Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Kwa muono wangu, Dk Ali Mohammed Shein hakustahiki kuwekwa katika safu ya nyuma iliyopangwa kuwekwa mabalozi wa nchi za nje, wakati alipokwenda Comoro kuhudhuria kuapishwa kwa Rais mpya wa visiwa hivyo.
Dk Shein hata kama asingelikuwa Rais wa Zanzibar, hadhi yake ya kumwakilisha Rais, Dk John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatosha kabisa kumuweka, kiitifaki, katika safu ya mbele.
Kama siko sahihi, nani basi wa kulaumiwa? Ni Mkuu wa itifaki ya msafara wa Dk Shein na mshauri wake wa mambo ya Nje na Diplomasia, Balozi Mohammed Ramia au wenyeji?
Nielwesheni lakini si kwa jazba!