Aliyeandika waraka wa 'wasomi' wa UDOM kuadabishwa

Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,723
9,189
Serikali ya wanafunzi wa Udom imekasirishwa na kitendo alichokifanya Thobi Richard na muda wote ilikuwa inafikiria namna ya kumuadabisha dogo. Kwa habari iliyonifikia muda huu kutoka ndani ya cabinet ni kwamba dogo anaweza akavuliwa uwaziri na serikali ya wanafunzi watatoa tamko rasmi la kimaandishi.
 
Tamko limeshatolewa kupitia gazeti la Majira la tar 28 November 2010 ikiwa ni pamoja na kukanusha taarifa ya UDOM kulaani wabunge wa Chadema kumsusia JK.
 
Huyo dogo wamtoe haraka sana, amedhalilisha chuo cha DODOMA, na hata uanafunzi wake uchunguzwe ndo vihiyo hao
 
Ili tuamini kweli serikali ya wanafunzi udom haikuhusika na tamko hilo la kulaani wabunge wa chadema inabidi wachukue hatua kali dhidi ya thobias ambaye anadaiwa kua waziri wa sheria wa serikali hiyo. Hii ni kwa sababu watu wengi wameshapoteza imani na UDOM na wanaamini chuo hicho ni chombo cha CCM. Udoso mnatakiwa kujisafisha na uchafu huo..
 
Hizo serikali za wanafunzi ni utumbo tuu..sioni hata manufaa yake kwa wanafunzi.
 
Kwani risala ile iliandaliwa na mtu mmoja na haikuonwa na mtu yeyote wa pili katika uongozi huo wa wakusoma? Asionewe kwa kusakamwa peke yake, Rais wao na top layer wa juu lazima waliijua risala hiyo yenye laana. Kwa hiyo serikali nzima iwajibike. Labda watatoa somo hata kwa viongozi wa kitaifa wa kizazi kipya Tanzania kujua kwamba kuwajibika ni muhali kama hata anayekuwakilisha atabofoa. Mzee Ruksa alitoa mfano na dunia ikamzawadia kwa uadilifu wake, sio kaka yetu L.....sa aliyedai kajiuzuru lakini akaanza kunung'unika huko nje kuashiria hakuwa tayari kujiuzuru.
 
nilifurahi sana kusikia JK akionya wanavyuo kujiingiza kwenye siasa... indirectly that harmed the little boy
 
nilifurahi sana kusikia JK akionya wanavyuo kujiingiza kwenye siasa... indirectly that harmed the little boy


Kwa mujibu wa CCM(JK inclusive), kujiingiza kwenye siasa maana yake ni kuwa mfuasi wa chama kingine tofauti na CCM.
 
jamani mnaumiza vichwa sana kwani hamjui kuwa uongozi wa vyuo vikuu kwa upande wa wanafunzi ni kinyang'anyilo cha vyama vya siasa hapa nchini? hivyo udom wanajulikana ni ccm hatuzuii hilo,hivyo cha muhimu ni kuendelea kupambana nao kwa lolote lile lisilo na maslahi na taifa hili

udom mwajibisheni dogo haraka iwezekanvyo

mapinduziiiiii daimaaaaa
 
Back
Top Bottom