kwa jinsi unavyoona gharama inayofaa.”
Noel Chochi, Jaji katika Mahakama Kuu amesema kuwa, ombi la kufutwa kwa kesi hiyo limekubalika katika mahakama hiyo na kuwa, gharama za kesi hiyo zitalipwa ila hazitawekwa waazi kuwa ni kiasi gani.
Chanzo: MwanaHalisi