Aliomba afikie nyumbani kwangu nikakataa. Je, nilikosea?

kindikinyer leborosier

JF-Expert Member
Jan 6, 2018
430
780
Habari wanajamii?

Poleni na majukumu ya week nzima!

Niende moja kwa moja kwenye uzi husika, mwaka 2013 nilianza mahusiano na binti mmoja ambae familia yao ilikua karibu sana na familia yetu.

Tulidumu kwenye mahusiano kwa muda kidogo mpaka 2017 ambapo tuliamua kuachana, sababu kubwa ikiwa yeye alikua akiwa na mahusiano mengine chuoni kwao, kwa siri. nilivyokuja kusikia nilichukua maamuzi hayo japo kweli nilikua nikimpenda sana.

Kwenye mihangaiko ya maisha nilikuja kuishi Mwanza, siku moja aliniambia anarudi kwao Musoma anataka kunipitia, nilimkaribisha, japo sikumleta kwangu, tuliishia kwa hotel.

Alikua na mambo mengi sana ya pride mara hiki mara kile, mara ampigie simu mwanaume alienae hivyo, nilikausha tuu, mwisho nilimwaga kama saa 2 usiku!

Juzi aliniandikia txt anaolewa, sikujali nikamjibu nitampa mchango wangu, nikatulia, jana amenitafuta ananiomba anatoka Dsm kwa mchumba wake, anataka afikie kwangu napoishi afanye manunuzi kabla ya kurudi Musoma.

Mwanzo nilikubali ila baadae niliwaza nikaona si busara, kwa sababu hizi:

1. Mahusiano yetu yalikua yakifahamika mpaka nyumbani kwetu.

2. Tabia zake za awali za majivuno na pride

Alikuja kugundua namwepuka kwani nilimwambia na ziara ya kikazi nje ya mkoa.

Alilalamika sana, na kusema kila mtu anajua yeye anaenda kuolewa hata kwetu, hivyo mimi kumkatalia nilifanya vibaya kwani hata wadogo zangu wanaweza kupata hifadhi siku moja kutoka kwake.

Asanteni wadau, Je nilikosea kumkatalia.

Natanguliza samahani endapo uandishi wangu haujakaa sawa!
 
Alipopita kwako mara ya mwisho ulimla?

Kama ameamua kuolewa ni bora tu uachane naye moja kwa moja kwa sababu mkiendelea na hizo danadana za kutembeleana utaendelea tu kumla hata baada ya kuolewa. Na hakuna dhambi mbaya hapa duniani kama kuzini na mke wa mtu.

Ulifanya vyema na Mungu Akusaidie usibadili msimamo wako.
 
Alipopita kwako mara ya mwisho ulimla?

Kama ameamua kuolewa ni bora tu uachane naye moja kwa moja kwa sababu mkiendelea na hizo danadana za kutembeleana utaendelea tu kumla hata baada ya kuolewa. Na hakuna dhambi mbaya hapa duniani kama kuzini na mke wa mtu.

Ulifanya vyema na Mungu Akusaidie usibadili msimamo wako.
Hapana kuna tabia ziliniudhi alivyokuja, hivyo sikufanya chochote, na ndipo nilipoamua kupoteza kumbukumbu zote kutoka kwake.

Asante! kuna kitu nimekipata!
 
Uko sahihi achana naye.
mkuu achana naye kimahusiano lakini upendo ubaki pale pale.. sijamaanisha mapenzi la hasha!
namaanisha muwe tu na upendo wa kawaida maana dunia hii haijulikani..
usimpotezee kiivo ila akitafuta jaribu tu ku_respond postively...
your economic successes may depend upon each other..
me nakushauri .. hapa duniani usimpotezee binadamu mwenzako.. ni bora umwambie tu ukweli kwamba haupo Naye kimahusiano..
kama ana akili atajiongeza..
 
Back
Top Bottom