#COVID19 Aliyekataa chanjo Marekani aitwa Ikulu kuelimishwa umuhimu wa chanjo lakini Tanzania askofu Gwajima aliitwa Tume ya Maadili kukemewa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,702
2,000
Kuna tofauti kubwa kati ya dunia ya kwanza na hii yetu ya third.

Wakati askofu Gwajima akiitwa kwenye tume za maadili za bunge na CCM na kuadhibiwa kwa kuhoji umadhubuti wa chanjo wenzetu kule Marekani ni tofauti kabisa.

Mwanamuziki Minaj baada ya kugomea chanjo kutokana na ushuhuda wa ndugu yake kuvimba korodani baada ya kuchanjwa, Serikali ya nchi yake ya Marekani imemualika Ikulu ili akaelimishwe kwa upana kuhusiana na chanjo ya covid 19.

Mungu ni mwema wakati wote!
 
MKANDAHARI

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
4,408
2,000
Kuna tofauti kubwa kati ya dunia ya kwanza na hii yetu ya third.

Wakati askofu Gwajima akiitwa kwenye tume za maadili za bunge na CCM na kuadhibiwa kwa kuhoji umadhubuti wa chanjo wenzetu kule Marekani ni tofauti kabisa.

Mwanamuziki Minaj baada ya kugomea chanjo kutokana na ushuhuda wa ndugu yake kuvimba korodani baada ya kuchanjwa, serikali ya nchi yake ya Marekani imemualika Ikulu ili akaelimishwe kwa upana kuhusiana na chanjo ya covid 19.

Mungu ni mwema wakati wote!
Wewe si ndo ulikuwa unashadadia "wapigwe" tu wakati wenzetu huko ni mambo ya kawaida?
 
coolboyjden

JF-Expert Member
Apr 10, 2021
288
500
tatizo ikulu yetu bado haina uhakika na chanjo kikubwa tunaenda pamoja sisi sio kisiwa
wenye nguvu wanawin tu leo unachukua chanjo kutoka China unaambiwa haitambuliki unajiuliza haitambuliki na mwili wangu au wenu
Africa tuna technology ndogo sn kujikwamua wenywe ndio maana chanjo itakayo tengenezewa africa itatumika Africa tu na sio vinginevyo
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,322
2,000
Kwa nini usiende moja kwa moja ukamtaja mtu huyo aliyeitwa naye ni Nicki Minaj
 
wakurochi

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
2,503
2,000
Umed
Kuna tofauti kubwa kati ya dunia ya kwanza na hii yetu ya third.

Wakati askofu Gwajima akiitwa kwenye tume za maadili za bunge na CCM na kuadhibiwa kwa kuhoji umadhubuti wa chanjo wenzetu kule Marekani ni tofauti kabisa.

Mwanamuziki Minaj baada ya kugomea chanjo kutokana na ushuhuda wa ndugu yake kuvimba korodani baada ya kuchanjwa, serikali ya nchi yake ya Marekani imemualika Ikulu ili akaelimishwe kwa upana kuhusiana na chanjo ya covid 19.

Mungu ni mwema wakati wote!
USA wamegundua chanjo yao wenyewe. Gwajima anajidai mtalaam wa chanjo ya watu wengine angeenda huko huko kuongea nao na kujielimisha.
Naona hilo umesahau wakati unabandika hii mada korofi.
 
Lukonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
401
500
Kuna tofauti kubwa kati ya dunia ya kwanza na hii yetu ya third.

Wakati askofu Gwajima akiitwa kwenye tume za maadili za bunge na CCM na kuadhibiwa kwa kuhoji umadhubuti wa chanjo wenzetu kule Marekani ni tofauti kabisa.

Mwanamuziki Minaj baada ya kugomea chanjo kutokana na ushuhuda wa ndugu yake kuvimba korodani baada ya kuchanjwa, Serikali ya nchi yake ya Marekani imemualika Ikulu ili akaelimishwe kwa upana kuhusiana na chanjo ya covid 19.

Mungu ni mwema wakati wote!

Jifunze ukataaji wa Minaji pia na ukataaji wa Gwajima na contents zake. Hatua za kuchukua pia zinategemea umbwiga na theories ambazo unazileta zisizo na kichwa wala miguu. Unatumia influnce yako kutoa taarifa usizo na uhakika au ushahidi wa kitaaluma ili kupotosha watu.

Nikiuliza tu swali la jumla:
Kama mtu aliyechanjwa chanjo ambayo ni sehemu iliyopunguzwa makali ya kiumbe husika baada ya miaka miwili atakufa au atakuwa zombi au hatazaa, Je aliyepata kuumwa baada ya kukipata kiumbe kizima/Corona baada ya hiyo miaka miwili unamweleza nini juu ya yaliyotajwa?
 
Kupunguzwa makali hayo kumethibitishwa na nani?

Au ni siasabiashara katikati ya ugonjwa?!!!
 
Lukonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
401
500
Kupunguzwa makali hayo kumethibitishwa na nani?

Au ni siasabiashara katikati ya ugonjwa?!!!

Haya ndiyo mambo ya msingi, nenda kajifunze chanjo zoote/yoyote unazozijua nini hasa?

Pia soma drugs discovery and development, jikite pia kusoma safety of drug molecules during clinical trials and its stages.

Tembelea angalau TMDA upate kujua wanafanyiaje kazi dawa zoote unazozitumia Tanzania hii, hata hiyo Paracetamol au clinical trial moja hapa Tanzania mfano: IHI ujifunze mambo yanaendeshwaje huko.

Soma requirements for a new drug/vaccine/medical device to be introduced into the market in Tanzania under TMDA.

Kama leo huiamini TMDA basi ujue tangu utoto wako mpaka hapo ulipo, umetumia kemikali za sumu kwani ndo wamekufikisha hapo ulipo na ujanja wako unaouona unao. Tafakari!!

Ukimaliza uje na lolote lenye tashwishi.
 
Mafiningo

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
4,071
2,000
Kuna wale waandishi wa habari USA waliokuwa wanapinga CHANJO, BARAKOA, DISTANCING NA NJIA ZOTE ZA KUJIKINGA NA KORONA, wamekufa kwa korona.

Tufanye siku zao ziliwadia, kwa maana hata mfalme Ahabu alipoonywa kuwa vita aiendeayo itamkost akashupaza shingo lake na kweli akaenda akaangamia.

Siku zikifika huwezi chomoa"
 
masopakyindi

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
15,853
2,000
Kuna tofauti kubwa kati ya dunia ya kwanza na hii yetu ya third.

Wakati askofu Gwajima akiitwa kwenye tume za maadili za bunge na CCM na kuadhibiwa kwa kuhoji umadhubuti wa chanjo wenzetu kule Marekani ni tofauti kabisa.

Mwanamuziki Minaj baada ya kugomea chanjo kutokana na ushuhuda wa ndugu yake kuvimba korodani baada ya kuchanjwa, Serikali ya nchi yake ya Marekani imemualika Ikulu ili akaelimishwe kwa upana kuhusiana na chanjo ya covid 19.

Mungu ni mwema wakati wote!
Gwajima ashitakiwe
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,702
2,000
Haya ndiyo mambo ya msingi, nenda kajifunze chanjo zoote/yoyote unazozijua nini hasa?

Pia soma drugs discovery and development, jikite pia kusoma safety of drug molecules during clinical trials and its stages.

Tembelea angalau TMDA upate kujua wanafanyiaje kazi dawa zoote unazozitumia Tanzania hii, hata hiyo Paracetamol au clinical trial moja hapa Tanzania mfano: IHI ujifunze mambo yanaendeshwaje huko.

Soma requirements for a new drug/vaccine/medical device to be introduced into the market in Tanzania under TMDA.

Kama leo huiamini TMDA basi ujue tangu utoto wako mpaka hapo ulipo, umetumia kemikali za sumu kwani ndo wamekufikisha hapo ulipo na ujanja wako unaouona unao. Tafakari!!

Ukimaliza uje na lolote lenye tashwishi.
Mtaalamu mmoja wa medical aliyejikita kwenye vinasaba alishanishawishi kwenye maelezo yake bwashee.

Kwamba binadamu alianzia Afrika na baadae ndio wakaanza kutoka nje ya bara wakiwa ndugu kwa ndugu na wakaenda huko na kuzaliana.

Hivyo wakawa na vinasaba vinabyowiana tena ni dhaifu ila Afrika vinasaba vyetu vimeingiliana mno kutoka Pembe moja hadi nyingine yaani Bukoba hadi Mtwara ndio maana tuko very strong.

Akasisitiza kuwa kwa udhaifu wao wale wahamaji ambao hata ngozi zao zimeungua ndio wenye ulazima wa chanjo.

Afrika huathirika zaidi na magonjwa ya kutengeneza siyo ya asili.
 
Mambo ya msingi pia, naelewa uimara huo. Haiitaji medical knowledge, hata watu wa historia wanayafahamu haya, hasa waliojishughulisha na biashara ya utumwa. Na ndo utofauti uliojitokeza kwa athari za Covid, je udeke kwa sababu ya maelezo hayo tu?

Suala ni katika haohao waafrika bado kuna risk groups.

Nenda kwenye mtandao kasome anti-vaccine groups zilivyowini baadhi ya mataifa hapo kabla na yale ya Africa yakiwemo yalipoacha chanjo za chini ya miaka mitano nini kiliwakuta mfano: Nigeria.

Ya kuambiwa changanya na akili yako.
Unasema huchukui hatua, wewe unaenda kuwaua rafiki, jirani, ndugu na wazazi wako walioko kwenye risks kwa kuwapelekea matatizo.
Think big.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom