Aliyegombea ubunge na zitto atiwa mbaroni, ccm wameanza visasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyegombea ubunge na zitto atiwa mbaroni, ccm wameanza visasi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtutuma, Jun 27, 2011.

 1. m

  mtutuma Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mgombea ubunge wa CUF katika uchaguzi wa 2010 jimbo la KIGOMA KASKAZINI ndugu OMAR MUSA MKWALULO amekamatwa leo mchana na polisi jijini Dar es salaam.

  Bwana mkwalulo alipigiwa simu na ofisa wa takukuru mkoa wa kigoma jana akiwa ifakara.

  Alimjulisha ofisa huyo kuwa yuko ifakara na ndipo ofisa huyo wa TAKUKURU alimjulisha bwana mkwalilo kuwa aende kwa ofisa wa TAKUKURU wilaya ya kilombero ili akasaini fomu maalum ambazo hazikuelezwa ni za namna gani.
  Bwana mkwalulo hakuweza kwenda kwa sababu tayari alikuwa ndani ya basi akirejea dar es salaam.

  Alipofika dar es salaam bwana mkwalilo akampigia yule ofisa wa takukuru mkoa wa kigoma kumjulisha kuwa hakuweza kushuka kwenye gari ili kumuona ofisa wa takukuru wa kilombero, ikabidi ofisa huyo wa kigoma amuombe bwana mkwalilo aende takukuru makao makao makuu dar es salaam na kuwa akifika tu atapewa fomu maalum ambazo lazima azijaze.

  Katika hali ya kushangaza leo majira ya mchana bwana mkwalilo alipoenda takukuru makao makuu dar es salaam aliwekwa chini ya ulinzi mkali na akaelezwa kuwa atasafirishwa hadi kigoma ambako ana mashtaka ya kutoa na kupokea rushwa aliyoyatenda wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana.

  Alipohoji kwa nini takukuru mkoa wa kigoma hawakumuita moja kwa moja hadi kigoma ili kuondoa mawindo waliyokuwa wakimfanyia alijibiwa kuwa hayo ni maagizo kutoka juu.

  Bwana omar mkwalulo ni mfanyabiashara mkubwa sana jijini dar es salaam, mwaka 2010 aliingia kwenye mchakato wa kura za maoni CCM jimbo la kigoma kaskaz akafanyiwa mizengwe hadi akashindwa na ndipo akafanya maamuzi ya kuhamia CUF.

  Alipohamia CUF ujumbe wa CCM ukiongozwa na baadhi ya viongozi wakubwa ulikwenda kigoma ili kusuluhisha na kumshawishi asiende CUF lakini akashindikana.

  Bwana mkwalulo aliingia kwenye kinyang'anyiro hicho cha ubunge na kupambana na zitto na mgombea wa CCM na mwisho wa siku zitto aliibuka kidedea huku kura alizopata mkwalulo ukijumlisha na za mgombea wa CCM zilizidi zile za zitto na hiyo ina maana kuwa iwapo asingehamia CUF na kugawa kura za CCM , mgombea wa CCM angeibuka kidedea.

  Uchaguzi mkuu ulipoisha mwaka jana mkwalulo alifuatwa na maafisa wa TRA mara kadhaa na kumbambikizia kuwa halipi kodi lakini aliwapa vithibitisho vyote kuwa analipa kodi kwa uhakika na TRA wakakosa cha kumkamatia.

  Hivi sasa serikali ya CCM inawatumia takukuru ili kujaribu kulipiza kisasi kwa mkwalulo na haijulikani watafanikiwa kwa kiasi gani.

  Chanzo cha kuaminika cha habari hii kimewasiliana na omar musa mkwalulo akiwa SALENDER BRIDGE chini ya ulinzi mkali na amesema hajui ni makosa yapi ya kuchukua na kutoa rushwa kwani anasema hajawahi kutoa wala kupokea rushwa wakati wa uchaguzi.

  Vyanzo kutoka CUF vinaeleza kuwa mawakili wa chama na naibu katibu mkuu JULIUS MTATIRO wanahaha kuona namna gani wanaweza kumtafutia dhamana mgombea huyu na kisha aende mwenyewe kigoma kukabiliana na mashtaka husika.

  Wanasiasa wanaendelea kushughulikiwa.
   
 2. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Haya-magamba yasipokwanguliwa kwa nguvu na kuteketezwa yatatumaliza, ''sure am telling you''
   
 3. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  'hii ni amri kutoka juu' huyo juu jamani kuna shida gani kwani kila mtu anaye kamatwa bila makosa sababu inatolewa kuwa ni amri kutoka juu jamani huko juu ni wapi? au ni amri kutoka mbinguni.
   
 4. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Amri zinatoka mbinguni? Walahi mwaka huu ukisha salama basi kuna mkono au kiganja cha mtoto.
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Fikra potofu kwamba ni CCM ndiyo wameelekeza. Kulikuwa na ugumu gani kumtengenezea kesi wakati ule ili ikiwezekana hata kura asipige? Na huyu ni yule ambaye Zitto alidai kwamba ametumwa na CCM ili kumvurugia kura kwa sababu ni muislam mwenzake. Hii ni paradox ambayo haiingii akilini.
   
 6. P

  Peter bedson Member

  #6
  Jun 27, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  waheed una mawazo kama yangu nchi inavyoendeshwa mambo yanavyokwenda naona giza
   
 7. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  kweli style waliyotumia kumkamata naona kama hawajamtendea haki, kwani mpaka anapiga simu hakuonesha dalili yoyote ya kujificha. Ila kwa tuhuma hizo zipo, mimi huko kgm kasikazini ni kwetu na hata nilivoenda huko baada ya uchaguzi nilizisikia sana kule kuwa jamaa alijitahidi kusaka kura kwa kasi sana, anayebisha aende kijiji cha mukigo kwao na jamaa ambako ana shule na chuo cha ualimu, kisha panda kalinzi hadi mahembe ukifika pale mahembe waliulize kufuru gani alifanya hapo?utapata full story zake. unajua kuna mambo mtu kwa mzuka wa kusaka uongozi unaweza kujikuta unamwaga pesa bila hata kujificha. Jamani kila siku hapa tunailalamikia TAKUKURU kuwa haifanyi kazi zake sasa vipi tena inapofanya kazi yake tunaanza kuibeza? Jamani bado anatuhumiwa tu mpaka ushahidi utakapo dhihiri ndio atatiwa hatiani, unajua watu kama watu wanaweza sema mengi, hata mimi nilivyosikia wala hata sikuyaamini kwani najua TAKUKURU walikuweko nashangaa walikaa kimya mpaka leo. Nahisi mbwembwe za huyo jamaa watu wa zitto wanazifaham kwani yeye mgomvi wake alikuwa zitto na si mgombea wa ccm
   
Loading...