Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha CCK mbaroni kwa kujifanya ‘usalama’

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
1643350706396.png

Picha: Renatus Muabhi

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (53) na mwenzake wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Kwa kosa la kujifanya maofisa usalama huku wakijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Mbali na Muabhi mwingine ni mfanyabiashara Yusuph Yusuph (33) ambao kwa pamoja walitenda makosa hayo Katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam

Akisoma hati ya mashtaka katika mahakama hiyo leo Januari 27, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mwanaamina Kombakono mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rhoda Ngimilanga, alidai katika shitaka la kwanza lililofanyika Desemba 24, 2021 katika ofisi ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mshtakiwa Muabhi kwa nia ovu alijitambulisha kama ofisa usalama wakati akijua si kweli.

Katika shitaka la pili inadaiwa kwamba Julai 10, 2021 katika ofisi hizo za BoT washitakiwa wote Kwa pamoja walijitambulisha kwa Clay Apio kuwa wao ni maofisa usalama wakati wakijua si kweli.

Hata hivyo, washitakiwa hao wamekana kutenda makosa hayo, lakini upande wa mashitaka umesema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Baada ya maelezo hayo Hakimu, Ngimilanga alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wakiwa na barua zinazotambulika na wasaini bondi ya Sh5 milioni.

Mshitakiwa Yusuph aliachiwa kwa dhamana lakini Muabhi amepeleka mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana hiyo na kesi imeahirishwa hadi February 10, 2022 kwa ajili ya kutajwa.

PIA, SOMA:

- Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK) mbaroni kwa kuomba rushwa ya Tsh. Milioni 50 (12/12/2019)
 
😃😃😃 Unanijuwa Mimi ni nani? Watu wanachoma vichwa usiku na mchana kupaisha uchumi huko Kenya huo ndo UTISii
 
View attachment 2098144

CCK ilianzishwa na CCM ili kuuvuruga upinzani lakini wakashindwa.
 
Back
Top Bottom