Aliyefikiria umri wa Rais uwe 40 na zaidi alikuwa ana akili sana

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,072
18,258
Nawaza tuu huyu jamaa angepata urais akiwa na umri wa Makonda tungepata shida sana kumtoa , Sababu inayo nifanya niwaze hivi ni tabia yake ya kuto heshimu katiba na kuamini hurka zake ziongoze nchi.

Pia kuto kua na nia ya kujenga Tanzania yenye msingi bora badala yake anajenga Tanzania yenye kumnufaisha yeye na watu wachache wanaomzunguka walio tayari kulinda maslahi yake kama kina Makonda.

Pia kitendo chake cha kutumia matatizo ya wananchi kujinufaisha kisiasa kwa kuwahadaa kwa kunyanyasa kundi moja ili apendwe na kundi maskini zaidi wakati hakuna alicho wasaidia.

Mbaya zaidi anasema yeye ni Rais kama kweli sisi ndio tulio mchagua hana haja ya kujitambulisha. Yamkini haamini katika demokrasia kwa kitendo chake cha kubariki maovu ya kunyang'anya ushindi wa chama cha CUF kule Zanzibar na kumpongeza Jecha ( Jecha dhambi yako haitafutwa hadi uitubu)

Hata hivyo umri wake umeenda hilo nalo ni jambo LA kumshukuru Mungu.

Wana ccm mtuunge mkono kulaani vitendo vibaya vinavyo dhalilisha utu wa Watanzania kwa kisingizio cha maendeleo vinavyo fanywa na serikali hii katili. Hakuna aliye juu ya katiba, katiba ndio mwongozo wa Watanzania wote. bila kujali umezaliwa wapi.

Mungu wabariki wote walio iandika katiba ya tZ hasa aliye fikiria umri na ukomo wa vipindi viwili.
1480564397836.jpg
1480564407376.jpg
1480564415793.jpg
 
Nawaza tuu huyu jamaa angepata urais akiwa na umri wa Makonda tungepata shida sana kumtoa
Moja ya mambo ambayo nafaham itakuwa shida sana kwa huyu jamaa ni hapo kwenye RED! Anyway, sio hivyo bali kutoka... huyu jamaa kuna kila dalili kwama atagoma kutoka! Ana kila tabia zote za wale wanaoamini wao ndo wanajua kila kitu na ni wao ndio wana uwezo wa kufanikisha jambo fulani! Watu kama hawa siku zote ni wang'ang'anizi wa viti vya enzi! Na hivyo kuna masakala kila kona kwenye hii nchi ni haya masakala ndiyo yataanza kumpa bichwa kwamba aendelee tu huyo huyo hata kama muda umepita!

God Forbid, lakini yale ya Kuurundi nayaona ni kama yanakuja kwenye ardhi ya Bwana Jangala Pilipili Makoroboi huku Bwana Makoroboi akiwa ndio chanzo!!!

Mungu anakuona Bwana Jangala!
 
Makonda anajikaanga na mafuta Yake kama kitimoto siasa ni mchezo wa kijinga Leo anajiona yuko juu kama wigi kesho unaweza kujikuta kanyolewa kipala kwa kipande cha chupa
 
Nawaza tuu huyu jamaa angepata urais akiwa na umri wa Makonda tungepata shida sana kumtoa , Sababu inayo nifanya niwaze hivi ni tabia yake ya kuto heshimu katiba na kuamini hurka zake ziongoze nchi.

Pia kuto kua na nia ya kujenga Tanzania yenye msingi bora badala yake anajenga Tanzania yenye kumnufaisha yeye na watu wachache wanaomzunguka walio tayari kulinda maslahi yake kama kina Makonda.

Pia kitendo chake cha kutumia matatizo ya wananchi kujinufaisha kisiasa kwa kuwahadaa kwa kunyanyasa kundi moja ili apendwe na kundi maskini zaidi wakati hakuna alicho wasaidia.

Mbaya zaidi anasema yeye ni Rais kama kweli sisi ndio tulio mchagua hana haja ya kujitambulisha. Yamkini haamini katika demokrasia kwa kitendo chake cha kubariki maovu ya kunyang'anya ushindi wa chama cha CUF kule Zanzibar na kumpongeza Jecha ( Jecha dhambi yako haitafutwa hadi uitubu)

Hata hivyo umri wake umeenda hilo nalo ni jambo LA kumshukuru Mungu.

Wana ccm mtuunge mkono kulaani vitendo vibaya vinavyo dhalilisha utu wa Watanzania kwa kisingizio cha maendeleo vinavyo fanywa na serikali hii katili. Hakuna aliye juu ya katiba, katiba ndio mwongozo wa Watanzania wote. bila kujali umezaliwa wapi.

Mungu wabariki wote walio iandika katiba ya tZ hasa aliye fikiria umri na ukomo wa vipindi viwili.
View attachment 441565View attachment 441566View attachment 441567
Mhe. Rais amteue makonda kamanda wa operesheni kuzuia uvuvi haramu, ataisaidia sana nchi. Hapo alipo hatumiki vizuri, anaoverqualify!!
 
Huyu Makonda anajiita yeye ndie Mungu wa Dsm..
Aende akatizame MDOMO wa Balozi Seif Idd ulivyo hivi sasa.. Alafu Atafakari..!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom