Aliyeaga kwenda misa ya kwanza Kristo Mfalme akutwa akizini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyeaga kwenda misa ya kwanza Kristo Mfalme akutwa akizini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kapwani, May 17, 2010.

 1. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliyeaga kwenda misa ya kwanza Kristo Mfalme akutwa akizini Send to a friend Sunday, 16 May 2010 20:09 0diggsdigg

  Daniel Mjema, Moshi

  MJI wa Moshi na vitongoji vyake, jana ulizizima baada ya mwanamke mmoja aliyekuwa amemuaga mumewe kuwa anakwenda misa ya kwanza kanisa la Kristo Mfalme kufumwa akifanya mapenzi na kijana mmoja mbeba mizigo.

  Tukio hilo ambalo lilivuta hisia za wananchi wengi ambao walifurika kituo kidogo cha polisi cha Kiborlon kushuhudia, lilitokea saa 1.00 asubuhi katika nyumba ya kulala wageni (inahifadhiwa) iliyoko eneo la Majengo mjini hapa.

  Habari zilizowakariri mashuhuda wa tukio hilo na baadhi ya maofisa wa polisi zilidai kuwa kilichomponza mwanamke huyo ni ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) aliotumiwa na hawara yake huyo akimtaka wakutane hiyo jana asubuhi.

  “Jana (juzi) huyo kijana mbeba mizigo hapa Kiborlon alimtumia SMS huyo mke wa mtu, lakini kumbe mume wake aliiona na kujikausha kuwa hajaiona na ndipo leo (jana) alipotoka tu mumewe alianza kumfuatilia,” kilidai chanzo hicho.

  Habari hizo zinadai kuwa baada ya mwanamke huyo kumuaga mumewe anaenda misa ya kwanza na kuondoka, mumewe alimfuatilia ambapo mke alipanda daladala maarufu kama Hiace na mumewe akakodisha Taxi.

  “Mumewe aliendelea kuifuatilia hiyo Hiace kila inaposimama kwenye kituo naye anasimama kwa mbali hadi ilipofika karibu na daraja ambapo kuna kituo yule mwanamke akashuka kuelekea kwenye nyumba ya kulala wageni ,” kimefafanua chanzo hicho.

  Huko ndiko mwanamke huyo mdogo kiumri alipokutana na mbeba mizigo huyo na kwenda moja kwa moja chumbani ambako mumewe baada ya kufika hapo na kuulizia alielekezwa namba ya chumba walichokuwa wameingia.

  Akimkariri mume wa mwanamke huyo, polisi mmoja alilidokeza Mwananchi kuwa baada ya kuona hivyo, mume wa mwanamke huyo alirudi tena hadi eneo la Kiborlon na kuchukua vijana wengine wanne wa miraba minne.

  “Walipofika pale ‘guest’ aliagiza kinywaji aina ya Konyagi na kuanza kunywa lakini walikuwa wanatazama mlango wa chumba na baada ya muda alitoka yule kijana akiwa amefuatana na mke wake,”alifafanua.

  Kutokana na mshituko alioupata baada ya kumuona mumewe, mwanamke huyo alianguka ghafla na kupoteza fahamu kwa muda na alipozinduka walichukuwa pamoja na hawara yake hadi nyumba moja iliyopo Kiborloni.

  Katika nyumba hiyo, mwanamme huyo alipatiwa kipigo cha nguvu kwa kutumia minyororo huku mwanamke akishuhudia na saa 2:40 waliwapeleka wote wawili kituo cha polisi, lakini mwanamme alikuwa ameumizwa vibaya.

  Mwananchi mmoja wa Kiborlon aliyekuwa nje ya kituo cha polisi Kiborlon pamoja na mamia ya wananchi, Charles John maarufu kama King alisema mwanamme aliyefumaniwa alikuwa ameumizwa na alikuwa akitembea kwa shida.

  Mume wa mwanamke huyo alisikika akifoka kwa hasira kituoni hapo kuwa alikuwa anataka kuachana na mwanamke huyo hapohapo kituoni, lakini polisi wakamshauri suala hilo wakalizungumze na wazazi wa pande mbili.

  Baadaye polisi walimwachia mwanamke huyo ambapo alichukuliwa na mumewe na kuingizwa kwenye Taxi na mumewe alisikika akisema anamrejesha kwa wazazi wake huko Kibosho na hana mpango wa kuishi naye tena.

  Mume wa mwanamke huyo ni mfanyabiashara wakati mkewe alikuwa akiuza duka la mabegi alilofunguliwa na mumewe katika eneo hilohilo la Kiborlon ambalo zamani lilikuwa ni maarufu kwa uuzaji wa nguo za mitumba.

  Mnamo saa 4:30 asubuhi, Mwananchi lilishuhudia gari la kituo cha polisi Majengo aina ya Toyota Landcruiser likifika kituo cha Kiborlon na kumchukua mwanamme aliyekuwa amefumaniwa.

  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa , alipoulizwa jana alisema alikuwa hajapata taarifa hizo, lakini ofisa mmoja wa polisi alisema wameamua kuwaachia mwanamke na hawara kwa sababu fumanizi sio kosa la jinai kisheria na kwamba waliwahifadhi pale kwa muda kwa sababu za kiusalama.

  Mmmh tuuite mmomonyoko wa maadili? kutokutoshelezwa kwenye ndoa? au asiye na dhambi aanze kumtupia jiwe? JE ILIKUWA HALALI KUWAPIGA WAFUMANIWA KIASI HICHO? WANA JAMII WENZANGU MNISAIDIE
  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
   
 2. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kipigo huyo jamaa alichopata ni cha aina gani mbona alikuwa anatembea kwa shida? au alivunjwa miguu? huyo mwanaume namsifu kwa moyo wa ujasiri kukaa nje ya gesti huku akijua kabisa mke wake ndani anashugulikiwa na njemba wengine huwa wanaliaga au kuzimia sio wavumilivu.
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  nimekosa hata la kuongea kutokana na kisa hiki ,yaani mwanamama anaaga anaenda church kumbe urongo !!
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mmmh basi mwanamke kakosa sababu zote nyengine mpaka amsingizie Mungu?! agggrrr
   
 5. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo, ni nani wa kuamini siku hizi? Katika vyote kumzimikia mbeba mizigo? Lo ni lazima hiyo ndoa ilikuwa na serious problem kabla ya fumanizi hili!!!! Hii ni kiama!!! Na hizi simu za viganjani zitatusaidia kufahamu mengi kuhusiana na partners wetu??!!!! Tena siku zijazo itakuwa easy maana hata ukitaka kumfahamu mwenye namba ya simu unawahonga tu wale wafanyakazi wa mitandao!!! Wazinzi kwisha kazi!!!
   
 6. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,056
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Huo ni unyanyasaji, ukosefu wa maadili, kuchukua sheria mikononi na ukatili wa kiwango cha juu sana.
  Alikuwa ana ushahidi gani kama mkewe kamegwa na huyo mbeba mizigo?
   
 7. mbarikiwa

  mbarikiwa JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 507
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  No comments! Kwa sababu ingekuwa ni huyo mwanamume mkewe kamfumania na hausi geli angemfanyaje?
  Wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Tukisema kwamba hatuna dhambi tunajidanganya na ukweli haupo ndani yetu. Toa kwanza Boriti iliyo ndani ya jicho lako ndio utatoa kibanzi kilicho ndani ya jicho la mwenzako.
   
 8. bht

  bht JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  na kweli
  pengine walienda kuongea biashara tu je???
   
 9. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Duh! Nimeshindwa kuchangia nikabaki naduwaa tu!
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  May 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,253
  Trophy Points: 280
  Huyo mwanamke ni muongo, maana anasingizia hadi nyumba za ibada!!!
  Huenda nana msururu wa mabwana hapo mjini Moshi
   
 11. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #11
  May 17, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,056
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Si unaona navokagonga leo Edilaisie?

  Mi mpaka wanithibitishie bila kuwepo mashaka kuwa mama wa watu alimegwa na mbeba mizigo mwenzangu. Otherwise huo ni ukatili wa kiwango cha juu kabisa.
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  May 17, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hakukuwa na sababu ya kuwapiga! huyu mwenye mume nadhani anatatizo zaidi mkewe mpaka kuamua kwenda kupata pumziko na mbeba mizigo! Njia nyepesi angeamua kuachana naye mdada wa kichagga aendelee kuwa na mapenzi na huyu kuli. Ukizingatia walikubaliana wala hakubakwa
   
 13. bht

  bht JF-Expert Member

  #13
  May 17, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  hapa tutaongea lugha zinazofanana mapka tuthibitishiwe vinginevyo Pako!!!!
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  May 17, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wadada wakibosho kumbe nao ni balaa!
   
 15. Prisoner

  Prisoner Senior Member

  #15
  May 17, 2010
  Joined: Jan 26, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  akome sina comment
   
 16. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #16
  May 17, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,056
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Si unaona? Watu wanashabikia kumbe uthibitisho hawana? Hapa unatakiwa UTHIBITISHO kama wa TAKUKURU. Siyo wa kimazingira bana.
   
 17. G

  Gozigumu JF-Expert Member

  #17
  May 17, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unasahau wanaoiba sadaka za Kanisa na tende na nyama za misikiti?
   
 18. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #18
  May 17, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ujanja mwingine wakujifanya unajua siyo mzuri,ingekuwa kwako ungesema hivyo? mkuki kwa nguruwe mtamu kwa binadamu mchungu
   
 19. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #19
  May 17, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mimi walioniacha hoi ni hao Polisi. Yaani Polisi wetu wengi ni bure kabisa; wawezaje kumwachia huyo mwanamume aliyemjeruhi mwenzake wakati amesababisha maumivu makali kwa 'ngoni' wake? Hebu jiulize, huyo "mgoni' akifa itakuwaje wakati Polisi wameshamuachia huyo aliyejeruhi mwenzake.

  Yaani Polisi wetu wanongozwa na emotions; ningekuwa mimi ni Polisi pale nisingemuachia huyo mume na mke wake waende maana wana ushahidi gani kuwa yule 'mgoni' alichukua mke wa mtu? YAani mtu anamjeruhi mwenzake vibaya sana halafu anaachiwa! Shame on our Police!
   
 20. j

  jewels Senior Member

  #20
  May 17, 2010
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wallah nimebaki mdomo wazi! mungu atusitiri na hii mitihani, Amina.
   
Loading...