Aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa na Mwanasheria Mkuu (Werema) ashinda rufani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa na Mwanasheria Mkuu (Werema) ashinda rufani

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by VIKWAZO, Jun 20, 2011.

 1. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mahakama ya Rufani, imetengua adhabu ya kifo dhidi ya Evelina Ngatala mkazi wa mji mdogo wa Makambako Wilaya ya Njombe mkoani Iringa, ambaye alihukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kumtia hatiani kwa kosa la kumuua bila kukusudia mtoto mchanga wa siku tisa.

  Ngatala, alipewa adhabu hiyo Disemba 18, 2007 baada ya Jaji aliyekuwa akisikiliza shauri hilo Frederick Werema, (Sasa Mwanasheria Mkuu wa Serikali) kumtia hatiani kwa kosa la kumuua mtoto huyo, akidaiwa kumpa sumu inayotumiwa kuulia wadudu kwenye mazao ya nafaka.

  Ilidaiwa mahakamani hapo kwamba mshitakiwa huyo alisababisha kifo cha mtoto huyo baada ya kwenda kumtembelea nyumbani kwao, kisha kumshauri mama yake, wakae nje kwa madai kuwa ndani kulikuwa na joto.

  Mbele ya jopo la majaji wa Mahakama ya Rufaa linaloongozwa na Jaji Euserbia Munuo iliendelea kudaiwa kuwa baada ya kutoka nje, mama wa mtoto huyo aliingia ndani kuchukua maji ya kunywa, lakini alipotoka tena nje, alishangaa kuona mshitakiwa akiwa amempakata mtoto huku povu likimtoka mdomoni mtoto huyo.

  Ilielezwa kuwa mama wa mtoto huyo, alipoona mabadiliko ya mwanae, aliamua kupiga yowe jambo liliwakusanya watu na baadaye kwenda kwenye ofisi za kijiji, lakini wakiwa huko mtoto huyo alifariki.

  Hata hivyo, ilidaiwa kuwa shahidi wa kimazingira, ulitumiwa na mahakama kuu ya Tanzania kumhukumu adhabu ya kifo, Eveline Ngatala kwa kusababisha kifo cha mtoto huyo kwamba haukidhi mahitaji kiasi cha kusababisha, mteja wake ahukumiwe kunyongwa hadi kufa.

  Wakili aliyekuwa akimtetea mshitakiwa huyo, Onesmo Francis, aliiomba mahakama hiyo kumwondolea mteja wake huyo adhabu iliyohukumiwa kutokana na ushahidi wa kimazingira uliokuwepo kutokidhi mahitaji.

  Wakili mwandamizi wa serikali, Andikalo Msabila, alikubaliana na upande wa utetezi, na kuiomba mahakama hiyo kutengua adhabu iliyotolewa kwa mrufani huyo.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  hicho ndicho kipimo tosha na ushahidi kuwa huyu bwana ndiyo maana alisema "KATIBA MPYA HAPANA"
   
 3. D

  DURACEF JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 244
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  mambo hayo......mara ya mwisho sheria ya kunyongwa ilitekelezwa lini?
   
 4. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  wewe sawa hpja yako mkuu, unataka kusema nini? kwamba hii issue ya uongo au ilikuwa sawa huyo mtu kuhukumiwa kunyongwa maana hiyo sheria haitekelezwi?
  kama unauliza mara ya mwisho ni lini jibu ni kwamba hiyo sheria ipo so uwezi kusema mara ya mwisho kutekelezwa sheria hipo
   
 5. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  wakichunguza kuna wengi aliwakatili kutoka na upeo wake wa kisheria
  siju kwenye mikataba ya serikali inakuwaje huko
   
 6. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ameachiwa huru au atafungwa miaka mingapi?
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Tuliwahi kujiuliza huko nyuma kuwa jamaa huyu werema anaweza kuwa ametoa hukumu za utata kutokana na ufinyu wa akili zake
   
 8. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  sijui zaidi ya hapo ila inaonyesha hana hatia maana misingi iliyomtia hatia haina nguvu hivyo ni wazi ni mtu huru
  kashinda rufani
   
 9. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  nadhani huyu jamaa hana huruma kesi zake zote alizosimamia zichunguzwa upya
   
 10. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
  Najaribu ku-imagine kama High court ingekuwa mahakama ya mwisho, huyu mama angelinyongwa bure!!!!!!!!!!!!!!!. Mwanasheria Mkuu sasa anatoa hukumu inatenguliwa, sijui, mimi sio mwanasheria lakini inatia shaka na weledi kwa ngazi aliyopewa sasa.
   
 11. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mbona hii alisha prove kwenye shwala la KATIBA watu wanamuuliza maswali muhimu yeye anajibu wanaotaka katiba mpya ni wanaongea kama mabata

  kwenye kulipa RICHMOND alisema fasta tu walipwe
  juzi hapa bunge kabanwa na LISU nasema lisu ana tafuta umaarufu kuonekana kwenye TV matokeo yaka wakambana afute kauli na spika anakasema ndio ifute

  kwa kifupi ni PROF KILAZA
   
Loading...