Aliyefanikiwa kupata namba yake ya utambulisho NIDA kupitia tovuti atoe ushuhuda

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,729
5,923
Sijajua kama ni mimi tu lakini kiukweli kila ninavyojaribu kuingiza taarifa zangu kwenye website ya NIDA ili nipate NIN kama wenyewe wanvyoita nimeshindwa kabisa.

Kama yupo/wapo ambaye amefanikiwa kupata kupitia tovuti aweke hapa namna alivyofanikisha ili tupunguze foleni kule.
 
Mimi ni shahidi nimepata namba ya nida kupitia hiyo tovuti na copy ya Kitambulisho pia.. Nadhan inatakuwa ujaze taarifa kama ulivojaza kwenye form ya nida kama aliyekujazia taarifa zako alikosea baadhi ya taarifa huwezi pata kupitia huu mfumo hadi uende nida ofisini kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijajua kama ni mimi tu lakini kiukweli kila ninavyojaribu kuingiza taarifa zangu kwenye website ya NIDA ili nipate NIN kama wenyewe wanvyoita nimeshindwa kabisa.

Kama yupo/wapo ambaye amefanikiwa kupata kupitia tovuti aweke hapa namna alivyofanikisha ili tupunguze foleni kule.
Ingia hapa 👇

Screenshot_20191226-070633_Chrome.jpg

Kisha chagua Fahamu namba yako (NIN) , itakuleta hapo 👇
Screenshot_20191226-123510_Chrome.jpg

Ingiza taarifa zako sahihi kama ulivyojaza kwenye fomu, kisha gusa Tafuta . Kama namba yako ipo tayari watakuonesha.

Mpaka sasa nimetumia njia hii kupata namba (NIN) za watu wawili niliowasaidia kutafuta.
 
Ninashughuli zangu za steshenari kila siku watu wa nakuja ili niwatoleee Namba zao kupitia tovuti ya nida wanakwambia taarifa si sahii,mpaka sasa nimeshapoteza kama wateja 70,na hakuna hata mmoja niliyewahi kumpatia Namba ,ila kwa wenye Namba kupata online copy kwenyewee haisumbui

Sent using Jamii Forums mobile app
hawakupi taarifa sahihi, niko jirani na steshenari 1 kila siku wanatoa namba kwa wateja (walio wengi)

mie pia nimepata namba online
 
Mimi nilifanikiwa kupata namba na copy yao kwenye website.....!Ni lazima uwe na taarifa sahihi ya ulichokijaza kwenye fomu yao
 
Sijajua kama ni mimi tu lakini kiukweli kila ninavyojaribu kuingiza taarifa zangu kwenye website ya NIDA ili nipate NIN kama wenyewe wanvyoita nimeshindwa kabisa.

Kama yupo/wapo ambaye amefanikiwa kupata kupitia tovuti aweke hapa namna alivyofanikisha ili tupunguze foleni kule.
Kama kwenye website yao wanazingua tuma sms kwa kupiga *152*00#, chagua namba 3 (Ajira na Utambuzi), kisha namba 2 (Nida). Mimi nilipata NIN kwa njia hiyo! Lakini utatakiwa kuwa na ingalau salio la Sh 100 kwenye simu yako
 
Sijajua kama ni mimi tu lakini kiukweli kila ninavyojaribu kuingiza taarifa zangu kwenye website ya NIDA ili nipate NIN kama wenyewe wanvyoita nimeshindwa kabisa.

Kama yupo/wapo ambaye amefanikiwa kupata kupitia tovuti aweke hapa namna alivyofanikisha ili tupunguze foleni kule.
Wanazingua hao wanakwambia taarifa zako haziko sawa ila juzkat kuna mtu aliona jina langu na namba ya NIDA kwenye kituo nilicho jisajili kwakua nilikua mkoani akafanya kunistua...akanitumia nilivyo fungua website yao nilifanya kudownload Online Softcopy ID..

Sasa najiuliza kule Ofisini namba imetoka Kwenye Website walikua wanasema taarifa hazipo ila nilivyo iweka namba nikafanikiwa kupata iyo Online softcopy ID

It seems like kuna Uzembe flan iv
 
Back
Top Bottom