Aliyechomwa moto South Beach afariki! Kigamboni vurugu tupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyechomwa moto South Beach afariki! Kigamboni vurugu tupu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Askari Kanzu, Apr 17, 2011.

 1. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  ALIECHOMWA MOTO SOUTH BEACH AFARIKI DUNIA


  by Othman Michuzi on Sunday, April 17, 2011 at 11:11am

  [​IMG]

  Marehemu Lilah siku za mwisho za uhai wake akiwa hospitali.

  Lilah, yule mwananchi aliyechomwa moto kwa kosa la kuzamia Disco kwenye hoteli ya South Beach Kigamboni jijini Dar es salaam, amefariki dunia.

  Wakizungumza kwa masikitiko ndugu wa marehemu Lillah alifariki dunia jana jioni na mipango ya mazishi inafanywa huko Kigamboni ambapo anatazamiwa kuzikwa leo jioni katika makaburi ya Mji Mwema.

  Marehemu Lilah ambaye alikuwa mfanyabiashara maarufu wa nguo za kuogelea na vitu vya kitamaduni kwa waendao Beach za Kigamboni, alikumbwa na mauti baada ya kukutwa ndani ya Disco akiwa hana tiketi maalumu inayovaliwa mkononi kwa wale wote wanaoingia ndani ya ukumbi huo wa South Beach.


  Spoti na Starehe ni mmoja wa marafiki wa marehemu kwani alikuwa akitembelea na kuuza bidhaa zake katika fukwe Mbalimbali za Kigamboni ikiwemo Chadibwa Beach.
  Marehemu Lillah alikamatwa na walinzi wa fukwe ya South Beach Jumapili iliyopita kwa kudaiwa kuingia bila kulipa kiingilio kwenye Disco linalopigwa mwishoni kwa kila wiki fukweni hapo, Lillah hatimaye alipelekwa kwa meneja wa hoteli hiyo ambaye aliamrisha achomwe moto.

  Akionge kwa taabu na Mwandishi wetu katika Hospitali ya Kigamboni kabla ya kuhamishiwa Muhimbili alikoagia dunia, Marehemu Lillah alisema hata Kupona mpaka pale anamshukuru Mungu kwani hakutegemea kupona kutokana na kipigo na maumivu ya moto ule.Tunaomba haki itendeke ili kukomesha unyama huu, hata kama Marehemu Lilah alikuwa mkosaji au kibaka kama walivyodai hapaswi mtu yeyote kutoa hukumu ambayo Lillah amepata. Huu ni mfululizo wa kujichukulia sheria mikononi ambapo wezi na vibaka wamekuwa wakichomwa moto na wakati mwingine bila hatia yeyote, kwani matukio mengine yakitokea akishakamatwa anatafutwa aliyeibiwa haonekani. Mwanzoni mwa mwaka kijana mmoja alipoteza maisha maeneno ya Mwenge kwa kuitwa mwizi ilihali yeye ndio alikuwa ameibiwa Laptop yake na alipojaribu kuwakimbiza wezi walimgeuzia kibao na hatimaye wananchi walimvamia na akapoteza maisha.

  Marehemu Lillah ameacha mke na watoto.

  Chanzo: SPOTI STAREHE BLOG
   
 2. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #2
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,208
  Likes Received: 3,773
  Trophy Points: 280
  Tunataka kujua aliyemchoma yupo wapi na amechukuliwa hatua gani? Nipo tayari kutoa msaada wa kisheria
   
 3. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Itakuwa vizuri kama utawasiliana na Othman Michuzi kwa sababu anasema alikuwa anamfahamu marehemu. Kontakt za Othman ni hizi hapa:

  E-mail: jamiothman@gmail.com
  Tel:+255 222129550 Mobile
  +255 713775869 Home
   
 4. m

  mashuke Member

  #4
  Apr 17, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hivi wana JF uhai wa mtu unaweza kufananishwa na thamani ya disco?Wahusika lazima watafutwe na haki itendeke.Ndugu wa marehemu fuatilieni haki ipatikane.
   
 5. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2011
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
  Wanaharakati fuatilia hili tafadhali haki itendeke
   
 6. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Vibaka wanachomwa moto kila siku hapo mtaani kwako, mbona hujawasaidia kisheria?
   
 7. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha sana, siku hizi mtu kufa Tanzania inachukuliwa kama kitu cha kawaida sana, aiseeee!
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Mhindi kajitangazia vita na wanakigamboni!
   
 9. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Aisee, kama wewe huwezi kutoa msaada si afadhali ukae kimya. Kwani ni lazima ujibu?
   
 10. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Roho imeniuma sana! Poleni wafiwa.
   
 11. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana, Poleni wafiwa, Sijui kauli ya Pinda ni nini kwa suala kama hili.
   
 12. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya Channel ten Kamanda wa Polisi wa mkoa wa kipolisi wa Temeke DAVID MISIME amenukuliwa akisema kwamba wahusika wote(waliomchoma moto Lilah) wamekamatwa tena leo na Polisi baada ya awali kukamatwa na kuachiwa kwa dhamana,amesema kwamba watu hao watafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumchoma moto Lilah na kusababisha kifo chake
   
 13. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Inaniuma, adhab alyopewa haiendani na kosa alilofanya. Wasaidie ndugu wa marehemu haki itendeke. MUNGU AKUBARIKI SANA YERICKO. Poleni ndg, jamaa na marafiki. Mungu awape moyo wa subira ktk kpndi hiki kigumu. RIP mpendwa wetu.
   
 14. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hatuko kwenye mashindano ya kuchangia hapa so wkt mwngine co lazima uchangie km huna cha kuchangia. Au wewe ndo uliyemchoma nini????
   
 15. LivingBody

  LivingBody Senior Member

  #15
  Apr 17, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 166
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Unajuwa nashindwa kuelewa kwa nini wanadamu tumekosa imani????
  inawezekana kweli mtu anajichukulia sheria mkononi namna hii, mimi kama wangechomwa hao mafisadi ningefurahi,, ila si huyu kuingia tu disco,, ni hasara kiasi gani kasababisha hadi ahukumiwe kifo?
  tuwe na imani.
   
 16. only83

  only83 JF-Expert Member

  #16
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  ..........Natamani kulia,huu unyama kwasababu ya disco tu,there is something behind the event....
   
 17. A

  Ame JF-Expert Member

  #17
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Hawa wenzetu wenye rangi inayofanana na wazungu namacho yanayofanana na sisi sijui kwanini hwapendi kuelewa kuwa attitude zao ni mbaya katika jamii. It once happened to me pale city garden; nilipaki gari langu kwenye parking meneja wa hiyo hotel akiwa katika gari lake akataka kupaki hapo karibu na mimi dereva wake akaona ile nafasi ni ndogo akashuka kuangalia then dereva wangu alikuwa hapo karibu alipomwona kamwambia hapo hawezi kupaki atakwangua gari sasa akamwambia acha mimi nilitoe gari langu ili ninyi mpaki mimi nitafute parking sehemu nyingine. Dereva wangu actually na yeye aliona huyo mzungu mweusi anahaki zaidi ya sisi wakati parking ile ni yakulipiwa na hakuna reserve pale tulipopaki. Wakati madereva wanajadiliana boss akaona yeye hastahili ile hali akamnyang'anya funguo dereva wake akaingia ndani ya gari kabla hajaliweka vizuri akaligonga gari langu. I was just in a distant watching, alipoligonga watu wakaja juu wakaanza kumzonga yule boss akaona zile kelele hazimhusu akaingia ndani ya ofisi yake. Then mimi nikanyanyuka naku mwita dereva wangu nilitaka niite trafic aje pale asilitoe lile gari pale. Akaja officer wa hotel kumbe yule alikuwa akichungulia whats going on akasema kaka sory huyu dereva wetu kaligonga gari lako bahati mbaya so boss anaomba uende ofisini umwambie ni kiasi gani kitatosha utengeneze hilo gari. Kwakweli I felt very bad yaani yule boss mimi nimfuate ofisini kwake wakati yeye ndiyo mkosaji? Then amebadilisha issue na kumsingizia dereva while I was seeing what was happening. Nikamwambia nadhani hii kesi haimhusu yeye (ofisa) ila nadhani traffic maana ni mambo ya magari na parking na si hotel basi naomba asijali naita traffic waje then wahusika wataenda kujitetea mahakamani mimi sina haja ya kuongea na mtu. Lakini likaja wazo la leagal enforcement nikajiona very small for the first time lakini nikaamua kulinda heshima yangu nakumwambia I know what I will do ila kwa sasa siko tayari kumwona huyo boss wako ila mwambie nitatumia njia nyingine kukomesha hii tabia yake na wote wanaofanana na yeye.

  Thats actually why am so much involved in opposition maana raia watanzania kwakweli serikali yao imeshindwa kuwalinda wao na mali zao. Si rahisi kujua ila mpaka ukutane na mambo haya ndo utagundua jinsi raia wanavyo nyanyaswa. Pale nilipokuwa vijana wengi waliona kama vile am somebody with mighty power kumfunza adabu yule msomali maana kazidi kuwanyanyasa; I knew why they thought that way not knowing mimi kama nilivyo was as helpless as them. Na yule msomali pia aliogopa kwasababu ya mawazo yake juu yangu ambayo hayakuwa na ukweli wowote; kumbe maskini I was just as any other Tanzanian barabarani asiye na msaada kama serikali yake haimsaidii. I learnt kwamba Tanzania si sheria inayotawala bali majina something which even rulers dont know siku raia wakichoka wao ndo watakuwa victim wakubwa. Nobody is safe kama hakuna utawala wa sheria.
   
 18. O

  Ogah JF-Expert Member

  #18
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Watu wengine bana...............halafu eti anajiita Gama...........dah!

  Poleni sana wafiwa.......nalaani vitendo hivi viovu vya kutoa uhai wa mtu........
   
 19. z

  zamlock JF-Expert Member

  #19
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  mshenzi nini unacheza na uhai wa mtu tena amefanyiwa unyama na wewe unaleta kejeli za kijinga hapa na mimi nitasaidia mpaka mwisho wake na haki itatendeka na itakuwa ni fundisho kwa watu wanaojichukulia sheria mikononi
   
 20. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #20
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  BT, na bosi wao (mhindi) naye amekamatwa?
   
Loading...