Tukumbushane kauli mbalimbali za Wanamichezo

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,681
Heshima mbele wakuu,

Katika thread hii tutapata kukumbushana kauli zilizowahi kutolewa na wanamichezo Duniani kote.

Kila mtu kwa kumbukumbu yake anafulsa ya kubandika Quotes iliyowahi kumfurahisha ama kumchukiza katika medani ya Michezo. Pia ni ruhsa kuelezea kauli hiyo ilitolewa lini ama kwa tukio lipi.

BISMILLAH.
 
''hata Real Madrid wakicheza wachezaji 15 uwanjani basi nina uhakika AC Milan tutaibuka na ushindi ktk mechi hii''.

Kauli hiyo iliporomoshwa na Kocha wa AC Milan Aligo Sacchi ktk mechi ya nusu fainali ya klabu Bingwa Ulaya mwaka 1989.

Katika mechi hiyo Real Madrid walichapwa goli 5-0.
AC Milan siku hiyo waliwakuwa na Nyota kama Galli, Tassotti, Maldini, Costacurta, Baresi, Palombo, Donadoni, Rhiijkard, Van Barsten, Gullit, Ancelotti...

Hiki ndicho kikosi kinachoaminika kuwa bora katika historia ya Soka Ulimwenguni.
 
teh teh teh, Gang Chomba na Ulimakafu vipi tena si mmesema kauli za wanamichezo.

Basi nawapa nyingine ya baba Isaya 'Ukiona fowadi anakuzidi mbio na wewe ni beki usiruhusu atanguliziwe mpira maana anakuzidi mbio atauwahi tu' huyo ni kocha Minziro siku alipoharibu historia tangu akiwa mchezaji hadi kocha alikuwa hajawahi kufungwa tano.
 
Italy ikifungwa ni kwa sababu imecheza vibaya lakini ikishinda ni kwa sababu timu pinzani imecheza vibaya, hii si kweli leo tumeshinda kwa sababu tulikuwa wazuri kuliko Ujerumani, hivyo sisi na Uhispania ndo timu nzuri mbili zilizofika fainali - Mario Balloteli.
 
Back
Top Bottom