Aliyekuwa akijiita ripota wa star TV na mtoto wa kamanda Kova atupwa jela mwaka mmoja kwa utapeli

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
TV.jpeg

Katavi . Aliyekuwa akiita Ripota wa STAR TV wa Mkoa wa Katavi na mtoto wa Kamanda Selemani Kova anaejulikana kwa jina la Gerald Kova Mkazi wa Mkoa wa Mwanza amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kufanya uapateli na kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu .

Hukumu hiyo ilitolewa hapo jana na Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Mpanda Marko Pagyo baada ya Mahakama kulidhika na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo na upande wa mashitaka .

Mwendesha mashitaka wa jeshi la Polisi WP Salima alidai Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo hapo Februari 8 mwaka huu katika eneo la Hotel ya Madina Manispaa ya Mpanda.

Ilidaiwa kuwa mshitakiwa huyo ambae alikuwa anajitambulisha kuwa ni mwakilishi wa STAR TV yenye Makao yake makuu Mkoani Mwanza na ni mtoto wa Kamanda Selemani Kova alijipatia kwa njia ya udanganyifu Kamera moja aina ya Canoni yenye thamani ya Tshs 3,500,000 Lap top moja na stendi ya Kamera ya video mali ya Elias Mlugala.

Alisema kuwa mtuhumiwa baada ya kuwa amejipatia mali hizo kwa njia ya udanganyika aliondoka Mpanda na kutokomea kusiko julikana huku akiwa ametapeli kamera nyingine kwa Eneresti Kibada aina ya Nikon D 7,200 mali ya Chama cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Katavi yenye thamani ya Tshs 4,900.000.

Mwendesha mashitaka huyo alieambia Mahakama mshitakiwa baada ya kutokomea haikujulikana aliko kuwa amekimbilia mpaka hapo mwezi Agosti alipokamatwa huko Kahama na huko alikuwa ajitambulisha kwa jina la Crispin Masawe na alikamatwa baada ya kuwa amefanya utapeli mwingine wa kujipatia kwa njia ya udanganyifu Lap top moja ya mwandishi wa habari wa Kahama .

Alidai kuwa baada ya kukamatwa alfikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Hahama na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitatu au kulipa faini ya Tshs 100,000 hata hivyo hakuweza kulipa na alikwenda gerezani .

Mwendesha mashita alieleza ndipo Elias na Kibada walipoa taarifa kituo cha polisi cha Mpanda juu ya mtuhumiwa wao kuhukumiwa kifungo hivyo walifanya utaratibu na waliweza kwenda Kahama na kumlipia faini hiyo na kumtowa gerezani na kisha akawa chini ya ulinzi wa polisi na aliweza kusarishwa hadi Mpanda na ndipo alipofikishwa Mpanda na Polisi alipoweza kuonyesha vifaa vyote ambavyo alikuwa amemuuzia mfanya biashara mmoja wa huko Maji Moto Wilayani Mlele Mkoani hapa.

Mshitakiwa Gerald Kova katika utetezi wake kabla ya kusomewa hukumu aliiomba Mahakama imwachie huru kwa kile alichodai kuwa anakunywa dawa ya ARVs kufubaza maambukizi ya ukimwi na anamatatizo ya ugonjwa wa sikoseli pia mama yake mzazi ni mgonywa na anamtegemea yeye.

Baada ya utetezi huo hakimu Paragyo alisoma hukumu na kuamuru mshitakiwa atumikie kifungo cha mwaka mmojs jela na pindi atakapo toka gerezani atatakiwa kulipa Tshs 800,000.

Mshitakiwa huyo anatarajiwa kufikishwa tena mahakamani hapo kwa ajiri ya kesi ya pili inayomkabili ya kujipatia kamera Nicon mali ya Chama cha Wandishi wa Habari ambapo kesi hiyo itaendelea kusikilizwa. MWISHO
 
Mwaka mmoja tu hautoshi kwa utapeli alioufanya, angeongezwa ya kutosha ili awe mfano kwa matapeli wengine kama yeye.
 
Back
Top Bottom