Aliyejisifia Kwa Mambo ya Ngono Kuchapwa Bakora 1,000 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyejisifia Kwa Mambo ya Ngono Kuchapwa Bakora 1,000

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbonea, Oct 9, 2009.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  </SPAN>


  Abdul-Jawad akiwa kitandani akielezea jinsi alivyomla uroda jirani yake wakati huo akiwa na umri wa miaka 14.

  Mwanaume wa Saudi Arabia ambaye alijisifia kwenye kipindi cha luninga kuhusiana na utaalamu wake wa mambo ya ngono na kumla uroda jirani yake wakati alipokuwa na umri wa miaka 14, amehukumiwa kwenda jela miaka mitano na kuchapwa bakora 1,000.


  Mazen Abdul Jawad mkazi wa mji wa Jeddah nchini Saudi Arabia alikamatwa baada ya kuhudhuria kipindi kinachoitwa "Red Line" kinachoandaliwa na televisheni ya LBC yenye makazi yake nchini Lebanon.

  Katika kipindi hicho ambacho kina watazamaji wengi nchini Saudia, Jawad alijisifia jinsi alivyokuwa akifanya mapenzi na wanawake mbali mbali na kuendelea kujisifia kuwa alianza kufanya mapenzi tangia alipokuwa na umri wa miaka 14.

  Kipindi hicho ambacho kilirushwa hewani julai 15 mwaka huu, kilisababisha hasira kubwa toka kwa wananchi wa Saudi Arabia.

  Takribani watu 200 walifungua mashtaka ya malalamiko dhidi ya Abdul Jawad, ambaye ni mfanyakazi wa shirika la ndege la Saudia.

  Serikali ya Saudia iliamua kuchukua hatua kali kwa kuzifunga ofisi mbili za LBC nchini humo na kumkamata na kumfungulia mashtaka Abdul-Jawad.

  Kipindi hicho kilianza kwa kumuonyesha Abdul-Jawad, akielezea jinsi alivyomla uroda jirani yake wakati huo akiwa na umri wa miaka 14.

  Baada ya hapo aliwaongoza watazamaji kwenye chumba chake ambacho chenye karibia vitu vyote ni vya rangi nyekundu na aliwaonyesha pia toys zake za ngono.

  Baada ya hapo alijiunga na wanaume wengine watatu na kuanza kujadiliana masuala ya ngono.

  Mahakama ya nchini Saudia ilimuona Abdul-Jawad ana hatia na ilimhukumu kwenda jela miaka mitano pamoja na kuchapwa jumla ya bakora 1,000. (ELFU MOJA).

  Mbali na adhabu hizo, Abdul-Jawad amepigwa marufuku kusafiri kwa kipindi cha miaka mitano akishatoka jela na pia hataruhusiwa kuongea na vyombo vya habari kwa kipindi cha miaka mitano baada ya kumaliza kifungo chake.

  Mwanasheria wake alitangaza kuwa atakata rufaa hukumu hiyo na alidai kwamba Abdul-Jawad alikuwa akielezea maisha ya mapenzi ya watu wengine.

  Mwanasheria huyo alidai kwamba televisheni ya LBC ilikuwa ikimrekodi mazungumzo yake bila ya mwenyewe kujua kwamba anarekodiwa.

  Wanaume wengine watatu ambao walichangia mawazo yao katika mjadala wa mapenzi wa Abdul-Jawad walipatikana na hatia ya kujadili masuala ya mapenzi hadharani na walihukumiwa kwenda jela miaka miwili na kuchapwa bakora 300 kila mmoja.

  Source: Daily Nation
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  HII KALI!
  Unafiki ulioje? Mbona wanakuja TZ na na sehemu nyingine duniani na kujirusha na wanawake au kwa vile wako daraja tofauti?
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  VC, NILITEGEMEA UMSHANGAE HUYO JAMAA NA SI VINGINEVYO!Yaelekea umeshakubaliana na wanaJF waliokuponda kwenye mada yako ya `wanaume wanapenda kila mwanamke anayechomoza mbele yake`!By the way, nae huyu jamaa, kwanini atambe mbele za watu juu ya kufanya ufuska mwingi hivyo...mbona kuna watu tunaowajua live wamefanya makubwa kuliko yake, lakini hawabwatuki vilevile!!
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nawashangaa wote - huyo jamaa na waliompa adhabu ambayo kwangu naona ya kipuuzi!
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  MWANAUME NI KAMA PANYA, KILA AKIONA SHIMO ANATAKA ACHUNGULIE HAHAHAHA hawa MAARAB tunawajua sana hata huko kwao wanayafanya lkn kwa kujificha tena wao wanatumia sana huu mtandao wetu wa bei rahisi T*&^%$# hahaha
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Watu bana!Kwanini mnapenda kubadilisbadilisha maneno namna hiyo?Kwanini mnaidhalilisha TIGO kihivyo? Kama sio umbea, VOda inamaanisha nini, Zain je, maana hii ndo ya mwarabu kabisa, na TTCL ndo kiungo gani cha mwili?Huh...! Shame on you all!
   
 7. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona hapa tz wapo wengi tu mfano GONGA GONGA wa dom?
   
Loading...