nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
LEMA alikua ananitaka kimapenzi nikakataaa
Babu na uzee wake nae alitaka niwe mke wake nikakaata wakanifanyia zengwe mpaka nikafukuzwa uanachama japo nilikuwa diwani.
Nawashauri akina mama msijiunge na chadema viongozi wa huku wanatabia chafu wanajifanya wazalendo kumbe ni wazarendo wa chupi kama degree za chupi
DIWANI WA CHADEMA ALIEHAMIA CCM LEO AKIILANI VIKALI CHADEMA KWA MAELFU YA WANAINCHII WALIOJITOKEZA KUSHUHUDIA ANGUKO LA CHADEMA aliyekuwa diwani wa cdm, kata ya olasite.akiongea kwa uchungu baada ya kutendwa
Rehema Mohamed Diwani wa Zamani wa CHADEMA akitokwa na MACHOZI ya UCHUNGU MKALI Sana...
Kutoka CHADEMA:
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).
TAARIFA KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI KUU YA CHADEMA YALIYOFIKIWA KATIKA MKUTANO WA DHARURA ULIOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI/JUMAPILI TAREHE 06-07 AGOSTI 2011 KATIKA HOTELI YA IMAGI MJINI DODOMA.
TAARIFA KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI KUU YA CHADEMA YALIYOFIKIWA KATIKA MKUTANO WA DHARURA ULIOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI/JUMAPILI TAREHE 06-07 AGOSTI 2011 KATIKA HOTELI YA IMAGI MJINI DODOMA.
Kamati Kuu ya CHADEMA ilikutana katika Mkutano wa Dharura uliofanyika siku ya Jumamosi na Jumapili tarehe 06 Agosti 2011 katika Hoteli ya Imagi Mjini Dodoma. Pamoja na mambo mengine Ilifikia maamuzi yafuatayo :
1. Kamati Kuu ilipokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo iliyoyatoa katika Mkutano wake wa tarehe 17 Julai 2011 iliyowataka madiwani wa CHADEMA Arusha kujiuzulu nafasi walizozipata pamoja na kuomba radhi kwa makosa waliyoyafanya kutokana na mwafaka uliofikiwa baina yao na madiwani wenzao wa TLP na CCM kwa kuwa chama hakikuridhia wala kuutambua mwafaka huo.
2. Kamati Kuu imezingatia kuwa, kati ya madiwani 10 waliopewa maelekezo na Kamati Kuu, madiwani watano (5) ndio wametekeleza maelekezo kikamilifu wakati madiwani wengine watano (5) wamekataa kuyatekeleza maelekezo hayo.
3. Baada ya kutafakari kwa kina taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati Kuu, na kuwapa nafasi ya kujieleza mbele ya Kamati Kuu Madiwani ambao walikuwa hawajatekeleza maelekezo,Kamati Kuu imezingatia kuwa madiwani wamekataa kutekeleza maagizo ya Kamati Kuu.
Aidha, Kamati Kuu imezingatia kuwa kitendo cha madiwani kukataa kutekeleza maagizo halali ya Kamati Kuu ni utovu mkubwa wa nidhamu na ni kuvunja maadili na kanuni za chama, na kinaenda kinyume na msingi mama wa CHADEMA wa uwajibikaji.
Hivyo basi, kwa kutumia mamlaka ya Kikatiba Kamati Kuu imewafukuza uanachama madiwani watano wafuatao kwa kosa la kukataa kutekeleza maagizo ya Kamati Kuu:
i) Ndugu Estomih Mallah
ii) Ndugu John Bayo
iii) Ndugu Charles Mpanda
iv) Ndugu Rehema Mohamed
v) Ndugu Reuben Ngowi
Watajwa hapo juu wamejulishwa maamuzi ya Kamati Kuu ndani ya Mkutano tarehe 07 Agosti 2011 saa 7:57 usiku, Aidha, kila mmoja wao atakabidhiwa barua yenye kueleza maamuzi ya Kamati Kuu.[/QUOTE]