Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,778
Habari ya Jumamosi wapendwa,
Leo nimekumbuka story ya shost,
Shost huyu alikuwa mzuri na mrembo, alianza kujiingiza katika mambo ya ulimbwende akiwa kidato cha V, alipomaliza kidato cha sita aliamua kwenda mjini London kutafuta maisha. Akiwa kule mgeni alikaribishwa na rafiki akiwa anakaa kwenye chumba.
Shost alikutana na Peter (jina la kubuni) kwenye party. Peter alikuwa kijana wa ki-Tanzania ambae alizaliwa Uingereza miaka ya 70 wakati wazazi wake wanasoma huko, baada ya kumaliza kidato cha nne Peter aliamua kwenda kuendelea na maisha mjini London kwani alikuwa na uraia wa kule. Alivyokutana na shost kwenye party Peter alivutiwa sana na uzuri wake. Walibadilishana namba za simu na mawasiliano yalianza pale.
Peter alifanya kazi kama mhudumu wa canteen ya bank moja, kazi yake ilikuwa J3 mpaka Ijumaa na alimudu kununua nyumba ya chumba kimoja cha kulala. Mapenzi yalivyonoga shost alihamia kwa Peter, wakati huo alipata kibarua cha kutandika vitanda kwenye hoteli moja ya 5* mjini. Peter alikuwa kijana anaekwenda na wakati, weekend alikuwa kwenye disco au party, kutokana na nature ya kazi ya shost, mara nyingi weekend alikuwa kazini.
Shost alipopata ujauzito, alimwambia Peter, hapo ndipo kijana alipong'aka kuwa hayuko tayari kuoa ili amsaidie mtu apate makaratasi, mimba itolewe wala yeye hana mawazo ya kuwa kwenye serious relationship, 'he was just having fun'. Kwakuwa shost alikuwa bado kuku mgeni, hajui mbele wala mwisho, aliitoa ile mimba, alipotoka hospitali ndipo alipochukua mabegi yake na kuondoka, alikwenda kupanga chumba na maisha yakaendelea.
Muda ulifika na wazazi wa Peter pia walipenda kijana wao aoe, alikuja nyumbani likizo, na kutambulishwa kwa binti ambae ndiyo amemaliza shule tu. Peter alirudi London na kuanza kujiandaa kuoa, muda ulifika alirudi nyumbani na harusi ya kanisani ilifungwa, msichana alijua amelamba dume, anaolewa na kwenda kuishi London.
Baada ya ndoa wamefika mjini, kwa mshangao bibi harusi anamuuliza Peter, hivi ukisema unaishi London nikijua unaishi kwenye nyumba kumbe ni hiki ki-store. Peter la kujibu hana, binti alimwambia hawezi kutoka ndani na baridi kali eti kwenda kazini, na mimi ni mkeo, ninahitaji pesa ya saloon, shopping, manicure na pedicure. Peter amekuwa mdogo kama piriton.
Harusi ilijibu na walipata mtoto wa kiume, bi dada kumbe alikuwa wale wadada wa kwenda Rose Garden kusubiri mabooz, maisha ya London si aliyoyategemea, amekuwa miserable kuliko neno lenyewe. Peter akiwa kazini anachat na mashost zake bongo, anawaeleza mkenge aliouvaa, hana raha kwenye ndoa. Huku na kule kwenye facebook alikutana na ex boyfriend ambae alikwenda USA. Kuchat mwanaume kaziingiza na dada akajaa, walikubaliana arudi bongo ili aanze kumtengenezea safari ya USA.
J'mosi moja mke anamwambia Peter kaa na mtoto ninakwenda saloon, wakati huo mtoto ana miaka miwili. Kumbe mdada alishatanguliza mizigo kwa mashost, ametoka pale akaenda kuchukua mizigo yake, huyo Heathrow, kurudi bongo. Peter amekaa mpaka saa nne anasubiri mke atoke saloon.
Peter ilibidi awe single father, anampeleka mtoto kwa child minder na yeye kwenda kazini. Maisha yamekuwa magumu, alianza kumkumbuka shost yangu, aliendea marafiki zake, aliuliza habari za shost. Alielekezwa kanisa analosali, J'pili moja anajitokeza kanisani na mtoto wake, anamuomba shost wakayaongee, mwanaume analia machozi. Shost alimwambia yale yamepita, kwakweli nimekusamehe lakini kunihitaji sasa hivi nikusaidie ulezi samahani.
Ulishatendwa na mtu baadae anakuja kuomba msamaha yaishe?