Alininyanyasa sana nilipofukuzwa kazi, MUNGU ameniona, sasa yamegeuka

magombe junior

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
1,877
2,000
ao wazee walikua wap wakati mwanamke anakunyanyasa!?..

Anyways moyo niwako ila ujue ukirudiana nae na mambo yakaenda kombo tena huna chako
 
StudentTeacher

JF-Expert Member
Jan 30, 2019
1,607
2,000
Siku moja nisiyopenda kuikumbuka nilitwa ofisini kwa bosi wangu na kukabidhiwa barua ya kufukuzwa kazi
Hiyo ilikua ni baada ya uchunguzi wa miezi kdhaa wa kosa nililokua nimelifanya bahati mbaya. Miezi mitatu nyuma nilimuingizia pesa mteja kimakosa kwenye akaunti yake kiasi cha million mia tatu na hamsini ambazo alitakiwa kuwekewa Mteja mwingine halali kupata pesa hizo.

Kama humu ndani Kuna banker ataelewa nachokisema, kwamba makosa kama haya benki ni kawaida sana. Ukigundua kosa kama hili unawahi una reverse hiyo entry una m-credit anaetakiwa shida ni kama uliemwekea kimakosa akawahi kuzichukua ndipo yanakukuta yaliyonikuta mimi.

Baada ya kufukuzwa kazi mke wangu alibadilika kabisa
Nilishuhudia yafuatayo:-

(1) Alitamka mimi ni mjinga ndio maana nimefukuzwa kazi.

(2) Chake kikawa chake tu.

(3) Akawa anawaambia wazi watoto kuwa kitu fulani kimenunuliwa na yeye na sio mimi.

(4) Muda wa kurudi home ukabadilika sasa anarudi usiku mwingi, nampa kipigo cha nguvu anazira na kukimbilia kwao, kwenye usuluhishi anawaambia wasuluhishi kwamba mimi namuonea wivu kwa kuwa ana kazi mimi sina.

(5) Niliuza Gari zangu mbili ili nipate mtaji wa kufanya biashara hivyo nikawa sina Gari nilijua maadam wife ana Gari tutatumia wote maana hata yeye wakati hana Gari alikua akitumia magari yangu.

Kinyume na matarajio hakutaka kabisa niguse Gari lake mimi nikawa mtu wa miguu.Majirani wakawa wanashangaa mfumo wetu wa maisha.

(6) Life yetu ya bedroom ikawa imekufa no intimacy no love making nothing. Alianza kidogo kidogo leo mara aseme anaumwa, kesho kachoka, hadi mwezi unaisha. Nikaamua isiwe tabu nikaacha kuulizia tena, nae akawa amepotezea moja kwa moja.

Hata wazazi wangu aliwa mistreat sana wakawa hawaji tena kwangu, mama yangu akawa ananitumia vitu kwa njia basi kutoka nyumbani kama mchele, maharage, unga na kadhalika ili na mm nionekane nachangia.Wakuu siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Kila nilichojaribu kukifanya ili nijinasue kinakwama, nakuta mtaji wote unakata naanza moja.Ilikatika miaka minne nikiwa kwenye hali hii maana nilipata matatizo 2010. Mwaka Jana kuna Dada mmoja tulisoma wote primary school akaamua kunisaidia, huyu dada tulikutana Posta accidentally tukapeana contact
mimi nilishamsahau ila yeye alinikumbuka.

Baadae akaniunganisha na mumewe ambae ni HR manager kwenye shirika fulani, nikamwelezea ukweli wote na akaniingiza kaziniWife sikumwambia kuwa nimepata kazi akaanza kuona nakuja na mahitaji ndani, nikawa naondoka zangu alfajiri narudi usiku mwingi. Nikaita mafundi wakabomoa ukuta wote wa fensi uliokua umeoza waliiba sana cement wakati wa ujenzi ukajengwa upya, vitu vyote vilivyochoka ndani nikabadilisha. Wife alishangaa sana ila akashindwa kuniuliza maana hadi hapo tulikua hatuongeleshani zaidi ya salam za asubuhi na jioni tu basi.

Wana jf siwezi kuwaficha sehemu niliyopata naingiza hela Mara kumi ya ile kazi yangu ya benki, hii sikutokana na mshahara bali njia mbali mbali katikati ya mwezi kitengo chetu tupo wanne,hali ikiwa nzuri huwa tunagawana hadi laki mbili kila siku, kama hali ni mbaya tunagawana laki moja kwa siku hii ni mbali na ile tunayogawana mwisho wa mwezi kama million 3 each person mshahara ni mdogo tu ni laki saba tu kwa mwezi.Maana mshikaji alisema anaweza kuniingiza kazini ila kama mfanyakazi wa kawaida kwa kuwa benki nilifukuzwa hakukua na reference wala background check so nikaamua kufuta kwenye CV kuwa nilifanya bank.

Nimeanza mchakato wa talaka kupitia mwanasheria mmoja rafiki yangu, mwezi January mwaka huu amemwandikia barua ya kumtaarifu uamuzi huo na copy Ustawi wa jamii pia, baadae tutafungua shauri la talaka.Kinyume na matarajio yangu wife kwa kuwa alishañichoka na hakuna kinachoendelea kati yetu nilijua angekubali tu. Cha ajabu hivi sasa kupitia wazee wake wameniita kikao zaidi ya Mara 6 sasa ili tusuluhishe tofauti zetuKawa mpole sana, alidhan nitaendelea kuteseka milele

Wakuu sasa sipo nyumbani kwa hasira ya mambo aliyonitendea hivi sasa sipo nyumbani nimepanga upande wa nyumba nimeanza ujenzi ili nihamie. Kila siku lazima nipite kwa watoto niwaone ndo niondoke. Nimesimama njia panda, mm binafsi nilishaamua simtaki tena huyu mwanamke ila wazee na viongozi wa dini tunakoabudu wanasema turudiane juzi mke wangu alinipigia magoti tukiwa kikaoni kwamba nimsamehe, nifute kusudio la kuomba talaka mahakamani. Wazazi wangu hawataki kusikia kabisa neno msamahakwa matendo aliyotufanyia.

NB: Nimetaja kipato ili kuwapa mwanga na uelewa wa tatizo isichukuliwe vinginevyo

Nimesikia amepata matatizo kazini ila sina uhakika na taarifa hizo

Naomba ushauri wenu
Msamehe na ukiweza sahau yote aliyokutendea lakini usiendelee kuishi nae. Hakuna ndoa hapo. Ndoa ni "mahaba" ,mahaba yakitoweka mnakuwa kama mtu na dada ake tu.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
JABALI LA KARNE

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,198
2,000
Hakuna dhambi kubwa kwa mwanaume kama;
1.Kumsomesha mwanamke
2.Kumrudia mwanamke aliyekunyanyasa
3.Kuoa mwanamke aliyezaa na mtu halafu mtu huyo yupo

Songs mbele achana naye huyo.

Note my words
Lover boys ndo wanateseka na haya mambo uliyoyataja. Ukiwa mwanaume mwenye tabia za mwanaume na una uwezo kifedha hayo mambo hayana maana.

Ss nikimpa mwanamke m3 ya ada nikamtumia nipendavyo nikaridhika nikamwacha nimepoteza nn?

Unanyanyaswaje na mwanamke walivyo wengi na wana njaa ya ndoa hata mke wa tatu au kuwekwa nyumba ndogo wanakubali?

Kama mtu wake kamshindwa mm nikimweka ndani nikampa huduma zote na wanae nawasomesha shida ipo wapi ikiwa napewa nitakacho na nikimchoka talaka zipo?
 
Renegade

JF-Expert Member
Mar 18, 2009
6,094
2,000
Mkuu Mimi nakushauri usimwache Mkeo! Maadamu amekuangukia na kukupigia magoti Msamehe na endelea naye kwa mstakabali wa watoto wako.Watoto ni Muhimu zaidi kuliko kitu kingine,wao hawajui kitu lakini kwao HAKUNA KAMA Mama!
Pia Fahamu kuwa ASILIMIA KUBWA ya Wanawake ndivyo walivyo.Hata kama utamwacha na kumchukua mwingine,siku mambo yakikuharibikia mfano umekosa kazi hata huyo Mwingine anaweza kukufanyia vituko na kukuacha vile vile.
Ni viumbe dhaifu kabisa katika maswala ya ndoa.
Pili fahamu kwa kizazi chetu hiki ASILIMIA KUBWA ya Wanawake wanaolewa na PESA na Vitu alivyonavyo Mwanaume hawaolewi na MWANAMME SURUALI.Kwa hiyo vikiondoka vitu hivyo ndipo utakapowajua!
Mkuu ushauri wangu tena,kwa kuwa Mungu amekubariki akakupa kazi na huenda atakuongezea zaidi,USIMWACHE MKEO!
Muhusika alionekana JF Mara ya mwisho May 8,2015.
 
KANYIMBI

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
1,288
2,000
Miaka sita huyu jamaa atakuwa Kuna Jambo limemtokeaaa CYO bure bure hv
Inawezekana walishtukiwa hizo fedha wanazogawana nje ya Mshahara. Si ajabu kwa sasa yupo Jela. Kumbuka baada ya 2015 Rais alikuwa JPM na alidhibiti vitu kama hivi.

Ila kiukweli Mwanamke ukimnyanyasa Mwanaume aliyewahi kukufanyia jambo kubwa maishani mwako, hawezi kukupenda tena.
 
Pununkila

JF-Expert Member
Jan 7, 2021
230
500
Siku moja nisiyopenda kuikumbuka nilitwa ofisini kwa bosi wangu na kukabidhiwa barua ya kufukuzwa kazi
Hiyo ilikua ni baada ya uchunguzi wa miezi kdhaa wa kosa nililokua nimelifanya bahati mbaya. Miezi mitatu nyuma nilimuingizia pesa mteja kimakosa kwenye akaunti yake kiasi cha million mia tatu na hamsini ambazo alitakiwa kuwekewa Mteja mwingine halali kupata pesa hizo.

Kama humu ndani Kuna banker ataelewa nachokisema, kwamba makosa kama haya benki ni kawaida sana. Ukigundua kosa kama hili unawahi una reverse hiyo entry una m-credit anaetakiwa shida ni kama uliemwekea kimakosa akawahi kuzichukua ndipo yanakukuta yaliyonikuta mimi.

Baada ya kufukuzwa kazi mke wangu alibadilika kabisa
Nilishuhudia yafuatayo:-

(1) Alitamka mimi ni mjinga ndio maana nimefukuzwa kazi.

(2) Chake kikawa chake tu.

(3) Akawa anawaambia wazi watoto kuwa kitu fulani kimenunuliwa na yeye na sio mimi.

(4) Muda wa kurudi home ukabadilika sasa anarudi usiku mwingi, nampa kipigo cha nguvu anazira na kukimbilia kwao, kwenye usuluhishi anawaambia wasuluhishi kwamba mimi namuonea wivu kwa kuwa ana kazi mimi sina.

(5) Niliuza Gari zangu mbili ili nipate mtaji wa kufanya biashara hivyo nikawa sina Gari nilijua maadam wife ana Gari tutatumia wote maana hata yeye wakati hana Gari alikua akitumia magari yangu.

Kinyume na matarajio hakutaka kabisa niguse Gari lake mimi nikawa mtu wa miguu.Majirani wakawa wanashangaa mfumo wetu wa maisha.

(6) Life yetu ya bedroom ikawa imekufa no intimacy no love making nothing. Alianza kidogo kidogo leo mara aseme anaumwa, kesho kachoka, hadi mwezi unaisha. Nikaamua isiwe tabu nikaacha kuulizia tena, nae akawa amepotezea moja kwa moja.

Hata wazazi wangu aliwa mistreat sana wakawa hawaji tena kwangu, mama yangu akawa ananitumia vitu kwa njia basi kutoka nyumbani kama mchele, maharage, unga na kadhalika ili na mm nionekane nachangia.Wakuu siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Kila nilichojaribu kukifanya ili nijinasue kinakwama, nakuta mtaji wote unakata naanza moja.Ilikatika miaka minne nikiwa kwenye hali hii maana nilipata matatizo 2010. Mwaka Jana kuna Dada mmoja tulisoma wote primary school akaamua kunisaidia, huyu dada tulikutana Posta accidentally tukapeana contact
mimi nilishamsahau ila yeye alinikumbuka.

Baadae akaniunganisha na mumewe ambae ni HR manager kwenye shirika fulani, nikamwelezea ukweli wote na akaniingiza kaziniWife sikumwambia kuwa nimepata kazi akaanza kuona nakuja na mahitaji ndani, nikawa naondoka zangu alfajiri narudi usiku mwingi. Nikaita mafundi wakabomoa ukuta wote wa fensi uliokua umeoza waliiba sana cement wakati wa ujenzi ukajengwa upya, vitu vyote vilivyochoka ndani nikabadilisha. Wife alishangaa sana ila akashindwa kuniuliza maana hadi hapo tulikua hatuongeleshani zaidi ya salam za asubuhi na jioni tu basi.

Wana jf siwezi kuwaficha sehemu niliyopata naingiza hela Mara kumi ya ile kazi yangu ya benki, hii sikutokana na mshahara bali njia mbali mbali katikati ya mwezi kitengo chetu tupo wanne,hali ikiwa nzuri huwa tunagawana hadi laki mbili kila siku, kama hali ni mbaya tunagawana laki moja kwa siku hii ni mbali na ile tunayogawana mwisho wa mwezi kama million 3 each person mshahara ni mdogo tu ni laki saba tu kwa mwezi.Maana mshikaji alisema anaweza kuniingiza kazini ila kama mfanyakazi wa kawaida kwa kuwa benki nilifukuzwa hakukua na reference wala background check so nikaamua kufuta kwenye CV kuwa nilifanya bank.

Nimeanza mchakato wa talaka kupitia mwanasheria mmoja rafiki yangu, mwezi January mwaka huu amemwandikia barua ya kumtaarifu uamuzi huo na copy Ustawi wa jamii pia, baadae tutafungua shauri la talaka.Kinyume na matarajio yangu wife kwa kuwa alishañichoka na hakuna kinachoendelea kati yetu nilijua angekubali tu. Cha ajabu hivi sasa kupitia wazee wake wameniita kikao zaidi ya Mara 6 sasa ili tusuluhishe tofauti zetuKawa mpole sana, alidhan nitaendelea kuteseka milele

Wakuu sasa sipo nyumbani kwa hasira ya mambo aliyonitendea hivi sasa sipo nyumbani nimepanga upande wa nyumba nimeanza ujenzi ili nihamie. Kila siku lazima nipite kwa watoto niwaone ndo niondoke. Nimesimama njia panda, mm binafsi nilishaamua simtaki tena huyu mwanamke ila wazee na viongozi wa dini tunakoabudu wanasema turudiane juzi mke wangu alinipigia magoti tukiwa kikaoni kwamba nimsamehe, nifute kusudio la kuomba talaka mahakamani. Wazazi wangu hawataki kusikia kabisa neno msamahakwa matendo aliyotufanyia.

NB: Nimetaja kipato ili kuwapa mwanga na uelewa wa tatizo isichukuliwe vinginevyo

Nimesikia amepata matatizo kazini ila sina uhakika na taarifa hizo

Naomba ushauri wenu
Piga chini takataka hiyo....
 
clecla

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
800
1,000
Inawezekana walishtukiwa hizo fedha wanazogawana nje ya Mshahara. Si ajabu kwa sasa yupo Jela. Kumbuka baada ya 2015 Rais alikuwa JPM na alidhibiti vitu kama hivi.

Ila kiukweli Mwanamke ukimnyanyasa Mwanaume aliyewahi kukufanyia jambo kubwa maishani mwako, hawezi kukupenda tena.
JPM the best president ever...,lazima atakua yupo mtaani coz mzee hakutaka uhuni wa kugawa mamilioni ya pesa kwa mwezi ilhali Kuna walimu wanalipwa 2k
 
May 25, 2020
79
125
Mkuu Mimi nakushauri usimwache Mkeo! Maadamu amekuangukia na kukupigia magoti Msamehe na endelea naye kwa mstakabali wa watoto wako.Watoto ni Muhimu zaidi kuliko kitu kingine,wao hawajui kitu lakini kwao HAKUNA KAMA Mama!
Pia Fahamu kuwa ASILIMIA KUBWA ya Wanawake ndivyo walivyo.Hata kama utamwacha na kumchukua mwingine,siku mambo yakikuharibikia mfano umekosa kazi hata huyo Mwingine anaweza kukufanyia vituko na kukuacha vile vile.
Ni viumbe dhaifu kabisa katika maswala ya ndoa.
Pili fahamu kwa kizazi chetu hiki ASILIMIA KUBWA ya Wanawake wanaolewa na PESA na Vitu alivyonavyo Mwanaume hawaolewi na MWANAMME SURUALI.Kwa hiyo vikiondoka vitu hivyo ndipo utakapowajua!
Mkuu ushauri wangu tena,kwa kuwa Mungu amekubariki akakupa kazi na huenda atakuongezea zaidi,USIMWACHE MKEO!
Usimpotoshe mwenzio,HAKUNA mke hapo Ila ni Malaya kapata bahati ya kuolewa
 
KANYIMBI

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
1,288
2,000
Usimpotoshe mwenzio,HAKUNA mke hapo Ila ni Malaya kapata bahati ya kuolewa
Kweli mkuu, na ukichunguza sana utagundua wanaobahatika sana kuolewa huwa ni hawa wenye chembechembe za umalaya. Hivyo wanasababisha kuikosesha thamani taasisi ya Ndoa.
 
khamis kilo

JF-Expert Member
May 23, 2016
635
1,000
stori yako inafanana na ya kwangu, songa mbele mkuu huyo siyo wa kurudiana nae tena piga chini hiyo inaweza ikawa ndio njia yako ya mafanikio
 
TheCombination

Senior Member
May 21, 2021
140
250
JPM the best president ever...,lazima atakua yupo mtaani coz mzee hakutaka uhuni wa kugawa mamilioni ya pesa kwa mwezi ilhali Kuna walimu wanalipwa 2k
Wapumbavu wachache sana tena wasio na bahat kama ww na wenzako ndio mnaamin enzi za jpm hakukua na deals maofisin..You are very wrong.
Nimejenga nyumba enzi ya utawala wa jpm kwa hela za deal tena kwa siku nilikua naweza piga hata 900k ..sema ikikua sio daily inaweza hapen mara 2 au 3 kwa mwezi sik nyingine unapiga za kawaida kawaida tu daily.Serikal ya jpm ilijaa hadaa nying sanaa
 
BabaDesi

JF-Expert Member
Jun 30, 2007
4,299
2,000
...Mkuu, Mungu amekuwa Mwema sana kwako na kumfanya Mke wakp akuonyeshe Indiketa!!
Tafakari mkirudiana halafu baada ya Mwaka unapata tena matatizo Kazi na Unasimamishwa..kama sio kufukuzwa kabisa kazi.
Wewe ndio unamjua Mkeo. Sisi wengine ni Wapambe tu....jiulize na ujijibu kutoka ndani kabisa ya moyo wako
...yakikutokea tena kama yalivyokutoke, mkeo atafanya nini???
Jibu unalo mwrnyewe.... ....!!
 
clecla

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
800
1,000
Wapumbavu wachache sana tena wasio na bahat kama ww na wenzako ndio mnaamin enzi za jpm hakukua na deals maofisin..You are very wrong.
Nimejenga nyumba enzi ya utawala wa jpm kwa hela za deal tena kwa siku nilikua naweza piga hata 900k ..sema ikikua sio daily inaweza hapen mara 2 au 3 kwa mwezi sik nyingine unapiga za kawaida kawaida tu daily.Serikal ya jpm ilijaa hadaa nying sanaa
Asante ndugu,,,,Ila tatizo la Tz ni nchi iliyojaa unafiki uliokithiri,,,,,Kama hukuona kazi y JPM Sina Cha kuandika mie mkosa bahati Ila kwa calculation ya kawaidi mtoa maada kiwango Cha chini kabisa n 100k kwa siku n 3 ml kwa mwezi hapo toa mshahara,possible kila mwezi alikua anakusanya zaidi ya 5.8 million nje ya mshahara,,,ndo unataka ufananishe n ki900k chako Tena Mara 2 au 3 kwa mwezi....bro tuliza akili aiseeeeeee
 
goroko77

JF-Expert Member
Jul 9, 2019
1,171
2,000
Mtoa mada pengine amerestishwa in peace mnk Mara ya mwisho kuwa active Ni may 2015 mpk Sasa ajapost chochote Wala kukoment chochote huwenda mke kamrestisha in peace ili kuchukua Mali yake
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom