Aliyekataa rushwa ya mihadarati akabidhiwa milioni 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyekataa rushwa ya mihadarati akabidhiwa milioni 4

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lukwangule, Mar 13, 2010.

 1. L

  Lukwangule Senior Member

  #1
  Mar 13, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali (IGP) Saidi Mwema, leo ametoa motisha ya shilingi milioni 4 kwa askari mmoja wa Viwanja vya Ndege Jijini Dar es Salaam baada ya kukataa kupokea rushwa ya Dolla 3,000 za Kimarekani kutoka kwa mtuhumiwa mmoja wa madawa ya kulevya.
  Akikabidhi hundi ya fedha hizo kwenye mkutano wa askari wote wa Kanda ya dare s Salaam na Makao Makuu ya Jeshi la Polisi uliofanyika kwenye ukumbi wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam, IGP Mwema alisema Jeshi la Polisi linaendeleza utamaduni huo, kama sehemu ya sera za Jeshi lake katika kukabiliana na matendo ya kudai na kupokea rushwa.
  Hiyo ni moja ya utekelezaji wa ahadi ya Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi nchini aliyoitoa mkoani Singida hivi karibuni kuwa askari yeyote atakayekataa rushwa atamzawadia kiasi kama hicho hicho alichokataa kikiwa na ukomo wa shilingi milioni 10.
  Akizungumzia zawadi hiyo leo, IGP Mwema amesema hatua iliochukuliwa na askari ni kitendo cha kishujaa na kuwataka kila mmoja wao kuiga mfano huo ili kujenga heshia yake binafsi na heshima ya Jeshi la Polisi kama Taasisi muhimu.
  Amesema ingawa ni wajibu wa askari wa kusimamia na kulinda sheria lakini pia ni wajibu wa kila askari kukataa kudai ama kupokea rushwa.
  Amesema kitendo cha Konsebo John Mwisongo cha kuchukua rushwa ili abadilishe kielelezo halisi cha dawa alizokamatwa nazo mtuhumiwa na kuweka kingine bandia kama hatu ya kumsaidia kujinasua katika shitaka analotuhumiwa nalo ni jambo la kuigwa na kila askari hapa nchini.
  Hata hivyo IGP amesema kuwa mpango huo utaendelea na ataendelea kutoa zawadi kwa aslimia mia moja kwa askari yeyote atakayekataa rushwa lakini yenye ukomo wa kiwango cha shilingi milioni kumi kutokana na ukomo wa bajeti.
  Amesema kuwa askari wengi ni wazuri na wenye tabia njema na kwamba ni askari wachache tu ndio wanaojihusisha na vitendo viovu ambapo hatua za kinidhamu na kisheria huchukuliwa dhidi yao kila wanapobainika.
  IGP Mwema ametoa wito kwa kila askari kuwa mlinzi kwa mwingine ili kuwabaini na kuwafichua wachache wao wanaokwenda kinyume na taratibu za utumishi kwenye Jeshi hilo.
  Amesema kuwa hivi sasa Jeshi la Polisi linaendelea na mchakato wa kutengeneza sera itakayosaidia kukomesha kabisa vitendo vya rushwa ndani na nje ya Jeshi hilo ambapo pia amesema kinachohitajika ni elimu zaidi kwa Askari na wananchi wenyewe kuchukia na kukataa kutoa ama kushawishi vitendo vya rushwa.
  Awali Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege nchini ACP Mwajuma Kiponza, alisema kuwa Konstebo John ambaye alikuwa ni mtuza vielelezo kwenye ghala la kituo cha Polisi cha Uwanja wa Ndege, alirubuniwa na mmoja wa watuhumiwa wa madawa ya kulevya ili ayabadilishe na kuweka dawa bandia kama hatua ya kumnasua mtuhumiwa huyo na shitaka lake la kupatikana na dawa za kulevya.
  Alisema mara baada ya kuahidiwa kupewa fedha hizo, askari huyo alitoa taarifa kwa uongozi wa Polisi juu ya mpango huo na ndipo ulipowekwa mtego na kumkamata mtuhumiwa huyo akitoa rushwa huku akiwa na pipi 65 za dawa bandia zilizofungwa kwa mfano wa dawa za kulevya ili askari huyo azibadilishe na dawa halisi zinazotunzwa katika ghala hilo la vielelezo.
  Kamanda Kiponza amesema kuwa Polisi pia waliwakamata watuhumiwa wengine wanne ambao walitajwa na mtuhumiwa kuwa walikuwa ni washirika wa madawa ya kulevya ambao pia walikutwa wakiwa na kiasi kingine cha dolla za Kimarekani.
  Kwa upande wake Mkuu wa Mafunzo kwenye Jeshi la Polisi nchini ACP Abdrahaman Kaniki, amesema kuwa mkakati wa makusudi umeundwa ili kujenga ujasiri na nidhamu kwa askari watakaokwenda kinyume na maadili ya Jeshi hilo na kuwapa uwezo Makamanda kuwazawadia ama kuwaadhibu askari watakaofanya vizuri ama kwenda kinyume na maadili kuadhibiwa.
   
 2. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  1. Hongera zake

  2. Kuna ushahid kwamba alipewa hiyo rushwa akaikataa?

  3. Kumbe hela za motisha zipo? Basi si wawekewe sawa maslahi yao?
   
 3. K

  Kosmio Senior Member

  #3
  Mar 13, 2010
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 128
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Bahati kubwa alikoenda kuripoti ngazi za juu nao walikuwa wasafi. La sivyo huyo askari alikwenda na maji. Kuna tabia mbaya ya viongozi wa juu wenye tamaa sana hilo nalo ni tatizo kukomesha rushwa ktk jeshi la polisi na taasisi nyingi hapa nchini. Ombi langu ni Mkuu wa jeshi la polisi akae chini na kuwashauri na kuwasihi viongozi wakuu kuwa mfano mzuri kwa walio chini yao. Wadogo huwa wanaona maovu yanayofanywa na wakubwa wao hicho ndicho kinawakatisha tamaa hao askari wachache waaminifu. Pongezi zimfikie huyo askari mwadilifu.
   
 4. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  that's nice
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Nina wasiwasi sana na baadhi makamanda wakija kuletewa mtego kama huo....watawazunguka hao wadogo wakavuta...mwisho story!!!twalijua rigeshii retuuu
   
 6. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Hatuna uhakika na hil bana. Je hiyo ilikuwa ni rushwa ya kwanza kushawishiwa toka kipindi chote cha kazi yake? Wanatubabaisha tu hawa-Motisha milioni 4? Mh si bora waende kujenga nyumba za hawa mabwana waatoke huku uraiani kama wan mihela yote hiyo kwa ajili ya motisha tu?

  Hii motisha katika bejeti yao huwa inakuwa fungu gani? Na miaka yote manake ilikuwa inaliwa tu? Huyu wa mihadarati na yule aliyepambana na majambazi Ubungo yupi alistahili kupewa motisha kubwa?
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nilidhani ni ulaya kumbe bongo! Mwanzo mzuri chini ya usimamizi wa mtu Mwema
   
Loading...