Aliyeiokoa nmb isife,ateuliwa kuwa kamanda wa uvccm mbeya

Taswira

JF-Expert Member
Sep 23, 2012
1,198
0

NA Gordon Kalulunga, MbeyaMTAALAM wa kutegemewa katika mifumo ya benki barani Afrika, Oran Njeza, ameteuliwa kuwa kamanda wa Jumuiya ya vijana wa CCM(UVCCM), wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani hapa.


Akizungumzia uteuzi huo, Njeza alisema kuwa ameupokea kwa furaha baada ya kurudi nyumbani nchini Tanzania na kujishughulisha na kilimo mkoani Mbeya.


‘’Nimefanya kazi nchini nikianzia ofisi ya Waziri Mkuu, nikawa Mhadhili wa chuo cha SAUTI, nikaenda nchini Marekani katika masuala ya benki, Afrika kusini, Uingereza na nikaja kuifufua benki ya NMB ilipokuwa ikitakiwa kufufuliwa au kuuawa huku vitu vyote vizuri wakiwemo wafanyakazi wakipelekwa NBC’’ alisema Njeza.


Alisema kazi yake kubwa kwa sasa ni kusaidiana na jamii katika maendeleo na alitakiwa awe kiongozi wa benki nchini Kenya lakini kwasababu yeye anapenda zaidi kilimo ameamua kujikita katika kazi hiyo.


Mwenyekiti wa UVCCM wilayani humo, Msafiri Mwashambwa, alimshukuru kamanda huyo kuupokea uteuzi huo ambao umepitia ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya wilaya, Mkoa mpaka Taifa.


Katibu wa jumuiya hiyo, Christina Hussein, alimwambia Njeza kuwa, ajiandae kuapishwa baada ya taratibu za mkoa kukamilika na baada ya hapo atafanyiwa sherehe kisha naye kuwaapisha makamanda wa UVCCM, wa kata za chama hicho.


Naye katibu msaidizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo, Kumotola Kumotola, alimwambia kamanda huyo kuwa, vijana wanategemea busara zake ili kusonga mbele.
 

Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,195
Pongezi kwake, bila shaka amebahatika kuwa mmoja wa wahanga watakaoshuhudia CCM kikizikwa rasmi mwaka 2015.
 

omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,162
2,000
Pongezi kwake, bila shaka amebahatika kuwa mmoja wa wahanga watakaoshuhudia CCM kikizikwa rasmi mwaka 2015.
Huyu anaonekana ni mtu mzuri sana na mwenye moyo wa kuisaidia nchi yake lakini ni wazi anaweza kuwa ameingia kwenye kundi ambalo sio. Nikimuangalia Prof. wa nishati na wa ardhi naye naona anaelekea kuwa kama hao, angelitulia na kuchagua kundi lingine angeliweza kuitumikia jamii kwa ufanisi nadhani.

 

Maga

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
329
225
Oran njeza aliikoa nmb isife?? Dah kweli watu wanajua kuongea, hebu muulize kilichomuondoa nmb ni nini??!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom