Aliyebeba mimba yangu kaamua kuja kwangu na yule wa zamani naye kaja

king henry

Member
Sep 2, 2018
10
7
Jaman naomba ushauri wenu...

Nilikuwa na girl friend hapokei kwanza but tulikwaruzana Sana kufika kipindi akaamua kuondoka na kunitamkia mengi makali. Nilimpenda sana ila aliamua kwenda..

Niliingia mikononi mwa mtu mwingine alinionesha mapenzi ya dhati but nafsi yangu haikuridhika nae ila ndo aliyebeba mimba yangu na kaamua kuja na mabegi home kwangu na yule wa Zamani nae kaja anaomba msamahaa na bado nampenda na huyu ana kiumbe changu
 
Kama Simu/Computer ni yako kwanini uandike kama unakimbizwa? Hariri Bandiko lako lieleweke Vizuri!
 
Baki na huyo mwenye mtoto wako, huyo aliyekuacha mwambie umeshapata replacement yake. Muda mwingine tujifunze kukubaliana kutokukubaliana, jifunze kumpenda mwenye mtoto kama ulivyompenda huyo mwengine.
 
Kama alikuacha mwanzo kwa maneno na anarudi anakukuta una mtu mwengine tena anamimba yako alaf ukakubali kumsamehe na kurudiana nae then ukamuacha huyo mwenye mimba yako, hakika ipo siku utajutia maana anaweza kukuacha tena kwa dharau zaidi ya mwanzo maana atakuona bwege au msukule wake kwa kumuacha mwenye mtoto wako bila kosa na kumrudia yy. Be a real gentleman, kuwa na msimamo usikubali kupelekeshwa.
 
Huyo wa zamani karudi baada ya kukosa alichodhani amekipata, ni suala la muda tu kabla hajazipata sehemu nyingine achana nae kabisa mkuu
 
Nyie wanaume mistake kutuchekesha saizi lol....sasa wewe unatakaje mkuu uwe nao wote au uishi na uyo alie kubebea mimba
 
Piga chini wa zamani pambana na kijacho,huo muda alikua huko atakua ameshabadilika sio yule tena
 
Aya nimekuelewa baba
Mimi ndiye yule baba mwenye nyumba wako niliekutumia milion moja na nusu unitunzie,ila sasa hivi nakuruhusu unaweza kuzila pia kwa sababu ninyi wanawake mna njia yenu nzuri sana ya kulipa madeni mwanangu!
 
Mwanaume kukosa msimamo ni hatari sana mkuu tulia na huyo mwenye mimba, wewe umeshakanyaga mwiba alaf tena unarudia kukanyaga safari hii tetenasi na kansa vitakuhusu kuwa na msimamo kuepuka
 
Sasa mzee huyo wa zamani wa ninii tenaa Kama mpya nae unampendaa???
 
Back
Top Bottom