Aliyeandika wimbo wa “kajiandae” wa Ommy Dimpoz na Ali kiba ajitokeza! Adai hajalipwa pesa!

mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
2,863
2,000
Zimetufikia za kunyapia nyapia kutoka shirika la wambea SHILAWADU kuihusu hitsong ya wakali wawili wa muziki hapa Bongo Ommy Dimpoz na Alikiba na ngoma yao ya Kajiandae.

Inasemekana kuna mtu afahamikae kama Devi Zinda ambaye anadai kuwa kauandika wimbo huo na hapo awali alilipwa shilingi za kitanzania Laki 5 (500,000) na Ommy Dimpoz kama malipo ya wimbo huo na kuahidiwa kumaliziwa kitita kingine cha shilingi laki 5 ili kutimia million 1 kama ilivyokuwa makubaliano ya malipo ya uandishi wa wimbo huo.

Devi Zinda amepiga story na Soudy Brown leo hii kwenye U-Heard ya XXL na kutoa malalamiko yake yote juu ya Ommy Dimpoz kwasababu anadai kuwa amemtafuta bila mafanikio.
Ubuyu kamili kuhusiana na issue hiyo nimekuwekea hapa chini kwenye video hii, play ili kumsikiliza Devi Zinda akifunguka kwa uchungu kuhusiana na issue hiyo.

 

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
9,398
2,000
Kwa mashairi gani udai mil 1? Ningekuwa mi ndo Ommy Dimpoz ningemdai hiyo laki 5 niliyompa nimuachie elfu 50, kwanza kanyimbo kenyewe kabaya huoni haya kuomba hela?
 

jay311

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
2,883
2,000
Kwa hiyo sasa sisi tufanyeje? au unataka tumchangie hiyo iliyobaki?
 

lukesam

JF-Expert Member
Feb 23, 2015
10,690
2,000
Tanzania ina wanamuziki watatu tu
Ben pol
Barnaba
"Rama d"

Hawa wengine wajanja wajanja tu.. "Kiki" za kijinga zinawapaisha!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom