Aliyekuwa mbunge Sumbawanga mjini kukata rufaa

Sitaki kuwaudhi lakini ni ukweli usiopingika kwamb Chadema itashindwa uchaguzi 2015 na baada .ya hapo itasambaratika kutoka simba kuwa fisi. Historia itajirudia Kama ilivyotokea kwa NCCR-M mwaka 1995. Miaka ishirini ni kipindi cha kutosha kwa historia kujirudia.
 
yeye aendelee tu na rufaa yake,cha mhimu sisi tumefanikiwa kupunguza watu wa ndiyoooooooooooooooooooooo,mjengoni
 
Sitaki kuwaudhi lakini ni ukweli usiopingika kwamb Chadema itashindwa uchaguzi 2015 na baada .ya hapo itasambaratika kutoka simba kuwa fisi. Historia itajirudia Kama ilivyotokea kwa NCCR-M mwaka 1995. Miaka ishirini ni kipindi cha kutosha kwa historia kujirudia.

nenda maliwatoni katoe haja kubwa na utawadhe na gazeti la uhuru
 
Aliyekuwa mbunge wa Sumbawanga mjini Bwana Aeshy Hilaly ametangaza nia yake ya kukata rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa leo katika mahakama ya rufaa kanda ya sumbawanga na hakimu kuamuru uchaguzi urudiwe.
Kamanda Doma
Mytake
kwa hali ya sasa CCM hawana chao sumbawanga mjini

Hata aliye enguliwa mwenyewe analijua hilo. Vp ktk hiyo hukumu anaruhusiwa kugombea tena?
 
Watakata rufaa mpaka 2015 itawakuta bado wanapiga kesi wakati ukombozi wa nchi nzima utakuwa umewadia.
 
Sitaki kuwaudhi lakini ni ukweli usiopingika kwamb Chadema itashindwa uchaguzi 2015 na baada .ya hapo itasambaratika kutoka simba kuwa fisi. Historia itajirudia Kama ilivyotokea kwa NCCR-M mwaka 1995. Miaka ishirini ni kipindi cha kutosha kwa historia kujirudia.

Kama kawaida yenu WATUMWA kazi yenu tunaiona unaachia ushuzi halafu unajikausha Kama vile sio wewe,angalizo chunga nzi watakuumbua.Upo nchi gani vile?
 
Aliyekuwa mbunge wa Sumbawanga mjini Bwana Aeshy Hilaly ametangaza nia yake ya kukata rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa leo katika mahakama ya rufaa kanda ya sumbawanga na hakimu kuamuru uchaguzi urudiwe.
Kamanda Doma
Mytake
kwa hali ya sasa CCM hawana chao sumbawanga mjini

Arudishe posho zote, shangingi, rushwa zote ambazo amewahi kupokea na pia awaache mahara wote ambao amejilimbikizia
 
Aliiba kura.Alitoa rushwa.Ushahidi umewekwa wazi..
Amevuliwa ubunge..angekuwa ni mwenye hekima angekaa kimya tu..
Kwanini TAKUKURU hawajamkamta bado?
 
Mbunge wa CCM ang`oka


headline_bullet.jpg
Ni Aeshy Hillary wa Jimbo la Sumbawanga Mjini
headline_bullet.jpg
Hatiani kwa rushwa, kuzuiwa miaka mitano



Aeshy.jpg

Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshy Khalfan Hillary


Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga imetengua matokeo ya wa ubunge yaliyompa ushindi Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshy Khalfan Hillary, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Uamuzi wa kutengua matokeo hayo ulitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Bethwell Mmilla, ambaye alisikiliza kesi hiyo.

Kesi hiyo namba 01 ya mwaka 2010 ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Norbert Yamsebo.

Katika uchaguzi huo uliofanyika mwaka juzi, ulikuwa na ushindani mkubwa, Aeshi alipata kura 17,328 wakati Yamsebo alipata kura 17,132.

Katika hukumu hiyo yenye kurasa 68 iliyosomwa na Jaji Mmilla kwa saa tatu, alisema kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mlalamikaji hivyo kutengua matokeo hayo kutokana na hoja mbili.
Jaji Mmilla alisema alitengua matokeo hayo kutokana na madai ya kuwepo kwa vitendo vya rushwa na vurugu zilizokuwa zikifanywa na wafuasi wa CCM wakati wa kampeni. Mlalamikaji alikuwa amewasilisha hoja 21.

Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi iwapo mtu atapatikana na hatia ya rushwa katika uchaguzi hataruhusiwa kugombea nafasi ya kisiasa kwa muda wa miaka mitano. Adhabu kama hii ilipata kumpata Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wassira, wakati huo akiwa mbunge wa NCCR wa jimbo la Bunda. Sasa ni mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM.

HOJA ZA KESI
Baadhi ya hoja hizo ni ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi; matokeo ya uchaguzi kupishana katika vituo vitatu vya Kizwite pamoja na vituo viwili vya Kandandala; kupinga Justus Athanas ambaye ni mtendaji wa kata kuwa msimamizi wa uchaguzi katika kituo cha Katandala wakati akiwa ni kada wa CCM; tukio la kucheleweshwa kwa masanduku ya kupigia kura katika kata ya Katandala na msimamizi katika kituo cha Matanga kufungua masanduku ya kura.

Hoja nyingine ni tukio la makada wa CCM kwa kushirikiana na mbunge huyo kushiriki katika ununuzi wa shahada za kupigia kura; kubadilisha wapiga kura katika vituo vya Pito na Mbalika; vurugu zilizosababisha kutofanyika kwa kampeni za Chadema katika vijiji vya Mtimbwa na Kisumba kwa siku tofauti na vitendo vya rushwa kama kugawa vifaa vya michezo pamoja na pombe katika kijiji cha Pito.
Mgombea wa Chadema pia alilalamikia kutolewa kwa rushwa ya mifuko 20 ya saruji na vinywaji katika kijiji cha Katumba; kugawa fedha na vinywaji kwa wapiga kura katika kituo cha mazoezi kilichopo Kandalamba mjini Sumbawanga na kutoa msaada wa fedha kwa Kanisa Katoliki pamoja na msimamizi wa uchaguzi kubadilisha baadhi ya vituo vya kupigia kura kupelekwa mbali zaidi kati ya kilomita tano hadi nane, hivyo kuchangia kuathiri matokeo ya uchaguzi huo.

FURAHA YATAWALA MAHAKAMANI
Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo ya kutenguliwa kwa matokeo iliyosomwa kwa lugha ya Kingereza na kulitangaza Jimbo la Sumbawanga Mjini kuwa wazi, wafuasi wa Chadema walilipuka kwa furaha na kuipongeza Mahakama hiyo kwamba imetoa maamuzi ya haki.
Aidha, nje ya Mahakama hiyo zilibuka kelele za shanwge, nderemo na vifijo kutoka kwa wafuasi wa Chadema, hali iliyomlazimu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) Mkoa wa Rukwa, Laurent Magweshi, kuwatuliza vijana hao ili watoke eneo la Mahakama na kuepuka usumbufu kwa kuwa kesi nyingine zilikuwa zinaendelea.
AESHY: NAWASILIANA NA MAWAKILI
Baada ya hukumu hiyo, aliyekuwa Mbunge Aeshy Khalifan Hillary alisema: "Nimeisikia hukumu na nitawasiliana na mawakili wangu ili kujua ni kipi watakishauri katika kesi hii na kisha nitawajulisha."
Wakili wa Aeshy, Juma Nassoro, alisema anasubiri maamuzi ya mteja wake.
Aliongeza kuwa hukumu hiyo inakinzana na hoja zilizotolewa mahakamani hapo na kuwa atazungumza na mteja wake ili wakate rufani.
MGOMBEA WA CHADEMA: NAISHUKURU MAHAKAMA
Aliyekuwa mgombea wa Chadema, Norbeth Yamsebo, alisema kuwa ameipokea hukumu hiyo kwa mikono miwili na kuishukuru Mahakama hiyo kwa haki iliyotolewa na kusema kuwa bado anafanya mawasiliano na chama chake ili kujua ni nini kitaendelea.
CHADEMA: TUNALISUBIRI JIMBO
Mkurugenzi wa habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, alijigamba kwamba Chadema kinajiandaa kuchukua jimbo hilo.
Alisema jimbo hilo lilikuwa ni haki yao, lakini ikapindishwa na kwamba baada ya hukumu hiyo ya Mahakama, chama kinajiandaa kuingia katika uchaguzi ili kulinyakua.
WAFUASI WA CCM WANYONG'ONYEA
Wafuasi wa CCM pamoja na viongozi wa chama hicho mara baada ya hukumu hiyo walionekana kupigwa na butwaa huku wengine wakibubujikwa na machozi.
NAPE: NI MAPEMA KUSEMA LOLOTE
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Nape Nnauye, alipoulizwa maoni yake baada ya kuhumu hiyo, alisema ilikuwa ni mapema kuzungumza lolote.
Walalamikiwa wengine katika kesi hiyo walikuwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na msimamizi wa uchaguzi wanaodaiwa kukiuka sheria na kanuni za uchaguzi.
Katika kesi hiyo, mlalamikaji aliwakilishwa na kampuni ya uwakili ya Mkumbe & Company ya Mbeya huku upande wa Serikali uliwakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Paul Shahidi.
Aeshy aliwakilishwa na jopo la mawakili watatu wakiongozwa na Ileth Mawalla kutoka S. Mawalla Law Consultant and Attorney.
Kesi zote za kupinga uchaguzi zinatarajiwa kumalizika Mei 4, mwaka huu baada ya kuongezwa muda na Waziri wa Katiba na Sheria, Selina Kombani, kutokana na kutokamilika ndani ya mwaka mmoja tangu uchaguzi kumalizika.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Mohamed Chande, hivi karibuni alisema kesi zote za uchaguzi zitamalizika Mei 4, mwaka huu.

Hiyo ni hukumu ya pili ya kutengua matokeo ya ubunge. Aprili 5, mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilitengua matokeo ya ubunge Jimbo la Arusha Mjini, baada ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila, kumvua ubunge Godbless Lema (Chadema), baada ya kuridhika kuwa alikiuka maadili ya uchaguzi.


CHANZO: NIPASHE




 
Rufaa haki yake lakini kwa menendo wa ushahidi ulivyokuwa hata kama majaji wa rufaa wangekuwa ze comedi bado hatoki
 
Ni haki yake. Wacha aendelee kuteketeza visenti vyake. Vingine vitaendelea kuliwa na mchwa.
 
CCM they very strategically akikata rufaa kesi itabigwa danadana mpaka next year(2013) Then hukumu ikitoa atakuwa ameshindwa ila kutakuwa hakuna uchaguzi coz itakuwa imebaki miaka miwili mpk uchaguzi mwingine kwahiyo jimbo litabaki wazi. Huu ndiyo mchezo ambao wamegundua ila isaidi zaidi ya kupoteza muda.

Mytake:Kama kuna kitu ambacho CCM wanakiogopa kwa sasa basi ni by election hata iwe ya diwani coz wao ndiyo looser hata kama wanashinda kiti lakini CDM wanakuwa wameimarika hata kule ambako walikuwa dhaifu which give them Strengh.

By-election ni jambo la kikatiba, haliwezi kuamuliwa na chama kimoja cha siasa kwa hofu! Hata kama itabaki wiki kabla ya uchaguzi, wananchi wa S'wanga wana haki ya kuwakilishwa! itisheni mbwagwe, mjipange! Falsafa ya kujivua magamba itawamaliza! SIJAWAHI KUONA KOBE AKABAKI HAI NJE YA GAMBA LAKE!
 
Back
Top Bottom