Aliyejichoma moto kupinga ukosefu wa ajira afariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyejichoma moto kupinga ukosefu wa ajira afariki

Discussion in 'International Forum' started by kilimasera, Jan 27, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MUHITIMU wa Chuo nchini Tunisia ambaye aliamua kujitoa mhanga kwa kujichoma moto akipinga kukosekana ajira nchi nzima katika taifa hilo la Afrika Kaskazini amefariki dunia.Habari kutoka nchini humo zimeeleza kuwa Mohammed Bouazizi, (26) alifariki juzi jioni hospitalini nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo, Tunis.

  Kabla ya kifo chake, Bouazizi alikuwa akiuza matunda na mboga mboga kinyume cha sheria katika mji wa Sidi Bouzid baada ya kukosa ajira.

  Mwezi uliopita aliamua kujimwagia mafuta na kujitia kiberiti baada ya polisi kuaribu bidhaa zake kutokana na kutokuwa na kibali maalumu.

  Mmoja wa maofisa wa Serikali katika mji huo, Kamel Laabidi amesema kuwa watu wapatao 5,000 walihudhuria mazishi hayo yaliyofanyika jana katika makaburi yaliyopo karibu na mji huo wa Sidi Bouzid.

  Ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa, AFP kwamba waombolezaji walikuwa wakisema kuwa Kwa herini, Mohammed, sisi tutalipiza kisasi kwa ajili yako. Sisi leo tunalia leo hii kwa ajili yako, tutawafanya wale ambao wamesababisha kifo chako walie,".

  Mjomba wa marehemu, Mehdi Horchani naye ameliambia Shirika hilo la AFP kuwa Polisi walilazimika kuzuia umati mkubwa watu kufika nje ya ofisi ya gavana ambako Bouazizi alijilipulia.

  "Muhammad alitoa maisha yake kwa kuonesha umakini na hali yake na kwa ndugu zake, " alisema Horchani.

  Naye Rais wa nchi hiyo, Zine al-Abidine Ben Ali,ambaye ameitawala Tunisia kwa muda wa miaka 23, amezishutumu ghasia hizo ambazo zilisababisha mwandamanaji mmoja kuuawa baada ya polisi kufyatua risasi.
   
 2. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,713
  Likes Received: 3,119
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona kila siku unatuwekea habari za mwaka 46 tulishasoma hii habari kitambo. Tafadhali fanya utafiti kabla hujatuma post. Ni wakati wa kukumbushana tu.
   
 3. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #3
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,286
  Likes Received: 808
  Trophy Points: 280
  Du wewe ndio mtabiri kwani baada ya hapo ndipo mapinduzi ya Rais huyo wa Tunisia na Mubarak wa Misri yalipoanzia,hata hapa kwetu kuna kijana kajilipua moto baada ya maisha yake kuwa magumu na ndugu kutomsaidia deni la sh 700,000/= likafikia riba ya sh 1,300,000/=
  habari kamili ya si ya mwaka 46 ni ya leo na hata kesho ifundishwe madarasani 'mnyonge akibanwa kwa tofauti kubwa ya maisha tajiri yuko hatarini
  maelezo zaidi bofya Mohamed Bouazizi - Wikipedia, the free encyclopedia
   
Loading...