Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,635
- 29,509
Wadau,
Juzi usiku vilitokea vifo vya kusikitisha vya Askari wetu wanane katika eneo la Jaribu Mpakani lililoko Mkoa wa Pwani (M/Mungu akiona inafaa basi awaweke mahali pema peponi, ameen). Hapo awali ilidhaniwa kua waliofanya hivyo Magaidi ambao mara kwa mara inasemekana wako sana maeneo yale kuanzia Vikindu, Mkuranga hadi Kibiti na Ikwiriri.
Lakini taarifa ya Polisi iliyotolewa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Nsato Mssanzya Marijani inasema kua hapa Tanzania hakuna Ugaidi. Walioua askari 8 wilayani Kibiti nao wauawa | East Africa Television Paragraph ya pili kutoka mwisho ya taarifa hiyo inasema "Kuhusu hofu ya ugaidi, Kamishna Marijani amesema tukio hilo siyo la kigaidi bali ni uhalifu wa kawaida, huku akibainisha kuwa Tanzania hakuna ugaidi"
Hii taarifa imenichanganya kidogo maana nafahamu kuna washukiwa au watuhumiwa mbalimbali wa Ugaidi hapa nchini ambao kesi zao zinaendelea. Ref WATUHUMIWA 19 WA UGAIDI WAPANDISHWA KIZIMBANI JIJINI ARUSHA | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today, Watuhumiwa 25 wa ugaidi kortini Moro | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today,
Sasa kama Kamishna Nsato anasema hakuna Ugaidi Tanzania, hawa mahabusu wanatuhumiwa kwa Ugaidi upi tena huo?? Nilitaka kufikiri kua Hawa watuhumiwa ni issue ya Kimahakama wakati anachozungumzia Nsato ni issue ya kipolisi, lakini napata wasiwasi kwani hata hao Watuhumiwa wa Mahakama still issue zao (upelelezi) unaendeshwa na hawa hawa Polisi hivyo kwa namna moja ama ingine wanahusiana. Je hawa watuhumiwa wakidai kwamba wanaonewa sababu kitu wanachotuhumiwa nacho Polisi imekwishathibitisha hakipo haitakua shida??
Nashindwa kuelewa hapa Wanajukwaa, labda hili jambo liko wazi ila kuna kitu mimi pengine ndio sijakielewa. Alieelewa hili swala naomba anieleweshe na mie tafadhali