Aliyekuwa anasambaza habari za uzushi za kifo cha Mkuu wa Majeshi atiwa mbaroni

Tena ukizingatia mtu mwenyewe CDF-Chief of Defence Force!. Tatizo taasisi zetu nyingi wasemaji wake hawakupelekwa Shule ya namna ya kufikisha ujumbe kwa Umma panapojitokeza ukakasi .


Na kumpeleka kijana huyu mbele ya Mahakama wakati kama huu nako ni kosa la kiufundi!.
Unless wanajambo jingine nyuma ya pazi.
Kilichoniacha hoi ni taarifa eti DPP amepeleka mahakamani zuio la dhamana!
Kama vile kaua!

Ukivunja sharia ya mtandao...huruhusiwi kupata dhamana!? Au anashitakiwa kwa kosa gani huyu kijana?
 
Kama Kuna UKWELI Ktk. Shitaka Lake, Basi Tuachie Mahakama Itende Haki!! Ila Na Hawa Wengine Wanaoendelea Kuwachochea WATANZANIA, KUWADHARIRISHA Na KUWATUSI Watu!!! SIO Iishie Kwa BAADHI Ya Watu WACHACHE Tu!! Ili WATANZANIA Tuone Sheria Hii Iko MAKINI, Basi Ikate Pande Zote!!
 
Mbona story zimezidi? Mliopo mahakamani mtujuze nini kinaendelea muda huu???
 
Mods Paw Invisible mfanye kazi kwa weledi na uelewa hii habari niliyoileta ni tofauti kabisa na ya mwanzo.
Leo ni mwendelezo alichokisema mahakamani. JF inapoteza hadhi yake taratibu sijui mnafanya hili kwa nan? Yaana mnashindwa kabisa kuelewa hizi ni habari 2 tofauti?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu tenga mda kidogo upitie hiyo sheria ya makosa ya mitandoa.
Hakuna kifungu chochote kinachotutaka tusubilie wasemaji wa mamlaka husika tu ndo wawe watoa taarifa.argument yako haina mashiko.

Kumbuka katiba ndo sheria mama na katiba inatoa right ya kila mtu kuwa informed..how.?tunaweza tugalizungumza na hilo.

Shida sio kutoa au kupata taarifa, hilo najua limekaaje kisheria na kikatiba. Tatizo liko kwenye ukweli wa taarifa yenyewe na namna ya kuitoa au kuipokea. Sasa kama kijana anamtaka cdf ajitokeze ( kama kweli yuko hai ) vinahusiana je na taarifa aliyoitoa? Na kama kweli cdf kafa kijana yuko tayari kuoanisha kifo hicho na taarifa yake vikawa sawa. Je, kama cdf yuko hai, huyu kijana atasemaje? Na atatufidiaje sisi tulioamini uongo wake?

Sheria unayosema inahusu kutoa na kupokea taarifa. Lakini ziwe za kweli na mtoa taarifa awe tayari kuzithibitisha. Kama kijana yuko fit kwenye taarifa zake, tusubiri tuone
 
Mods Paw Invisible mfanye kazi kwa weledi na uelewa hii habari niliyoileta ni tofauti kabisa na ya mwanzo.
Leo ni mwendelezo alichokisema mahakamani. JF inapoteza hadhi yake taratibu sijui mnafanya hili kwa nan? Yaana mnashindwa kabisa kuelewa hizi ni habari 2 tofauti?

umekerwa kama mimi mkuu. sipendi kabisa
 
Last edited by a moderator:
BREAKING NEWS KUTOKA MAHAKAMANI LEO :

Kijana aliyetuhumiwa kwa kosa la kutoa taarifa ya kifo cha mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama aishangaza Mahakama,
Aijibu mahakama kuwa atakubali kuwa amemzushia kifo mkuu huyo wa majeshi kama MWAMUNYANGE au mkuu huyo atajitokeza hadharani na kutoa tamko la uzima wake na vinginevyo atabaki na msimamo wake uleule. Mwanasheria wa CHADEMA Mh JAMES MALLYA ndiye anayeisimamia kesi hiyo.
Je, wadau huyu dogo ana siri gani nyuma ya habari ya tuhuma za MWAMUNYANGE?

Source: Wozap

Mmmh????
 
Breaking news! Kwa taarifa niliyopenyezewa mda huu na source ya kuaminika ni kua mkuu wetu wa wajeda yupo njiani anakuja na atatua leo JNIA ila anatokea kule kwa Mafarao
 
unamanisha mkuu mwamu ni mngoni??? kunauwezekano akawa ndugu yake au nimekuelewa sivyo???

Hapana sijamaanisha hilo nilitaka kujua tu kama uyo dogo ni mngoni maana akina ngonyani ni majina ya wangoni uko. Mengineyo endelea kusikilizia movie inavyoelekea maana tumezoea sterling wa movie mwishoni mwishoni mwa movie lazima akamatwe ateswe sana alafu anakuja kutoka na nguvu ya ajabu na kuua maadui wote. Endelea kusubiria kidogo tu
 
DPP Ana Malmlaka Makubwa Mno, Mi Nimeshuudia Watuhumiwa WENGI Tu, Wakinyimwa DHAMANA Kwa Amri Yake, Although Kisheria Mashitaka Yao Yana Haki Ya DHAMANA!!! Mf. Sheikh Ponda, Mwaka Wa 2 Sasa Yuko Tu Mahabusu, Kwa Mashitaka Ya Kutoa Maneno Ya UCHOCHEZI Na Kufanya Mkutano Bila Ya Kibali!! Ila DPP Wamezuia DHAMANA Yake Kwa Miaka 2 Sasa! Na Hukumu Yake Imekuwa Danadana Tupu!! Sijui Kama 19 Oct 15 .Itatolewa!! Hivyo DPP Lazima Malmlaka Yaondolewe Mikononi Kwake!!
 
Hapana sijamaanisha hilo nilitaka kujua tu kama uyo dogo ni mngoni maana akina ngonyani ni majina ya wangoni uko. Mengineyo endelea kusikilizia movie inavyoelekea maana tumezoea sterling wa movie mwishoni mwishoni mwa movie lazima akamatwe ateswe sana alafu anakuja kutoka na nguvu ya ajabu na kuua maadui wote. Endelea kusubiria kidogo tu

anhaaaa sawa mkuu nmekupata, ngonyani ni wangoni hujakosea
 
Kijana Benedikiti Ngonyani amekamatwa na polisi kwa kusambaza ujumbe katika mitandao ya kijamii kuwa mkuu wa majeshi amelishwa chakula chenye sumu.

==============================


Chanzo: Nipashe





Kapandishwa Mahakamani leo Uliza kawajibu nni Mahakamani
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom