Aliyechora mipaka ya TANGANYIKA alitubeba. Lakini mpaka sasa miaka 50 ya uhuru tumeshindwa kubebeka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyechora mipaka ya TANGANYIKA alitubeba. Lakini mpaka sasa miaka 50 ya uhuru tumeshindwa kubebeka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jumakidogo, Dec 5, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nikiitizama ramani ya Tanganyika huru huwa najiuliza makusudi ya mbunifu wa mipaka yake.

  Unaweza kuona wazi kuwa ni nchi liyopewa nafasi kwa upendeleo mkubwa. Pengine aliyekuwa akigawa mipaka hiyo alikuwa mbabe kuliko wengine na kuamua kujigawia pande lenye utajiri mwingi.

  Tizama kuanzia Tanga pale juu, jamaa akachora mstari ulionyooka. Alipofika usawa wa ml Kilimanjaro, akakunja kona kidogo na kuchota mlima huo kisha akasonga mbele kuelekea juu. Alipofika Ziwa Victoria, akapasua huku sehemu kubwa zaidi ikiwa ndani. Akaelekea magharibi kwa ajili ya kuchukua usawa wa ziwa Tanganyika. Akapasua katikati mpaka mwisho, pala akakunja kuelekea mashariki kidogo. Alipofika usawa wa ziwa Nyasa, akakata kona kulilenga. Nalo akapasua katikati, alipofika mwisho wa ziwa hilo akasema sasa inatosha. Akakata kuelekea mashariki huku akichora kwa kulipualipua kuelekea mpaka bahari ya Hindi.

  Mgawaji huyu alikuwa mjanja kuliko wengine? au mbabe kuwazidi wenzake? Akaacha Tanganyika yenye kila aina ya utajiri na neema. Leo tunacheza ngoma kushangilia miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika masikini.

  Wakoloni walitubeba lakini mpaka leo tumeshindwa kubebeka.
   
 2. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ilikuwa lazima mlima Kilimanjaro uwepo either Kenya au Tanzania, kwani isingekuwa rahisi kupitisha mpaka juu katikati ya mlima. Kuhusu kuwepo Tanzania, ni matokeo tu ya probability hiyo, si upendeleo!
   
 3. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #3
  Dec 5, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwa nini mpaka haukuchorwa kwa kuja chini, au usingenyooka moja kwa moja kufanya mlima huo ubaki kulia. Tizama pale juu kwenye kona, unaona kabisa kuna ka usanii kalifanyika.
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kumbuka EA UIngereza alikuwa na Kenya na Uganda so Germany ilibidi awe na eneo kubwa.

  Alafu kumbuka borders nyingi huwa ni mito,maziwa so it was easy kwao kutumia izi lakes kama border ili kuondoa kero za mipaka bse izo water bodies hazihamishiki pamoja na landmark kubwa kubwa kama milima.

  KLM MT umekuwa kwetu bse Tayari UK alikuwa na Kenya MT.

  Haya yote ilikuwa enzi za Berlin Conference
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,383
  Likes Received: 22,263
  Trophy Points: 280
  Tungeendelea kuwa TANGANYIKA tungekuwa mbali sana. Wakina David Cameroon wanaharibu baraka na neema za nchi yetu
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwani Tz Meru haikuwepo?
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wanaaribu au nyie ndo mnawajengea hicho kiburi? kitendo cha kuwapa madini na nyie kubakiwa na 3% ndicho kinawacost leo na whata milele
   
 8. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wewe umejuaje kuwa alianzia kuchora Tanga kwenda Mara, na sio Mara kwenda Tanga? Maana yake tuwe fair, mtu mwingine anaweza kuja na argument kwamba tumepunjwa ardhi kwa logic kwamba mpaka ulianzia Mara ukanyooka na baada ya mlima ukabonyezwa chini badala ya kuendelea kunyooka. Otherwise uje na uthibitisho hapa kwamba mpaka ulianzia kuchorwa from Tanga to Mara, na sio Mara to Tanga.

  [​IMG]
   
 9. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #9
  Dec 5, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,136
  Likes Received: 7,389
  Trophy Points: 280
  Sikilizeni nyinyi watu,

  Hiyo michoro imechorwa kwa kichoreo gani?

  Mipaka mingi kama sio mto basi ni ya kufikirika zaidi, hakuna sopecific mstari uliochorwa kwenye physical land.

  Naungana na mtoa mada kua ingewezekana mpaka ukawa pia ni mlima, ila tu kwa upendeleo wa dhahiri, mpaka umekunjwa kuibeba Tanganyika.

  Hata kusini ingewezekana mto Ruvuma ukakaa kaskazini ya Msumbiji, but mgawa mipaka akaubebea na kuuweka Tanganyika.

  Ingewezekana kwa Bahari tuliyonayo tungetosheka kabisa na kuwachia wenzetu maziwa makuu, But kila ziwa kubwa tumelimega,
  Mlima mkubwa ni wetu, labda kwa kuawaonea huruma wenzetu kama ni mashindano tunaweza kuwapa Mlima Meru ndio washindane nao, but Mt. Kilimanjaro hawaukuti wala kuusogelea.

  Ndani ya mipaka kuna madini mbalimbali ambayo ni sisi tu ndio tunayo dunia nzima (competitive advantage), Tena yenye thamani kubwa tu. Inakadiriwa Gram ya dhahabu iliyokwishasafishwa ni kama Tshs alfu 60, Silver labda alfu 40, But Tananite ni kuanzia Laki 2 kwa Gramu moja ambayo haijaongezewa thamani, lakini bado sisi ni maskini.

  Ikumbukwe hata hizo dhahabu na almasi pia tunazo. Ni Nchi ya Aina gani Hii isiyoendelea?

  Kwa mujibu wa Maghufuli samaki walioko ndani ya Bahari Kuu kwenye bahari yetu ni kitega uchumi tosha kwa wakazi wa maeneo ya Pwani, pengine tungeweza kuweka viwanda vya kusindika Samaki na kuilisha sehemu kubwa ya Ulaya.

  "Arable Land" tunayo ya kutosha tu, na ipo idle tu.

  Kilimo Kwanza imekua nayo ni EPA nyingine, Matrekta tunaambiwa ni Mradi wa Shimbo, Watu wanakopa hela nyingi tu kwa kisingizio cha Kilimo kwanza kumbe zinakwenda kwenye issue nyingine.

  Tunabaki kufurahia tu kwa upendeleo tuliopewa kila tukitazama ramani,
   
Loading...