alipanga kulipasua tumbo ili kuiba mtoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

alipanga kulipasua tumbo ili kuiba mtoto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Mar 14, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwanamke mmoja wa nchini Marekani mwenye umri wa miaka 18 aliyekuwa akitamani kuwa na mtoto, ametiwa mbaroni baada ya kumshambulia mwanamke mjamzito na kujaribu kulipasua tumbo lake ili kukiiba kichanga kilichokuwa tumboni mwake.
  Mwanamke huyo mkazi wa Arizona nchini Marekani, Kassandra Toruga, 18, alikiri mbele ya polisi kuwa alikuwa na mpango wa kumuua mwanamke ambaye alikuwa ni rafiki yake mwenye mimba ya miezi tisa.

  Kassandra aliwaambia polisi kuwa alipanga kulipasua tumbo la rafiki yake na kisha kumuiba mtoto mchanga aliyekuwa tumboni mwake.

  Kassandra alipanga kuwaambia watu kuwa mtoto huyo ni wake na aliweka kwenye ukurasa wake wa MySpace picha ya ultrasound inayomuonyesha mtoto tumboni akidai ni picha ya mimba yake.

  Kassandra alienda kwa rafiki yake ambaye jina lake limewekwa kapuni akiwa na visu viwili vikubwa vya buchani, mkasi,nepi na nguo za mtoto, taarifa ya polisi ilisema.

  Wakati akimshambulia mwanamke huyo kabla ya kutimiza azma yake, Kassandra alilichoma moto kabati la nguo na kupelekea zimamoto kuwasili kwenye nyumba hiyo na mpango mzima wa Kassandra kuharibika.

  Kassandra alitiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka ya kujaribu kuua, wizi na kuharibu mali kwa moto.

  Rafiki yake amejifungua salama mtoto wake siku chache baada ya shambulizi hilo lakini amekuwa akijificha kwa kuhofia huenda Kassandra akamtafuta na kumteka mtoto wake.

  Mwaka juzi mwanamke mwingine wa nchini Marekani alimuua mwanamke mwenye mimba ya miezi minane na kulipasua tumbo lake na kumuiba mtoto wake mchanga.

  Maiti ya mwanamke huyo ilikutwa ndani ya kabati la nguo kwenye nyumba yake siku chache baadae wakati mtoto aliyenyofolewa toka tumboni mwa mama yake alipatikana wiki mbili baadae akiwa mwenye afya njema.
   
Loading...