Alipanga mauaji ya familia yake kisa kuficha ukweli kuwa hakuwa anasoma chuo

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,043
Tarehe 23, Desemba mwaka 2003, Katika kitongoji cha Sugar Land Texas, yalipo makazi ya watu wenye ukwasi kusini Mashariki mwa Houston, kulitokea tukio la mauaji ya kutisha. Familia ya watu watano ilichapwa risasi na kibaka aliyevamia nyumba yao.

Bart Withtaker na mdogo wake Kevin walikuwa ni zaidi ya ndugu, maana walikuwa karibu sana na marafiki. Bart na baba yake walikuwa wanapenda sana kuendesha baiskeli kwa masafa marefu. Familia yao ilikuwa ni familia ambayo kila mtu angependa kuwa nayo. Pesa kwao haikuwa tatizo na kila mara walienda mapumziko sehemu mbalimbali duniani. Watu waliofahamu familia hii waliona ni familia iliyojaa upendo.

bart.jpg

Tarehe 10, Desemba 2003 ilikuwa ni siku ya kawaida kwa wanafamilia ya Whitaker. Bart Whitaker aliwataarifa wazazi wake na mdogo wake kuwa amehitimu mtihani wake wa mwisho katika chuo Kikuu cha San Houston State. Wazazi wake waliamua kusherehekea kuhitimu kwake mtihani, kwa kumpatia zawadi ya saa ya Rolex yenye thamani ya dola 4000 sawa na milioni 10 kasoro za kitanzania. Pia usiku waliamua kwenda kusheherekea katika mghahawa wa karibu.

Wakiwa mgahawani familia ilipiga picha mbalimbali na wote walionekna wenye furaha. Lakini ndani ya moyo wake, Bart alikuwa anajua kuwa kuna mtu alikuwa kaingia kwenye nyumba yao akiwasubiri warejee nyumbani. Alijua kama kila kitu kitaenda kama alivyopanga, ndani ya dakika 30 zinazofuata baba, mama na mdogo wake watakuwa wamekufa.

"Sina neno la kueleza jinsi gani nilivyokuwa nahisi, ila ni kama nilikuwa ninaongozwa tu, sikuwa ninajielewa." alisema katika mahojiano.

Baada ya kusheherekea, familia ilirudi nyumbani, Bart akijua nini kilikuwa kiiwasubiri ndani ya nyumba, Bart alikimbia kurudi walipoacha gari akidai kwamba kasahau simu yake kwenye gari.

Kevin ndiye alifungua mlango na kuwa wa kwanza kuingia ndani ambapo alitandikwa risasi, Mama yake Bart aliposikia mlio alikimbia haraka ndani naye akakutana na risasi, baba pia kusikia mlio huo naye akaenda kutazama nini kinatokea akatandikwa risasi pia.

Bart anadai aliposikia milio ya risasi, alijua ni kipi kinaendelea, ila kutimizia mpango naye alikimbilia ndani akijifanya anajaribu kumkamata mvamizi. Akamkamata wakaviringishana kidogo kisha naye akapigwa risasi ya mkono ili ionekane naye ni mhanga.

Jirani aliyesikia milio ya risasi alipiga simu ya dharura, na maafisa waliowasili eneo la tukio, walikutana na mwili wa Kevini aliyekuwa na miaka 19 akiwa amefariki tayari risasi moja ikiwa imepenya kifuani. Mama yake Bart alikuwa hai ila alifariki akiwa kwenye helcopter akikimbizwa hospitali. Baba yake Bart ndiye alifanikiwa kupona pamoja na Bart mwenyewe.

Uchunguzi wa tukio unaanza

Baba yake Bart yeye alipigwa risasi mkononi hivyo alipona. Pia Bart aliweza kuigiza vizuri kama mhanga wa tukio zima. Polisi walihisi kuwa itakuwa lilikuwa tukio la wizi lilioenda vibaya, yani kibaka alivamia nyumba kuiba akidhani wenyeji wako mbali ila wakarudi ghafla.

Polisi walichunguza eneo la tukio kuona kama watapata ushahidi wowote utakaowasaidia kumpata muaji. Walikuta draw za makabati zikiwa zimefunguliwa kama vile mwizi alikuwa anatafuta chochote cha kupora. Pia waligundua sehemu ya kuhifadhia bunduki (gun safe) ilikuwa imefunguliwa mapema kabla ya tukio, ndani yake box la risasi lilikuwa linakosa risasi 4 huku bunduki yenye kipenyo cha milimita 9 ikiwa humo kwenye safe lakini kwenye eneo la risasi ikiwa inaonekana kuna risasi nne zimetumika.

Mkuu wa upelelezi Bwana Slot alitumia ushahidi huu kujaribu kumpata muaji lakini aligonga mwamba. Mbwa wa polisi wa kunusa waliweza kunasa harufu flani kwenye eneo la tukio na kuifuata mpaka nje, lakini waliishia tu barabarani. Kwenye eneo la tukio na nyumba nzima askari hawakuweza kupata alama ya vidole nje ya wanafamilia waliokuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo. HIvyo waliamua kuchukua ile bunduki kuipeleka kwenye maabara yao kwa ajili ya uchunguzi. Waliweza kupata alama ya kiganja lakini haikuwa yenye kujitosheleza kuweza kumtambua mtu. Ilikuwa kama kila ushahidi wao ulikuwa hauwezi kuwasaidia.

Kwa sasa Bart alikuwa ameanza kuwa na imani kuwa mpango wake kabambe ulikuwa umefanikia, ila Bwana Slot alikuwa ameanza kuwa na mashaka kwamba tukio hili halikuwa na wizi.

Habari ilipoanza kuandikwa na kutokea kwenye vyombo vya habari, kuna kitu kimoja kilileta mwanga mpya. Mmoja ya chombo cha habari katika kuwataja wahanga kilimtaja Slot kuwa hakuwa kamaliza chuo cha Sam Houston State, na ukweli ni kwamba hakuwa kajiunga na masomo ya aina yoyote.

Askari mmoja pia alikumbuka miaka miwili nyuma aliwahi kuitwa kwenye makazi ya Whitaker ambapo kulikuwa na mashtaka kwamba Bart alikuwa kawatishia maisha wazazi wake. Ila baadae walichukulia kwamba ulikuwa tu ulevi aliongea akiwa kalewa ni kutoelewana.

Bwana Slot alianza kuung ahaya matukio madogo madogo na kugundua inabidi kutazama upya hii kesi.

Bart na baba yake waliporuhusiwa kutoka hospitali, walirudi nyumbani wakaanza kuishi yeye na baba yake. Kwa miezi saba mfululizo Bart alionekana kuwa karibu sana na baba yake akitumia kila muda kuwa naye, akisoma sana Biblia na uchunguzi ulikuwa kamaumegonga mwamba.

Slot anadai alitamani kumwambia baba yake ukweli na muda wote baba yake alikuwa akidai anaweza kumsamehe muaji maana inaonekana alikuwa muoga tu.

Mara usku mmoja, mwanaume anaingia kwenye kituo cha polisi, na kujitambulisha kuwa ni rafiki wa zamani wa Bart na anajulikana kwa jina la Adam Hipp. Adam anadai Bart alikuwa amepanga mpango wa mauaji ambao aliuzuia dakika za mwisho, na yeye Adam alikuwa ndiye aliyepaswa kuwa muuaji. Mpango huo ulikuwa sawa na kilichotokea kwenye mauaji yaliyotokea.

Habari hii, polisi waliifuatilia na kugundua kuwa ni kwei hivyo waliamua kumuonya baba bart juu ya kuwa mwangalifu na mwanae wakimtaka aondoke nyumbani wakati wakitafuta ushahidi wa kumtia hatiani. Mzee aligoma katakata kumwacha mtoto wake.

Mwezi wa saba 2004, Brat alijua kuwa atakamatwa hivyo akaamua kukimbia nchi na kukimbilia Cerralvo Mexico, mji ulioko maili 50 kutoka kwenye mpaka. Kwa kutumia jina la Rudy Rios, aliweza kupata marafiki akaanza kwenda sana kanisani na kufanya urafiki na mpiga gitaa aliyekutana naye hapo, bidada SindyLu Salinas.

Baada ya muda wawili hawa waliingia kwenye mahusiano na Salinas anadai rudy alikuwa mwenye upendo sana. Salinas alimpeleka Rudy (Bart) kwao ili akutane na wa zazi wake na wazazi walitokea kumpenda sana. Baba yake Salinas alimpenda sana Rudy na kumuajiri katika duka lake la kuuza samani.

Nyumbani, upelelezi ulikuwa kama umekosa mwelekeo, mpaka pale jambo kubwa lilipotokea. Mwaka 2005, mwanaume ajulikanaye kama Steven Champgne aliyekuwa aiishi karibu sana na nyumba ya akina Brat, alidai kwamba anataka kuwa mkweli na anataka kwuambia mambo yote anayofahamu kuhusu tukio la Brat. Alikiri kuwa alishiriki katika kutekeleza mauaji hayo, na kutoa mtiririko wa hadithi nzima.

Champagne aliwambia wapelelezi kuwa Brat ndiye alipanga mauaji na kuwapeleka wazazi wake mgahawani kusherekea uongo wa kumaliza kwake mtihani wa chuo. Wakiwa mgahawani, Champagne anadai alikuwa kwenye sehemu ya kuegesha magari akiwatazama kwa mbali. Huku nyuma rafiki yake Brat, Chris Brashear, alikuwa kajificha kwenye gari la Brat nje ya nyumba ya akina Brat. Chapagne alieleza kiunaga ubaga jinsi Chris alivyoingia ndani kwa kutumia funguo, akazima kengele za ulinzi kwa kutuia namba aliyopewa na Brat. Champagne anadai alifuatilia familia ilipokuwa inarudi nyumbani na kuegesha gari karibu na makazi yao akisubiri.

Baada ya kutekeleza mauji, Chris alikimbilia kwenye gari la Champgne na ndiye aliyesaidia kukimbia eneo la tukio. Champagne anadai kuwa Bart aliwambia familia yake wana ukwasi mkubwa na aliwaahidi kuwapa pesa nyingi yani milioni ya madollar.

Kama mnavyojua Marekani siyo kama Bongo, japo jamaa alikuwa kakiri uhusika wake lakini polisi bado hawakuwa na ushahidi wa moja kwa moja unaoweza kutumika kumuunga Bart na muaji. Lakini Champagne aliwapa jambo zaidi, alidai kwamba yeye na Chris walitupa mfuko uliojaa ushahidi kwenye daraja lilipo kwenye ziwa la karibu na hapo

Bila kupoteza muda kikosi za wapiga mbizi kilizama eneo hilo na kuweza kuibuka na fuko lilikuwa limejaa ushahidi wa kutosha ulliokuwa umeanza kuoza. Japokuwa mfuko ulikuwa umekaa chini ya maji kwa miaka miwili, lakini maabara iliweza kusaidia kupatikana kwa DNA ya Chris kwenye mdomo wa chupa uliokutwa kwenye mfuko huo.

Ndani pia ya mfuko huo kulikuwa na simu ya mkononi iliyokuwa imeharibiwa vibaya. Simu hiyo ilitumwa Uingereza kwenye maabara ya kuunganisha data na majibu yaliporudi ilionekana ilikuwa ikimilikiwa na Bart. Sasa polisi walikuwa wamepata ushahidi wa kumuunga Bart na muaji. Hivyo waliomba hati ya kumkamata bart.

Kitu ambacho SLot hakujua ni kuwa mharifu alikuwa tayari ashakimbia yuko zake Mexico. Ila bahati ilikuwa upande wa polisi, Slot alipata simu kutoka kwa kijana ambaye ni konda wa bus aliyekuwa kiishi karibu na makazi ya akina Bart, akamwambia kuwa alimuuzia Bart kitambulisho chake kilichomsaidia kutoroka.

Tarehe 22, mwezi wa 9, 2005, Bart alikamatwa huko Mexico.

Machi 2007, mahakama ilimkuta na hatia bart ya mauaji ya mdogo wake na mama yake. Alihukumiwa kunyongwa kwa kudungwa sindano ya sumu. Aliyepiga risasi yeye alihukumiwa kifungo cha maisha pasipo uwezekano wa msamaha. Champgne yeye alipewa miaka 15.

Baada ya hukumu hiyo bar aliishia kusema, ndiyo mimi niko kama nilivyo.

Baba yake yeye alisimama mahakamani kuomba mahakama imuonee huruma mtoto wake. Baba alidai kwamba ataendelea kumsaidia mtoto wake mpaka siku ya mwisho. Baba anadai mwanaye ni kijana mzuri, awe alipanga au hakupanga, yeye ataendelea kumheshimu kijana wake.

Baba yake Bart ameshikilia msimamo wake juu ya kumsamehe na pia ameandikika kitabu kinaitwa Murder by family ambapo ameweka baya maumivu, machozi na imani aliyopitia kipindi chote toka litokee tukio hilo. Pia aliweka barua walizokuwa wanatumiana yeye na mwanaye akiwa gerezani, mojawapo ikiwa ni barua aliyomwandikia akimaliza kwa kumwambia, Mwanangu nakupena. Yote umesamehewa.

Hukumu ya Bart ilibadilishwa na sasa anatumikia kifungo cha maisha. Lengo la kuua familia yake ilikuwa tamaa ya mali, pia alijua kuwa siri yake itajulikana. Wazazi walikuwa wamemnunulia nyumba eneo la fukwe karibu na chuo wamemwekea kila kitu wamempa na gari ili asome vizuri, kumbe jamaa wala hakuwa mwanafunzi wa chuo.

End End End ... Tukutane Rudy's Farm kula mdudu nice weekend
 
Wazungu wana roho ngumu sana kuuana kwa sababu ya mali na life insurance kawaida

Matukio kama haya kwa wenzetu wazungu ni mengi sana na ndio maana wame advance sana kwenye uchunguzi....mtoto kumua baba au mama kuua mume ni vitu vya kawaida sana kwao...

Ukiangalia channel kama Criminal investigation network au discovery investigation ndio utajua hawa jamaa akili hawana!
 
Napenda Blood relatives, swamp murderers, na fatal encounter. Pia nilipenda sana dissappeared special.

Ila wenzetu aisee wanajua kutengeneza vipindi yani unaweza kuhisi ndiyo tukio linatokea. Kwenye dissappeared special jamaa anavyo narrate napenda sana.

Pia kuna almost a perfect murder. Nimekuwa addicted na mambo ya crime and investigation
 
Tarehe 23, Desemba mwaka 2003, Katika kitongoji cha Sugar Land Texas, yalipo makazi ya watu wenye ukwasi kusini Mashariki mwa Houston, kulitokea tukio la mauaji ya kutisha. Familia ya watu watano ilichapwa risasi na kibaka aliyevamia nyumba yao.

Bart Withtaker na mdogo wake Kevin walikuwa ni zaidi ya ndugu, maana walikuwa karibu sana na marafiki. Bart na baba yake walikuwa wanapenda sana kuendesha baiskeli kwa masafa marefu. Familia yao ilikuwa ni familia ambayo kila mtu angependa kuwa nayo. Pesa kwao haikuwa tatizo na kila mara walienda mapumziko sehemu mbalimbali duniani. Watu waliofahamu familia hii waliona ni familia iliyojaa upendo.

View attachment 1653984

Tarehe 10, Desemba 2003 ilikuwa ni siku ya kawaida kwa wanafamilia ya Whitaker. Bart Whitaker aliwataarifa wazazi wake na mdogo wake kuwa amehitimu mtihani wake wa mwisho katika chuo Kikuu cha San Houston State. Wazazi wake waliamua kusherehekea kuhitimu kwake mtihani, kwa kumpatia zawadi ya saa ya Rolex yenye thamani ya dola 4000 sawa na milioni 10 kasoro za kitanzania. Pia usiku waliamua kwenda kusheherekea katika mghahawa wa karibu.

Wakiwa mgahawani familia ilipiga picha mbalimbali na wote walionekna wenye furaha. Lakini ndani ya moyo wake, Bart alikuwa anajua kuwa kuna mtu alikuwa kaingia kwenye nyumba yao akiwasubiri warejee nyumbani. Alijua kama kila kitu kitaenda kama alivyopanga, ndani ya dakika 30 zinazofuata baba, mama na mdogo wake watakuwa wamekufa.

"Sina neno la kueleza jinsi gani nilivyokuwa nahisi, ila ni kama nilikuwa ninaongozwa tu, sikuwa ninajielewa." alisema katika mahojiano.

Baada ya kusheherekea, familia ilirudi nyumbani, Bart akijua nini kilikuwa kiiwasubiri ndani ya nyumba, Bart alikimbia kurudi walipoacha gari akidai kwamba kasahau simu yake kwenye gari.

Kevin ndiye alifungua mlango na kuwa wa kwanza kuingia ndani ambapo alitandikwa risasi, Mama yake Bart aliposikia mlio alikimbia haraka ndani naye akakutana na risasi, baba pia kusikia mlio huo naye akaenda kutazama nini kinatokea akatandikwa risasi pia.

Bart anadai aliposikia milio ya risasi, alijua ni kipi kinaendelea, ila kutimizia mpango naye alikimbilia ndani akijifanya anajaribu kumkamata mvamizi. Akamkamata wakaviringishana kidogo kisha naye akapigwa risasi ya mkono ili ionekane naye ni mhanga.

Jirani aliyesikia milio ya risasi alipiga simu ya dharura, na maafisa waliowasili eneo la tukio, walikutana na mwili wa Kevini aliyekuwa na miaka 19 akiwa amefariki tayari risasi moja ikiwa imepenya kifuani. Mama yake Bart alikuwa hai ila alifariki akiwa kwenye helcopter akikimbizwa hospitali. Baba yake Bart ndiye alifanikiwa kupona pamoja na Bart mwenyewe.

Uchunguzi wa tukio unaanza

Baba yake Bart yeye alipigwa risasi mkononi hivyo alipona. Pia Bart aliweza kuigiza vizuri kama mhanga wa tukio zima. Polisi walihisi kuwa itakuwa lilikuwa tukio la wizi lilioenda vibaya, yani kibaka alivamia nyumba kuiba akidhani wenyeji wako mbali ila wakarudi ghafla.

Polisi walichunguza eneo la tukio kuona kama watapata ushahidi wowote utakaowasaidia kumpata muaji. Walikuta draw za makabati zikiwa zimefunguliwa kama vile mwizi alikuwa anatafuta chochote cha kupora. Pia waligundua sehemu ya kuhifadhia bunduki (gun safe) ilikuwa imefunguliwa mapema kabla ya tukio, ndani yake box la risasi lilikuwa linakosa risasi 4 huku bunduki yenye kipenyo cha milimita 9 ikiwa humo kwenye safe lakini kwenye eneo la risasi ikiwa inaonekana kuna risasi nne zimetumika.

Mkuu wa upelelezi Bwana Slot alitumia ushahidi huu kujaribu kumpata muaji lakini aligonga mwamba. Mbwa wa polisi wa kunusa waliweza kunasa harufu flani kwenye eneo la tukio na kuifuata mpaka nje, lakini waliishia tu barabarani. Kwenye eneo la tukio na nyumba nzima askari hawakuweza kupata alama ya vidole nje ya wanafamilia waliokuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo. HIvyo waliamua kuchukua ile bunduki kuipeleka kwenye maabara yao kwa ajili ya uchunguzi. Waliweza kupata alama ya kiganja lakini haikuwa yenye kujitosheleza kuweza kumtambua mtu. Ilikuwa kama kila ushahidi wao ulikuwa hauwezi kuwasaidia.

Kwa sasa Bart alikuwa ameanza kuwa na imani kuwa mpango wake kabambe ulikuwa umefanikia, ila Bwana Slot alikuwa ameanza kuwa na mashaka kwamba tukio hili halikuwa na wizi.

Habari ilipoanza kuandikwa na kutokea kwenye vyombo vya habari, kuna kitu kimoja kilileta mwanga mpya. Mmoja ya chombo cha habari katika kuwataja wahanga kilimtaja Slot kuwa hakuwa kamaliza chuo cha Sam Houston State, na ukweli ni kwamba hakuwa kajiunga na masomo ya aina yoyote.

Askari mmoja pia alikumbuka miaka miwili nyuma aliwahi kuitwa kwenye makazi ya Whitaker ambapo kulikuwa na mashtaka kwamba Bart alikuwa kawatishia maisha wazazi wake. Ila baadae walichukulia kwamba ulikuwa tu ulevi aliongea akiwa kalewa ni kutoelewana.

Bwana Slot alianza kuung ahaya matukio madogo madogo na kugundua inabidi kutazama upya hii kesi.

Bart na baba yake waliporuhusiwa kutoka hospitali, walirudi nyumbani wakaanza kuishi yeye na baba yake. Kwa miezi saba mfululizo Bart alionekana kuwa karibu sana na baba yake akitumia kila muda kuwa naye, akisoma sana Biblia na uchunguzi ulikuwa kamaumegonga mwamba.

Slot anadai alitamani kumwambia baba yake ukweli na muda wote baba yake alikuwa akidai anaweza kumsamehe muaji maana inaonekana alikuwa muoga tu.

Mara usku mmoja, mwanaume anaingia kwenye kituo cha polisi, na kujitambulisha kuwa ni rafiki wa zamani wa Bart na anajulikana kwa jina la Adam Hipp. Adam anadai Bart alikuwa amepanga mpango wa mauaji ambao aliuzuia dakika za mwisho, na yeye Adam alikuwa ndiye aliyepaswa kuwa muuaji. Mpango huo ulikuwa sawa na kilichotokea kwenye mauaji yaliyotokea.

Habari hii, polisi waliifuatilia na kugundua kuwa ni kwei hivyo waliamua kumuonya baba bart juu ya kuwa mwangalifu na mwanae wakimtaka aondoke nyumbani wakati wakitafuta ushahidi wa kumtia hatiani. Mzee aligoma katakata kumwacha mtoto wake.

Mwezi wa saba 2004, Brat alijua kuwa atakamatwa hivyo akaamua kukimbia nchi na kukimbilia Cerralvo Mexico, mji ulioko maili 50 kutoka kwenye mpaka. Kwa kutumia jina la Rudy Rios, aliweza kupata marafiki akaanza kwenda sana kanisani na kufanya urafiki na mpiga gitaa aliyekutana naye hapo, bidada SindyLu Salinas.

Baada ya muda wawili hawa waliingia kwenye mahusiano na Salinas anadai rudy alikuwa mwenye upendo sana. Salinas alimpeleka Rudy (Bart) kwao ili akutane na wa zazi wake na wazazi walitokea kumpenda sana. Baba yake Salinas alimpenda sana Rudy na kumuajiri katika duka lake la kuuza samani.

Nyumbani, upelelezi ulikuwa kama umekosa mwelekeo, mpaka pale jambo kubwa lilipotokea. Mwaka 2005, mwanaume ajulikanaye kama Steven Champgne aliyekuwa aiishi karibu sana na nyumba ya akina Brat, alidai kwamba anataka kuwa mkweli na anataka kwuambia mambo yote anayofahamu kuhusu tukio la Brat. Alikiri kuwa alishiriki katika kutekeleza mauaji hayo, na kutoa mtiririko wa hadithi nzima.

Champagne aliwambia wapelelezi kuwa Brat ndiye alipanga mauaji na kuwapeleka wazazi wake mgahawani kusherekea uongo wa kumaliza kwake mtihani wa chuo. Wakiwa mgahawani, Champagne anadai alikuwa kwenye sehemu ya kuegesha magari akiwatazama kwa mbali. Huku nyuma rafiki yake Brat, Chris Brashear, alikuwa kajificha kwenye gari la Brat nje ya nyumba ya akina Brat. Chapagne alieleza kiunaga ubaga jinsi Chris alivyoingia ndani kwa kutumia funguo, akazima kengele za ulinzi kwa kutuia namba aliyopewa na Brat. Champagne anadai alifuatilia familia ilipokuwa inarudi nyumbani na kuegesha gari karibu na makazi yao akisubiri.

Baada ya kutekeleza mauji, Chris alikimbilia kwenye gari la Champgne na ndiye aliyesaidia kukimbia eneo la tukio. Champagne anadai kuwa Bart aliwambia familia yake wana ukwasi mkubwa na aliwaahidi kuwapa pesa nyingi yani milioni ya madollar.

Kama mnavyojua Marekani siyo kama Bongo, japo jamaa alikuwa kakiri uhusika wake lakini polisi bado hawakuwa na ushahidi wa moja kwa moja unaoweza kutumika kumuunga Bart na muaji. Lakini Champagne aliwapa jambo zaidi, alidai kwamba yeye na Chris walitupa mfuko uliojaa ushahidi kwenye daraja lilipo kwenye ziwa la karibu na hapo

Bila kupoteza muda kikosi za wapiga mbizi kilizama eneo hilo na kuweza kuibuka na fuko lilikuwa limejaa ushahidi wa kutosha ulliokuwa umeanza kuoza. Japokuwa mfuko ulikuwa umekaa chini ya maji kwa miaka miwili, lakini maabara iliweza kusaidia kupatikana kwa DNA ya Chris kwenye mdomo wa chupa uliokutwa kwenye mfuko huo.

Ndani pia ya mfuko huo kulikuwa na simu ya mkononi iliyokuwa imeharibiwa vibaya. Simu hiyo ilitumwa Uingereza kwenye maabara ya kuunganisha data na majibu yaliporudi ilionekana ilikuwa ikimilikiwa na Bart. Sasa polisi walikuwa wamepata ushahidi wa kumuunga Bart na muaji. Hivyo waliomba hati ya kumkamata bart.

Kitu ambacho SLot hakujua ni kuwa mharifu alikuwa tayari ashakimbia yuko zake Mexico. Ila bahati ilikuwa upande wa polisi, Slot alipata simu kutoka kwa kijana ambaye ni konda wa bus aliyekuwa kiishi karibu na makazi ya akina Bart, akamwambia kuwa alimuuzia Bart kitambulisho chake kilichomsaidia kutoroka.

Tarehe 22, mwezi wa 9, 2005, Bart alikamatwa huko Mexico.

Machi 2007, mahakama ilimkuta na hatia bart ya mauaji ya mdogo wake na mama yake. Alihukumiwa kunyongwa kwa kudungwa sindano ya sumu. Aliyepiga risasi yeye alihukumiwa kifungo cha maisha pasipo uwezekano wa msamaha. Champgne yeye alipewa miaka 15.

Baada ya hukumu hiyo bar aliishia kusema, ndiyo mimi niko kama nilivyo.

Baba yake yeye alisimama mahakamani kuomba mahakama imuonee huruma mtoto wake. Baba alidai kwamba ataendelea kumsaidia mtoto wake mpaka siku ya mwisho. Baba anadai mwanaye ni kijana mzuri, awe alipanga au hakupanga, yeye ataendelea kumheshimu kijana wake.

Baba yake Bart ameshikilia msimamo wake juu ya kumsamehe na pia ameandikika kitabu kinaitwa Murder by family ambapo ameweka baya maumivu, machozi na imani aliyopitia kipindi chote toka litokee tukio hilo. Pia aliweka barua walizokuwa wanatumiana yeye na mwanaye akiwa gerezani, mojawapo ikiwa ni barua aliyomwandikia akimaliza kwa kumwambia, Mwanangu nakupena. Yote umesamehewa.

Hukumu ya Bart ilibadilishwa na sasa anatumikia kifungo cha maisha. Lengo la kuua familia yake ilikuwa tamaa ya mali, pia alijua kuwa siri yake itajulikana. Wazazi walikuwa wamemnunulia nyumba eneo la fukwe karibu na chuo wamemwekea kila kitu wamempa na gari ili asome vizuri, kumbe jamaa wala hakuwa mwanafunzi wa chuo.

End End End ... Tukutane Rudy's Farm kula mdudu nice weekend
Niliiona hii episode kwenye Discovery ID ( IDX)
 
Back
Top Bottom