Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,455
- 29,133
Inna Lilah, Wa Inna Ilaihir Rajiuun,
Aliyekua Katibu Mkuu wa Yanga Bwana Abdul Sauko amefariki leo Alfajir katika Hospital ya Mloganzila.
Taarifa zaidi zitafuata
=====
Abdul Sauko (kushoto) akiwa na Seif Magari (kulia).
Klabu ya Yanga imepata msiba wa kiongozi wake wa zamani Abdul Sauko ambaye amefariki dunia leo Aprili 10, 2022 alipokuwa amelazwa katika Hospitali ya Mloganzila.
Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema: “Msiba umetokelea leo asubuhi (Aprili 10, 2022), tutaendelea kutoa taarifa zaidi kadiri familia itakavyokuwa inatujulisha, lakini kuna uwezekano wa maziko kufanyia leo hii kama ratiba hazitabadilika.
“Abdul Sauko enzi za uhai wake aliwahi kuwa Kaimu Katibu Mkuu, Katibu Mipango, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ndani ya Yanga.
“Ni mmoja wa viongozi wenye heshima kubwa ndani ya Yanga, pia katika mchezo wetu wa leo (dhidi ya Geita Gold) tutasimama dakika moja kumuenzi na wachezaji wote watavaa vitambaa vyeusi.”
Chanzo: Azam TV