Aliwahi kunicheka kisa nakaa uswazi, leo amekuja kuniomba hifadhi

boyson onlye

JF-Expert Member
Sep 13, 2015
1,108
1,397
Jina la Bwana liinuliwe

Nina rafiki yangu ambaye tulianza wote maisha, tulipanga geto moja, huku uswazi, tulikuwa tunaishi kama ndugu ila tulikutana tu mjini tumetoka mikoa tofauti yeye wa mwanza mm kule Bukoba, maisha yaliendelea, siku kikipatikana tunakula na tukikosa tunelala na njaa wote,

Mungu si Athumani, kwa uwezo wake kila mmoja alipata kazi inayomuhakikishia kipato, hivyo tukawa na uhakika wa kupata mahitaji muhimu, na maisha yakawa ya furaha geto likapendeza na maisha yakasonga mbele,

RAfiki alikuwa anapata malupulupu sana kazini kwake zaidi yangu, hivyo akaniambia anataka kuhama uswazi me nikamtakia kila la Kheri, kweli alihamia makumbusho alikaa miezi Sita, akahamia sinza na baadae mbezi beach, kipindi yuko mbezi beach mwaka mmoja uliopita alishawai kunitamkia maneno ya kejeli kisa bado nakaa uswazi miaka yote hii, kwa nini nisihamie mbezi beach, baadhi ya maneno aliyowai kuniambia ni ( Raha ya Dar uishi mbezi siyo mtu anakupigia simu anakuuliza unakaa wapi unamwambia mwananyamala) na maneno mengine Mengi, kashawai kuniambia hawezi kurudi Uswazi tena maana hana hadhi ya kuishi uswazi, nilimsikiliza tu, kisha nilikaa kimya maana najua kwa kipato amenizid,

Maisha yalisonga sikumuonyesha kama nimekasirika maana wote wanaume, na tunaendela kutafuta, Leo asubuhi bila kutegemea alinitumia text (siyo kawaida yake) akasema anataka kuongea na mm, nilimkubalia akaja uswazi, akanielezea shida yake, kwan sasa hana kazi na hana njia ya kumuingizia kipato hivyo anaomba hifadhi kwangu kwa siku kadhaa, hajataja siku ngapi.
======

UNAWEZA KUTAZAMA MKASA HUU UKISOMWA KTK KIPINDI CHA JAMII LEO

 
Msaidie Mwanaume mwenzio bila kumponda.

Hayo yanatokea katika maisha ila siku moja tu unamwambia awe anakumbuka alipotoka na asidharau watu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom