Aliyekatika mikono akamatwa akinyonga usukani kwa miguu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyekatika mikono akamatwa akinyonga usukani kwa miguu

Discussion in 'International Forum' started by Babuji, Nov 30, 2008.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Nov 30, 2008
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Polisi mjini Beijing walipigwa na butwaa baada ya kukuta dereva waliyemsimamisha hana mikono na alikuwa akinyonga usukani kwa kutumia miguu.

  Zing Shen, 42, alisema baada ya kukamatwa kuwa amekuwa akiendesha gari namna hiyo kwa miaka mingi.

  Bwana Zing alisema alipoteza mikono yake baada ya kupata ajali alipokuwa anafanya kazi kiwandani.Aliongeza amekuwa akinyonga usukani wa gari yake ambayo ni Automatic kwa kutumia miguu yake.

  Zing alijigamba kwamba yeye anaendesha gari salama sana kama watu wengine wasiokuwa na ulemavu na aliongeza amekuwa akiendesha kwa uangalifu sana sasa kuliko wakati alipokuwa hajapoteza mikono yake.

  Polisi walisema Zing alikuwa anajiamini sana kutokana na gari yake kuwa Automatic hivyo hakuwa na hofu ya kubadilisha gia.

  Habari kamili na picha za jamaa akiendesha gari gonga hapa NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
Loading...