Aliyejenga Nyumba Mpaka wa Tanzania na Kenya Afunguka.

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,440
16,242
Juma Ally, aliyejenga nyumba katikati ya mpaka Tanzania na Kenya katika kijiji cha Jasini wilayani Mkinga Mkoa wa Tanga amesema haoni
tatizo nyumba yake kuwa eneo hilo.

Amesema nyumba hiyo ipo katikati ya mpaka huo, na baadhi ya vyumba vyake vipo upande wa Tanzania na vingine upande wa Kenya.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Februari 14, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Damas Ndumbaro na naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji kutembelea kijiji hicho.

Katika ziara yao hiyo mawaziri hao walikumbana na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na suala la mipaka.

Katika maelezo yake, Juma amesema kuwa wao ni wakazi wa muda mrefu katika eneo hilo na hata huduma za kijamii wanazipata kutoka Kenya.

Amesema licha ya kupata huduma hizo Kenya, wao ni Watanzania.

“Nilivyojenga nilijua nimejenga Tanzania kwa kuwa ni nchi yangu ila baada ya mawaziri kufika hapa ndio nikasikia kuwa nyumba yangu iko upande wa Kenya na Tanzania,” amesema Juma.

Source: Mwananchi
 
huyo siyo Mtanzania wala mkenya! huyo ni mpemba!!!! aliulizwa swali!
Achague upande mmoja wa kubomoa vyumba ktka nyumba yake kati ya Kenya na Tanzania! yeye akajibu Bora abomoe "nyumba nzima" Aende zake PEMBA
 
Hahaa
 
Hivi Mpemba sio Mtanzania?

Sijui ulienda kusomea ujinga shule?

This ignorance is too gross!
 
Sheria za mipaka za kimataifa eneo alilojenga haliruhusiwi shughuli yeyote ya kibinadamu (mita kadhaa kila upande wa mpaka kama sio 50 ni 500) isipokufa ofisi za border wao huliita no mans land
 
Huyu nae asilete mbwembwe zisizo za lazima. Kwa nini asichague upande mmoja au ana ajenda gani isiyo wazi mahali hapo?
 
Hivi Mpemba sio Mtanzania?

Sijui ulienda kusomea ujinga shule?

This ignorance is too gross!
alokwambia mpemba ni mtanzania umekaririshwa! wale ni taifa jingine kabisa!ndiyo maana ukichukua kitu kwao kuleta bongo lazima ulipie ushuru
 
alokwambia mpemba ni mtanzania umekaririshwa! wale ni taifa jingine kabisa!ndiyo maana ukichukua kitu kwao kuleta bongo lazima ulipie ushuru

Mbuzi wewe...

Definition ya taifa ni "ukilipia ushuru mahali"?

Hiyo definition ya taifa?

Mtu wa mainland China anapolipia ushuru akitoa kitu Hong Kong inamaanisha Hong Kong sio sehemu ya taifa la China?

Taifa jingine umesema wewe kwa akili zako binafsi...sio rekodi rasmi zilizopo!

Kwahiyo Pemba ni "Taifa la Pemba"?

Mpemba anabeba passport imeandikwa "Passport ya Pemba"?

Mbuzi wa maziwa kabisa.......

Ficha ujinga wako onyesha werevu wako...Kitu umesoma kwa miaka 14 leo unajifanya hamnazo!
 
msamehe asee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mipaka ya kikoloni hiyo viongozi wa pande zote mbilii waipuuze, sisi wote ni waafrika
 
Mbuzi wewe...

Definition ya taifa ni "ukilipia ushuru mahali"?

Hiyo definition ya taifa?

Mtu wa mainland China anapolipia ushuru akitoa kitu Hong Kong inamaanisha Hong Kong sio sehemu ya taifa la China?

Taifa jingine umesema wewe kwa akili zako binafsi...sio rekodi rasmi zilizopo!

Kwahiyo Pemba ni "Taifa la Pemba"?

Mpemba anabeba passport imeandikwa "Passport ya Pemba"?

Mbuzi wa maziwa kabisa.......

Ficha ujinga wako onyesha werevu wako...Kitu umesoma kwa miaka 14 leo unajifanya hamnazo!

Kumbe tuna mbuzi humu!
 
FAHAMU: Hii nyumba ipo wilayani Mkinga(Tanga) ambapo inaleta utata wa kidiplomasia. Chumba kimoja kipo Kenya na chumba kingine kipo Tanzania (aliposimama NW Dkt. Damas Ndumbaro). Mwenye nyumba akitaka kula mirungi anakaa nje ya nyumba upande wa Kenya na askari wa Tanzania hawamfanyi kitu.
50759431_1120568488115705_1798284203002039341_n.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom