Aliyekuwa DIWANI wa CHADEMA ahamia CCM... asema LEMA alikuwa anamtaka KIMAPENZI

Status
Not open for further replies.

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,869
1,225

LEMA alikua ananitaka kimapenzi nikakataaa

Babu na uzee wake nae alitaka niwe mke wake nikakaata wakanifanyia zengwe mpaka nikafukuzwa uanachama japo nilikuwa diwani.

Nawashauri akina mama msijiunge na chadema viongozi wa huku wanatabia chafu wanajifanya wazalendo kumbe ni wazarendo wa chupi kama degree za chupi

DIWANI WA CHADEMA ALIEHAMIA CCM LEO AKIILANI VIKALI CHADEMA KWA MAELFU YA WANAINCHII
WALIOJITOKEZA KUSHUHUDIA ANGUKO LA CHADEMA aliyekuwa diwani wa cdm, kata ya olasite.akiongea kwa uchungu baada ya kutendwa
Rehema Mohamed Diwani wa Zamani wa CHADEMA akitokwa na MACHOZI ya UCHUNGU MKALI Sana...

Kutoka CHADEMA:

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).

TAARIFA KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI KUU YA CHADEMA YALIYOFIKIWA KATIKA MKUTANO WA DHARURA ULIOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI/JUMAPILI TAREHE 06-07 AGOSTI 2011 KATIKA HOTELI YA IMAGI MJINI DODOMA.

Kamati Kuu ya CHADEMA ilikutana katika Mkutano wa Dharura uliofanyika siku ya Jumamosi na Jumapili tarehe 06 Agosti 2011 katika Hoteli ya Imagi Mjini Dodoma. Pamoja na mambo mengine Ilifikia maamuzi yafuatayo :

1. Kamati Kuu ilipokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo iliyoyatoa katika Mkutano wake wa tarehe 17 Julai 2011 iliyowataka madiwani wa CHADEMA Arusha kujiuzulu nafasi walizozipata pamoja na kuomba radhi kwa makosa waliyoyafanya kutokana na mwafaka uliofikiwa baina yao na madiwani wenzao wa TLP na CCM kwa kuwa chama hakikuridhia wala kuutambua mwafaka huo.

2. Kamati Kuu imezingatia kuwa, kati ya madiwani 10 waliopewa maelekezo na Kamati Kuu, madiwani watano (5) ndio wametekeleza maelekezo kikamilifu wakati madiwani wengine watano (5) wamekataa kuyatekeleza maelekezo hayo.

3. Baada ya kutafakari kwa kina taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati Kuu, na kuwapa nafasi ya kujieleza mbele ya Kamati Kuu Madiwani ambao walikuwa hawajatekeleza maelekezo,Kamati Kuu imezingatia kuwa madiwani wamekataa kutekeleza maagizo ya Kamati Kuu.

Aidha, Kamati Kuu imezingatia kuwa kitendo cha madiwani kukataa kutekeleza maagizo halali ya Kamati Kuu ni utovu mkubwa wa nidhamu na ni kuvunja maadili na kanuni za chama, na kinaenda kinyume na msingi mama wa CHADEMA wa uwajibikaji.

Hivyo basi, kwa kutumia mamlaka ya Kikatiba Kamati Kuu imewafukuza uanachama madiwani watano wafuatao kwa kosa la kukataa kutekeleza maagizo ya Kamati Kuu:

i) Ndugu Estomih Mallah

ii) Ndugu John Bayo

iii) Ndugu Charles Mpanda

iv) Ndugu Rehema Mohamed

v) Ndugu Reuben Ngowi

Watajwa hapo juu wamejulishwa maamuzi ya Kamati Kuu ndani ya Mkutano tarehe 07 Agosti 2011 saa 7:57 usiku, Aidha, kila mmoja wao atakabidhiwa barua yenye kueleza maamuzi ya Kamati Kuu.
[/QUOTE]
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,869
1,225
CCM; Wamemunua? Kweli hii inafaa kwenye MKUTANO wa HADHARA badala ya kuongelea HOJA na Nini CCM itafanya ili ipendwe na Wananchi wa ARUSHA na Tanzania kwa UJUMLA???
 
Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
42,257
2,000
Hana akili huyao diwani kabisa, alikuwa wapi siku zote kusema hayo????
Usimpangie siku ya kusema leo ndio ni muda muafaka kwake kusema...yaani huyu mama kusema ukweli ndio ana akili, mkuu punguza mapenzi huyo mama kavunjiwa heshima yake. Ukweli siku zote mchungu.
 
Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
42,257
2,000
CCM; Wamemunua? Kweli hii inafaa kwenye MKUTANO wa HADHARA badala ya kuongelea HOJA na Nini CCM itafanya ili ipendwe na Wananchi wa ARUSHA na Tanzania kwa UJUMLA???
Mkuu unataka hoja gani tena zaidi ya hii mama katoa angalizo kwa kina mama wenzake wawe makini na viongozi wa Chadema kwa tabia chafu.
 
politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,250
Yote hayo unayasema baada ya kufukuzwa uanachama swali ulikuwa wapi siku zote usiyaseme unayasema mara baadaya ya kushindwa rufaa yako ya kuendelea kuwa mwanachama na diwani wa chadema. afadhali umewapata akina nape na Jangili Kinana watakulipia hizo milioni 15 mnazodaiwa na chadema kulipa mahakama....umesahau mama na Mbowe pia alikuwa anakutaka pia.
 
Perry

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
9,997
2,000
CCM; Wamemunua? Kweli hii inafaa kwenye MKUTANO wa HADHARA badala ya kuongelea HOJA na Nini CCM itafanya ili ipendwe na Wananchi wa ARUSHA na Tanzania kwa UJUMLA???
kwan nani kakuambia kua wananchi wa arusha hatuipendi ccm?
 
MNYISANZU

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
7,050
1,225
Huyo ni mfa maji tu. Ameoza kama CCM ilivyooza. Apumzike kwenye moto wa milele.
 
Nzi

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
13,830
2,000
Alikuwa wapi alipotakiwa?
Alipeleka malalamiko kwenye vyombo husika vya chama?

Njaa inaharibu fikra za wanasiasa wengi wa kiafrika.

Ila, kuna haja ya watajwa kujitokeza na kuyapinga hayo madai.
Maana hisije ikawa kwamba, "uongo ukisemwa na kurudiwarudiwa, uonekana ndiyo ukweli".

Ingawa wengine wanaamini katika kukaa kimya,linapokuja suala la kumjibu mtu wa namna ya huyu mwanamama.
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,869
1,225
Usimpangie siku ya kusema leo ndio ni muda muafaka kwake kusema...yaani huyu mama kusema ukweli ndio ana akili, mkuu punguza mapenzi huyo mama kavunjiwa heshima yake. Ukweli siku zote mchungu.
HAPO atachuma MAPESA kweli Sababu WAKILI MKOANI ARUSHA amewataka HAO MADIWANI wasaliti wa CHADEMA kuilipa CHADEMA 15M TZ SH's
 
MNYISANZU

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
7,050
1,225
Mkuu unataka hoja gani tena zaidi ya hii mama katoa angalizo kwa kina mama wenzake wawe makini na viongozi wa Chadema kwa tabia chafu.
Najua utakesha hapa maana kichwa chako kimejaa makamasi badala ya ubongo.
 
politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,250
Usimpangie siku ya kusema leo ndio ni muda muafaka kwake kusema...yaani huyu mama kusema ukweli ndio ana akili, mkuu punguza mapenzi huyo mama kavunjiwa heshima yake. Ukweli siku zote mchungu.
na sisi hatuwezi kuipangia CCM siku ya kuokota mizoga ya chadema. CCM inafurahia kuokota mzoga wa chadema kweli ccm imekwisha.
 
Penguine

JF-Expert Member
Nov 29, 2009
1,298
2,000
Usimpangie siku ya kusema leo ndio ni muda muafaka kwake kusema...yaani huyu mama kusema ukweli ndio ana akili, mkuu punguza mapenzi huyo mama kavunjiwa heshima yake. Ukweli siku zote mchungu.
sasa mbona huko alikoenda ndiyo ufuska uliozagaa? Pole mhe.diwani. huko ulikoenda sasa mpaka itapwaya.
 
Lyimo

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,824
1,225
Kwanini hukuyasema hayo wakati upo huko? Na mbona hukujitetea mahakamani kubusiana na kesi yenu ya kufukuzwa ubunge? Wengi tunaamini hiyo ni janja yako ya kutaka CCM ikulipie deni lako mahakamani ili usifungwe.
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,869
1,225
Mkuu unataka hoja gani tena zaidi ya hii mama katoa angalizo kwa kina mama wenzake wawe makini na viongozi wa Chadema kwa tabia chafu.

Real Democratic STATES Mambo ya UZINZI na UASHERATI hauongelewi kwenye MAJUKWAA yenye WANANCHI wengi... Wanaita PRESS CONFERENCE na kuongelea hayo... Wananchi waliokusanywa wanahitaji kusikia HOJA sio UHUNI

Nadhani Unaangalia CHAGUZI za INDIA; USA; UK; FRANCE - hakuna kuanika WAHUNI HADHARANI

NDIO MAANA KWENYA KATIBA MPYA ya KENYA Imekataza KUONGELEA UHUNI; MATUSI kwenye MAJUKWAA ya KISIASA; NA NADHANI KATIBA YETU PIA IFANYE HIVYO...

CLASSY POLITICIANS not LIKE SOME FROM THE GARBAGE BAGS
 
Nzi

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
13,830
2,000
Usimpangie siku ya kusema leo ndio ni muda muafaka kwake kusema...yaani huyu mama kusema ukweli ndio ana akili, mkuu punguza mapenzi huyo mama kavunjiwa heshima yake. Ukweli siku zote mchungu.
Kwa sasa siwezi kuuita ukweli, kwani sijasikia kauli za watuhumiwa.
Pia inatia shaka suala la timing ya yeye kuyasema hayo.

Alifukuzwa uanachama.
Akashindwa na kesi.
Akapaswa kulipia gharama za kesi na fidia.
Akaamua kujiunga na CCM.
Akatangaza kutakiwa kimapenzi na viongozi wa chama.

Mtu makini, lazima uhoji timing ya maneno kama hayo kutoka sasa!
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom