Aliyeishuhudia ajali iliyoua dereva bodaboda Goba saa 1 usiku (8-6-2021), tufahamishe ilivyokuwa

Kwa jinsi Dereva ' Bodaboda ' alivyokuwa kaumia vibaya Kichwani na Kuburuzwa nilishindwa Kujizuia na Kusikitika sana tu na kujikuta nakimbia (natoka Baru) eneo la Tukio kwa Kiwewe na kwenda 'Kuisikilizia' Ajali kwa mbali.

Najua (Huenda) Tukio lile lilishuhudiwa na mwana JamiiForums mwingine hivyo naomba asimulie hali nzima ilivyokuwa. Ni Ajali iliyotokea Goba Saa 1 Usiku wa leo Jumanne.

Jamani Wadogo zetu na Kaka zetu mnaoendesha hizi ' Bodaboda 'hasa' Kibiashara ' jioneeni Huruma jinsi mnavyokufa na kulemazwa hovyo kwa Ajali za Barabarani kwa Kuendesha kwa Nidhamu, kuwa Makini na kufuata sana Sheria. Taifa linawahitaji mno tu.
Kwa taarifa yako
Bodaboda anapoondoka geto kwake ahsubuhi, huwa anaikunja roho yake vizuuri na kuiweka sandukuni kisha anatoka akiwa kiwiliwili kitupu.. Ndo maana wanatatarika barabarani kama kuku mwenye kideri aliyepakwa pilipili kunako makalio
 
kuna dogo pia hapa mtaani leo nimeletewa daftari la michango,maskini ni mdogo sana hata 25 hajafika.amekutana na fuso ikapita nae!yaani nimesikitika kwa maelezo ya wenzie ni kwamba fuso ilimpanda kabisa miguuni hivyo mguu mmoja kuanzia kwenye paja umekatwa!!huo mwingine una afadhali
Acha wafe TU Ni malimbukeni,hawana nidhamu,wanagonga watoto wadogo barabarani na kukimbia bila kusimama kuwasaidia,nasema acha yafe mpaka watakapopata akili.
 
Wanagonga magari ya watu na kukimbia, wanagonga wapita njia kwenye sehemu maalum ya wapita njia. Yaani wana laana zote
 
Hawa jamaa wanagonga Magari ya watu alafu wanakimbia kwenye Trafic jam
Wanatembea na laana za watu hawa
 
Nliona ajali mbaya ya boda.
Walikuwa wanachanga elf 2 kila mshiriki then wanaanza kufukuzana, wa kwanza anazichukua zote. Basi bwana wakawa wamechanga 3 elf 6. Wakaanza kufukuzana. Umbali wenyewe kama mita 100 tu na kurudi walipotoka. Wameondoka vizuri tu sasa kama mita 50 kulikuwa na vx zile za zamani ishapigwa ngao, imepaki pembeni mwa barabara, kulikuwa na kona ya kijinga kijinga hivi, mmoja wa nyuma sijui alijichanganya aje akaingia mzima mzima kwenye vx. Nakwambia aliishia humo akatokezea nyuma akapitiliza hadi mtaroni akiwa keshakufa tayari. Dam yake ilichuruzika nyingi umbali mrefu tu
Hili ni janga la kitaifa.......Hivi ni Tz tu au ni Dunia nzima kwa ujumla?
 
nilikuwepo inatisha sana maana mdau alikua anatoka damu puani na mdomoni kwa kifupi amekufa kwa mateso sana mpaka inasikitisha aise na inasemekana alianguka mwenyewe bila kuguswa na gari yeyote.
Mh! Kapigwa juju huyooo
 
Kuna Mmoja mwaka Juzi niko Tegeta Masaiti akanipita kwa Spidi Kali huku akiwa anafanya Mbwembwe ( Mikogo ) yake mbele kidogo akakutana uso kwa uso na IST kwa Hasira niliyokuwa nayo dhidi yake na ukizingatia hata Nauli ya ninakokwenda ilikuwa haijatimia nilipomkuta katupwa Mtaroni akiwa anakaribia kuiacha Dunia wala sikuhangaika nae sana nilimsachi Mfukoni nakukuta ana ' Jero ' tu Pumbavu yule na ' Condoms ' kama Mbili ambazo ' nilizikomba ' zote na kumuacha pale pale ila Simu yake nzuri sikumchukulia kwani shida yangu ilikuwa ni hiyo Nauli tu na zile ' Condoms ' nilizozibahatisha Kumkuta nazo.
 
Msiwe wepesi wa kuhukumu, kuna watu wana roho nyepesi mno hawawez kabisa kuangalia ajali hasa ya mtu aliyeumia kama hivyo mana inawaathiri kisaikolojia.Mtu unaweza kukuta mwezi mzima na zaidi hilo tukio la ajali halijamtoka kichwani na linamdisturb vibaya

Sent from my SM-G900I using JamiiForums mobile app
Upo sahihi kabisa.!
 
nilikuwepo inatisha sana maana mdau alikua anatoka damu puani na mdomoni kwa kifupi amekufa kwa mateso sana mpaka inasikitisha aise na inasemekana alianguka mwenyewe bila kuguswa na gari yeyote.
Pengine alikuwa na kifafa
 
Kwa jinsi Dereva ' Bodaboda ' alivyokuwa kaumia vibaya Kichwani na Kuburuzwa nilishindwa Kujizuia na Kusikitika sana tu na kujikuta nakimbia (natoka Baru) eneo la Tukio kwa Kiwewe na kwenda 'Kuisikilizia' Ajali kwa mbali.

Najua (Huenda) Tukio lile lilishuhudiwa na mwana JamiiForums mwingine hivyo naomba asimulie hali nzima ilivyokuwa. Ni Ajali iliyotokea Goba Saa 1 Usiku wa leo Jumanne.

Jamani Wadogo zetu na Kaka zetu mnaoendesha hizi ' Bodaboda 'hasa' Kibiashara ' jioneeni Huruma jinsi mnavyokufa na kulemazwa hovyo kwa Ajali za Barabarani kwa Kuendesha kwa Nidhamu, kuwa Makini na kufuata sana Sheria. Taifa linawahitaji mno tu.

Au wewendiye uliyesababisha ajali nini?
 
Huyu naye atakuwa alisoma pale SAUT Malimbe
 
Back
Top Bottom