Alishindwa Kikwete mtoto wa mjini ataweza Magufuli mtoto wa shamba?

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,452
3,150
Huwa nawashangaa sana watu wanaodai eti magufuli anakuja kufanya yale yalimshinda Kikwete. sasa najuliza Kikwete mtoto wa mjini kashindwa atawezaje Magufuli ambaye hata system inavofanya kazi hajui? Ikitokea magufuli akashinda namwona akichukua si chini ya miaka miwili kushangaa shangaa pale ikulu. Mpaka ushamba umtoke itachukua kipindi chote cha mika mitano. Tofauti na lowasa ambaye tayari anajua nini anataka kufanyaakifika pale ikulu na ni nini ataanza nacho! Na pia lowasa tayari ana uzoefu na maisha hayo ya kiikulu ikulu kwa hiyo hatahitaji muda wa kuaclamatize! Eti atapamba na mafisadi. utawezaj kufanya hayo wakati huijui hata system? Kikwete mafisadi walimshinda akajikuta naye anajiunga nao na kuwa fisadi sembuse magufuli ambaye kila kitu atakuwa anaongozwa?

On a serios note: Hivi kuna mtu anaamini magufuli atakuwa bora kuliko kikwete? Magufuli ambaye hakuwa na vision yoyote anasubiri kina kinana na Makamba wamwambie sema hivi na bahati mbaya anajikuta hata akishindwa kuifikisha message km ilivyotarajiwa! Mfano walipomwambia aseme mabadiliko yataleta vita na atolle mfano wa Libya. matokeo yake kajichanga. mara unamsikia akisema atafufua kiwanda cha nyama kilichokufa kumbe kiwanda chenyewe anchozungumzia ni cha ngozi au viatu! madhara ya kukaririshwa! Tumwombe mwenyezi mungu atuepushie mbali na huyu mtu ambaye atakuwa the worst ever president kutokea Tanzania km akichaguliwa! Lowasa ana mapungufu lakini ana nafuu sio sawa na huyu magugfuli. kukurupuka na na kukosa busara ni vitu hatari sana kwa mtu anayetaka nafasi kubwa ya urais. l
 
Hahaha jogoo Wa shamba siku hizi wanawika mjini ,sema ni wale wanaowika mchana wa saa sita , uchuro tuu
Appearance can tell a lot about a person ,jamaa yenu anavyovaa, anavyo ongea , Personality ya urais ni zero kabisa
Mtu anapewa mtoto mdogo ambebe mtoto analia hata bado hamshtuki
Acha born town Lowasa amfundishe Siasa
 
magufuli mshamba sana, kingereza chenyewe shidah, sijui mikataba atakuwa anamsomea mkewee
 
Si ndio hapo chacha. ABC za uraisi magufuli bado sana. Asubiri baada ya miaka 10
 
Dr.slaa mlikuwa mnasema ni mpango wa mungu ila imeshindikana kumtoa ccm, leo mpango wenu wa mungu mnamwita msaliti. Sasa Lowassa mpango wa shetani ndio ataweza kazi iliyoshindikana na mpango wa mungu?
 
Et makamba huyu mtt mdin na kinana mshukiwa wa ujangili ndio washauri wa mgombea mpiga pushapu teh teh
 
Nyerere...kutoka Butiama

Mkapa....kutoka Masasi

Magufuli kutoka Chato

Mwinyi kutoka Mkuranga
 
Jingalao unamfananisha Magufuli na Nyerere? Nyerere na Mwinyi walikuwa washamba?
 
Uhuru Dr Slaavkaamua kuungana na madhwautaini ccm. hata malaika pia waliasi ndioctunaowaita mashetani
 
Back
Top Bottom