Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Mwili wa Boniface Pius, mkazi wa Chanika aliyefukiwa na kifusi katika machimbo ya Kigogo Fresh, umezikwa katika kifusi kilichomfukia baada ya juhudi za kuutoa mwili wake kukwama.
Pius alifukiwa na wenzake wanne wakati wakichimba udongo katika machimbo yasiyo rasmi, Alhamisi wiki hii.
Juzi, maiti moja ilitolewa kwenye kifusi hicho na jana aliokolewa mmoja akiwa hai, lakini miguu yake ilikuwa imekatika na mmoja aliyebaki ambaye ni Pius, ilishauriwa azikwe humo kutokana na mvua na hatari ya kifusi hicho kuwaangukia waokoaji.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema aliyekuwa bega kwa bega na waokoaji hao tangu juzi, alisema udongo mwingi ulikuwa ukiporomoka wakati wa shughuli za uokoaji.
“Tumefanya jitihada kumuokoa mwenzetu lakini imeshindikana, tukiendelea huenda tukawapoteza wenzetu. Tumejitahidi tangu Alhamisi, lakini tumefanikiwa kuwapata wachache sasa tumekubaliana na familia tuzike hapa hapa maana hata muda wa uokoaji umeisha,” alisema Mjema.
Watu hao waliangukiwa na kifusi siku ya Alhamisi wakiwa wanne na mmoja wao alikatika mguu, mwingine mwili wake ulipatikana siku hiyo hiyo na mwingine Rashid Fadhili yeye aliokolewa jana kabla ya kazi hiyo kufikia mwisho.
Pia, alisema machimbo hayo yatafungwa na akatoa siku mbili watu wote kuondoa vitu vyao eneo hilo.
Baba mdogo wa marehemu, Pius, Aloyce Mlewa alizungumza kwa niaba ya familia kwamba wamekubaliana na ushauri wa mkuu wa wilaya wa kuzika mwili huo mahali hapo, kutokana na zoezi la uokoaji kuhatarisha usalama wa maisha ya wengine.
“Tumeona jitihada za Serikali katika kutafuta mwili wa mtoto wetu lakini imeshindikana kutokana na hatari iliyopo, watu wengine wanaweza kupoteza maisha. Kama familia tumekubali kufukia mwili huo hapa hapa na tunamtafuta mtumishi wa Mungu tu amuombee,” alisema Mlewa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni alisema zoezi hilo limefungwa na ataimarisha ulinzi ili kuhakikisha watu hawasogei tena eneo hilo kwa kuwa tayari machimbo hayo yamefungwa.
Chanzo: Mwananchi