Aliyedai kuwa mtoto wa Lowassa akamatwa na Polisi. Ni baada ya kuomba radhi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
Godbless E.J. Lema amesema, Yule binti aliyedai ametelekezwa na Mzee Edward Lowassa, amekamatwa baada ya kuomba radhi kwamba jamii imsamehe alikuwa anadanganya. Aliomba radhi kwa kumsingizia Mzee Lowassa.

"Muda huu ninavyoandika tweet hii, wamemchukua dada aliyeomba radhi jana kwa kusema yeye ni mtoto wa Mhe. Edward Lowassa ajulikanae kwa jina la Fatuma nyumbani kwake kigamboni.. Habari nilizonazo kwa sasa wanampeleka ofisini kwa Bashite" .

Habari zaidi, soma=>Hatari! Dada aibukia kwa RC Makonda na kudai ametelekezwa na baba yake ambaye ni Mzee Edward Lowassa

Aliyedai kuwa mtoto wa Lowassa aomba radhi kwa kumdhalilisha; asema tukio limechukuliwa kisiasa na sasa anakosa amani

Binti aliyetelekezwa na Mzee Lowassa asema Fred Lowassa alimtambua na kumhudumia. Lowassa agoma kupima DNA

 
Ndiyo yeye huyo Mkuu, lakini watastuka kumfanyia kibaya huyo dada maana kitu kimeleak hadharani ila atatishwa sana kuhusu “kuropoka ropoka” bila RUKHSA ya Bashite. Wanaweza pia kumpeleka kusikojulikana wakamchapa mijeledi ya uhakika kisha “kuokotwa” akiwa hajitambui. Maskini Tanzania yetu!!!

Eti Bashite ndiye kamanda wa watu wasiojulikana? Twafa na maamuzi ya zero brain, huyo hata unywele wake hautaonekana
 
Kwa hiyo kumbe aliyeratibu ule msamaha chini ya mtutu wa Bunduki ni Lema.!! Yaani anajua kila hatua anayopiga binti wa watu. Wanasiasa mtatuumiza Sana kwa mipango yenu!
Kuna mahali popote mtu ameonekana akiomba msamaha chini ya mtutu wa Bunduki? Mungu aepushie mbali huko mnapotaka kuipeleka nchi! Why didn't You go to Police and explain that someone was confessing at a gun point?
 
Kwa hyo pale kaomba msamaha gani? Mbona anasema yeye alitaka tu apate msaada baada ya kuzungushwa muda mrefu na hakutaka yawe makubwa!?

Kwa nni mlimfuatilia kumtia misukosuko mpaka kumteka akaombe msamaha chini ya upinzi!? Yeye anasema mligeuza suala lake la Kisiasa badala ya lengo lake la kutaka msaada wa babake.

Pale alipoombea msamaha palikuwa wapi na ni kwa nini yule binti hakuwa huru kama alivyotoa taarifa ya awali!?

Ni wapi amekanusha kwamba hahusiani na yule mzee wetu!? Na mbona hamkumtafuta na mamake akanushe!? Muogopeni Mungu!
Kuna mahali popote mtu ameonekana akiomba msamaha chini ya mtutu wa Bunduki? Mungu aepushie mbali huko mnapotaka kuipeleka nchi! Why didn't You go to Police and explain that someone was confessing at a gun point?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom