Aliyekamatwa na ‘unga’ Zanzibar kufikishwa kortini

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=1][/h]Written by Ashakh (Kiongozi) // 08/05/2012 // Habari // 2 Comments

Imeandikwa na Khatib Suleiman, Zanzibar; Tarehe: 7th May 2012
MKAZI wa Magomeni Makuti mkoani Dar es Salaam, Othman Bonde (35), anatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Zanzibar baada ya kukamatwa na kiwango kikubwa cha dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaan Karume wiki moja iliyopita.
Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Muhibu Juma Mshihiri alithibitisha kukamatwa kwa kijana huyo na kusema taratibu zinafanyika ili kumfikisha mahakamani.
Akifafanua zaidi, Mshihiri alisema Bonde alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amaan Karume akiwa katika ndege ya Shirika la Ndege la Oman Airline akitokea Sao Paul nchini Brazil.
Bonde alikamatwa uwanjani hapo baada ya kutiliwa shaka na wafanyakazi wa uwanja huo wakiwamo askari polisi, ambapo uchunguzi ulianza.
Pipi 105 zilitolewa na mtuhumiwa kwa njia ya haja kubwa wakati pipi sita zilitapikwa na mtuhumiwa. Kwa mujibu wa tiketi ya ndege ya Bonde, alikuwa akitoka Sao Paulo na kupitia Oman na kutumia ndege ya shirika hilo ambayo ilimfikisha hadi Zanzibar.
“Tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha uchunguzi na mtuhumiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazomkabili za kusafirisha madawa ya kulevya na kuyaingiza nchini,” alisema Mshihiri.
Hicho ni kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kukamatwa katika uwanja huo wa ndege kwa mwaka huu.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeimarisha vifaa vya ulinzi vya kugundua dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaan Karume kwa ajili ya kudhibiti kasi ya uingizaji wa dawa hizo katika njia kuu ya uwanja wa ndege pamoja na Bandari ya Malindi.
Aidha, Serikali ipo katika hatua za mwisho za kupeleka mbwa ambaye hunusa na kutambua dawa za kulevya pamoja na vitu vyengine hatari ambavyo havitakiwi kuingizwa nchini.
Chanzo: Habari Leo
 
si anyongwe mnamchelewesha nini? atatolewa am ndugu zake mafisadi then after one year ataleta tena madawa huko ...ingekuwa china nadhani mmeshajua
 
Hebu nisaidieni si udini maana sina nataka tu nielewe ni kwa nini kwa Tanzania anayekamatwa na madawa ya kulevya ni waislam wengi? Ukiacha wa nchi za nje ambao majina yao mengi pengine ni pagani au wakristu? Yaani Tanzania akikamatwa iwe mainland or Zanzibar kwa dawa au ualikaida ni wao tu!!!!! Wana moyo na roho ngumu au ni wavivu hawataki kazi ngumu au? Nisaidiwe kufahamu wakuu.
 
Zuberi Musa aliyekamatwa na unga kule china Kanyongwa leo, sasa sisi tunaanza kuisumbua mahakama kwa jambo la linaloeleweka kwa nini?
 
labda ulikuwa mzigo wa Carlos, yule muuza magari maeneo ya airport ya Karume
 
Huyo alie kamatwa hata akifika mahakamani ushahidi ushapotezwa na jeshi la police zamaniiii,kunaweza kukapelekwa saruji huko court,haya tumeyaona mengi hapa zanzibar,baadhi ya wafanyakazi wa jeshi la police wanaongoza kwa rushwa,wazo langu mimi,security ambayo inatakiwa itumike katika airport na port iwe ni za mashirika binafsi ili kuweza kuipa serikali nafasi zaidi kupambana na rushwa na majambazi ya madawa ya kulevya kama haya.
 
Hebu nisaidieni si udini maana sina nataka tu nielewe ni kwa nini kwa Tanzania anayekamatwa na madawa ya kulevya ni waislam wengi? Ukiacha wa nchi za nje ambao majina yao mengi pengine ni pagani au wakristu? Yaani Tanzania akikamatwa iwe mainland or Zanzibar kwa dawa au ualikaida ni wao tu!!!!! Wana moyo na roho ngumu au ni wavivu hawataki kazi ngumu au? Nisaidiwe kufahamu wakuu.
wengi wao ni wakazi wa dar ambao ni wialam,kama vile wachuna ngozi,wauaji albno wengi ni wakristo
 
Hebu nisaidieni si udini maana sina nataka tu nielewe ni kwa nini kwa Tanzania anayekamatwa na madawa ya kulevya ni waislam wengi? Ukiacha wa nchi za nje ambao majina yao mengi pengine ni pagani au wakristu? Yaani Tanzania akikamatwa iwe mainland or Zanzibar kwa dawa au ualikaida ni wao tu!!!!! Wana moyo na roho ngumu au ni wavivu hawataki kazi ngumu au? Nisaidiwe kufahamu wakuu.
Tembelea nchi inayoitwa Colombia uone Wagalatia wazalishaji na wasambazaji walivyoiteka nchi kwa hiyo biashara! Pia huo unga ameuchukuwa Brazil ambako juu ya mlima kuna sanamu kuubwaa ya BWANA !
 
Back
Top Bottom