Alisema hataki mapenzi tena na mimi lakini bado ananitafua tafuta

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,441
Wakuu salaam,

Kuna msichana nilidate nae mwaka Jana tumeishi kwa miezi kadhaa akapata ujauzito akang'ang'ania autoe, nikamwambia kama kutoatoa kivyako mimi usinishirikishe
baada ya kutoa akakata mawasiliano na ikafikia hatua akaanza chuki na akawa anataka kudate na rafiki yangu mimi nikapotezea.

Mwanzoni mwa mwaka huu kanitafuta kwa simu na kuapologize eti kanimiss nimempa mapenzi ambayo hajawahi kupata nikamsamehe mapenzi yakarudi. Baada ya wiki kadhaa msichana kashika mimba nyingine, mchezo ukawa ule ule kaitoa then kaniacha tena, nami sikujali, mwisho kaniambia hataki tena mapenzi nikamwambia poa nipotezee sasa anakaa kama wiki kimya halafu ananitafuta na kujifanya kunisimulia jinsi mishe zake za kutafuta kazi zinavyokwenda, mara aniambie nimtembelee.

Kiukweli huyu msichana nimetokea tu kumchukia nawaza nifanyaje asinizoe tena manake namwona ka shetani kwa matendo yake.

Nimfanyaje huyu asinizoee tena Jamani?
 
hebu kampime akili kwanza maana huku tz watu hawana utaratibu wa kupima akili

vigezo vya kuoa na kuolewa viongezeke na afya ya akili pia
 
Mmmmh yani na wewe ukaona nijambo lamaaana kushadadia kutoa mimbaa hata wewe ulikuwa nae pamoja kwenye swala LA kutoa coz km ungekuwa na msimamo hizo mimba asingezitoa..... Na km aliforce ungefata sheria ukamshaki kutoa mimba ni uuaji ....alafu unakuja unadai unamchukia
 
Dawa yke ni kumsamehe tu we msamehe tu kila cku msamehe ataacha kukuzoea(na ubwege nazi wko) haaaaaahaaaaaaaa!
 
Kwahyo umeshirik mauaj ya viumbe wawil kwel watu mna roho ngumu dah
 
Labda pengine kosa lipo na wewe, pengine huwa humjali akishika mimba, au una multiple dates mwenzio anahofia utamuacha.
Lakini pia tumia kinga basi. Na use na msimamo kama anasema bye Iwe hivo kweli. Umekuwa mwepesi mno kukubali
 
Pamoja na hayo yote nakulaumu mkuu kwa nini mnashirikiana kuua viumbe visivyo na hatia tena X 2
 
Pamoja na hayo yote nakulaumu mkuu kwa nini mnashirikiana kuua viumbe visivyo na hatia tena X 2

kaka hivi wewe hua una kazi gani mjini? au kinyozi tu muda wote umekaa na simu unachezea unasubiria vichwa tu, yaani wewe kila uzi basi wa kwanza kuujibu, yaani walipo na wewe upo hahahaahahah asee nakuandalia tuzo ntakuomba namba zako tuzo ikikamilika.
 
kaka hivi wewe hua una kazi gani mjini? au kinyozi tu muda wote umekaa na simu unachezea unasubiria vichwa tu, yaani wewe kila uzi basi wa kwanza kuujibu, yaani walipo na wewe upo hahahaahahah asee nakuandalia tuzo ntakuomba namba zako tuzo ikikamilika.
 
Tatizo lako mkuu unatafuta visichana , achana na visichana mara moja na MUOMBE MUNGU akupatie mwanamke wakufanana naye.
 
Back
Top Bottom